Shemeji anaharibu ndoa yangu

Pole sana mkuu kwa jambo hilo zito na lilokaa mahali nyeti haswa ukiangalia linakata kote yaani kwako na kwa dada yako! kwanza hongera hata kwa kuweza kuwa naye huyo mkeo mpaka muda huu na kupata uwezo wa kuomba ushauri, hiyo inaonyesha jinsi gani kweli unampenda kwa dhati lakini yeye ameshindwa kuwa mwaminifu na muadilifu! anakudhalilisha kwa kiasi kikubwa hicho, hata kama huyo shemejio ndo ana pesa No! hayo ni matusi makubwa!

Lakini ukikaa kimya na kusema unaogopa kwenye familia!! kumbuka mficha maradhi kifo umuumbua!!

Kama bado unampenda na unaweza kumsamehe na kuishi naye na kama mnao wadhamini wenu wa ndoa( wa uhakika) kaa nao na mkeo mliongelee hilo na pengine mtalimaliza hapo na pia kama mkeo ataonyesha kujutia na kutubu kutorudia tena!

Pili tafuta wazee ambao unaona huyo shemeji yako atawasiliza na anawaheshimu na ataweza kuwasikiliza, wanaweza kuwa ndugu katika familia zenu, kaeni chini muongelee na huyo shemeji aonywe kabisa ili asiendeleze ufilauni huo.

Mwisho nenda wewe na mkeo mkapime kama pengine kuna maambukizi yeyote. Kama mko poa endelea kuangalia mwenendo wa mkeo kama bado mrudishe kwao kama alivyosema mdau hapo juu! kwa kuwa atakuua nawe hautakuwa na mapenzi naye hapo!

Kikubwa mshrikishe Mungu kwa yote kwani yeye ndo kiongozi wa mambo yote katika maisha yetu (kama wewe ni muamini Mungu)

Pole sana Mungu akupe hekima, uvumilivu na maarifa katika jambo hili.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom