Shem utatapita pale petrol station..

sarikoki

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
1,194
721
Ilikua jumamosi asubui natoa gari getini, mara naskia mke wa jirai yangu ananiuliza Shemeji utapita pale Petrol satation?
Kwa sababu nilikua narudi njuma nilikua sijamuona ila yeye alikua kasimama pembeni ya geti kwa nje.
Nikajibu-Oooh za asubui shem...Hapana shemeji nilishaweka jana ila kwani kuna kitu unaitaji... akajibu Ndio shem naitaji Luku.
Nikamwambia haina shida ila mimi nitachelewa kurudi.. akanijibu hamna tatizo bado iko kidogo.
Kwenye mida ya saa mbili na nusu napiga honi ili geti lifunguliwe....mara naona simu inaita, napokea ni shem ananiambia umenipita hapa nyuma..nikamwabia ok ngoja nimpe Masai akuletee luku yako.
Ilipofika kwenye saa nne na nusu ivi bado niko naangalia TV , msg inaingia... ''shem naomba uje uniingizie, mimi nimeshindwa, na baba...... amewapeleka watoto shule Arusha niko mwenyewe, samahani kama nakusumbua''

Nikazima TV fasta nikaingia chumbani nikampigia wife simu nikamwambia nampenda na kumkiss good night,, mke wangu yuko Mbeya alienda kwenye msiba wa bibi yake. Nikazima simu nikasali , nikalala.
 
Sasa huoni kama kitendo ulichomfanyia jirani yako si cha kiungwana? Yeye alichokuwa anakuomba ni msaada wa kumuingizia Luku, lakini kwa sababu waswahili mawazo yenu siku zote yako kwenye mambo ya ovyo ovyo hasa ngono, ulihisi unaombwa kitu kingine hadi ukamfanyia jirani yako ukatili ambao huenda ulimsabisha alale gizani.
 
Hapana mawazo ya ngono hamna, ila niliepusha maneno... usiku nyumbani kwa jirani yangu na yeye hayupo ni noma
 
Kwa hiyo kesho yake ikawaje?maana hadithi imeishia njiani..
 
Dirty mind tu, yaani wewe ulishawaza unaenda kutongozwa, huyo jirani atakudharau sana kwa kumuhisi yeye ni Mal*ya
kama una nia kweli ya kuikimbia zinaa ungeenda na kuona anachotaka kufanya na hapohapo ungemkanya kwa maneo makali kabisa na sio kukimbia na kujidharirisha
 
  • Thanks
Reactions: ram
Sasa huoni kama kitendo ulichomfanyia jirani yako si cha kiungwana? Yeye alichokuwa anakuomba ni msaada wa kumuingizia Luku, lakini kwa sababu waswahili mawazo yenu siku zote yako kwenye mambo ya ovyo ovyo hasa ngono, ulihisi unaombwa kitu kingine hadi ukamfanyia jirani yako ukatili ambao huenda ulimsabisha alale gizani.

hapana mi nakubaliana na jamaa 100%, yeye anampenda mke wake na alikua anaogopa kuingizwa majaribuni..huwezi jua labda kashatoka kwa mganga kulikoroga sasa alikua anamsubiri jamaa aje.. kwani huyo mama hawezi kumuuliza mtu mwingine kwani yuko mwanaume mmoja tu mtaani hapo na je huyu jamaa angekua hayupo huyu mama angelala na giza? mianamke mingine kwa kutaka tu kuharibu ndoa za wengine nyambaafuuuu
 
Una matatizo ya Problem. Jirani kuomba msaada wa kuingiziwa luku kuna ubaya gani? kwa nini umkwepe? SHETANI HAKIMBIWI
 
hapana mi nakubaliana
na jamaa 100%, yeye anampenda mke wake na alikua anaogopa kuingizwa
majaribuni..huwezi jua labda kashatoka kwa mganga kulikoroga sasa alikua
anamsubiri jamaa aje.. kwani huyo mama hawezi kumuuliza mtu mwingine
kwani yuko mwanaume mmoja tu mtaani hapo na je huyu jamaa angekua hayupo
huyu mama angelala na giza? mianamke mingine kwa kutaka tu kuharibu
ndoa za wengine nyambaafuuuu

Na hiyo luku ina ufundi gani hasa mpaka iingizwe na wanaume tu? Huyo mama alikuwa na lake jambo. Mimi nampongeza mtoa mada maana heri nusu shari
 
wandugu eeh,ngojeni niwaaambie kitu nlichokiona mm kwa hii thread.huku MKE hayupo yupo ktk msiba MBEYAAA na kule BWANA hayupo kaenda ARUSHA kuwapeleka watoto shule.hii ni ngoma droo hapa. jamaa CD yake imeskip
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom