Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,639
- 47,716
Dah tumepangusa vumbi kanzu huku mikono ina masizi.
Kulitokea sintofaham kati ya broh na shem (mke wake). Baada ya ule ugomvi, shem akawa amenuna siku 3 mfululizo. Nimeenda kuwatembelea ndio broh ananimegea hiyo story.
Chanzo cha ugomvi ni kwamba kulitokea kutupiana maneno hadi kufikia kushikana mashati kati ya mke wa broh na Mama wa nyumba ya jirani kisa ni watoto. Broh alipotoka ndani kwenda kuamulia, kwa jinsi maelezo yalivyotoka ikaonesha wazi shem ndio alikuwa mkorofi. Aliwatenganisha na kumrudisha wife wake ndani.
Kufika ndani wife kafura why broh ajamzaba hata kofi yule mama wa jirani?
Kifupi mzozo wao ulianza hivyo yani.
Nkajaribu kumshauri broh, kuwa kwa jinsi wanawake walivyo, ni kwamba baada ya siku 3 za kununa, ameshamsamehe tayari ila inabidi broh ajiongeze/ajishushe kidogo ili mambo yarudi sawa.
Sasa juzi wakati tupo town na broh, tukapita mbele ya duka la vitambaa, khanga na vitenge. Nikamshauri amchukulie shem hata doti moja ya khanga. Katika kuchagua chagua, tukachagua khanga ina rangi ya dhambarau na doti nyingine rangi kama ya njano mpauko. After that tukapitia butcher akachukua nyama kilo na nusu.
Tukaagana broh akaelekea kwake na Mimi nikarudi kwangu.
Shem alifurahi sana kwa Kale ka parcel hasa doti za khanga. Lengo la kumchagulia zile rangi ni kwamba ndio ambazo anazipenda sana. Tofauti na matarajio, shem hakudeal na rangi, fasta akaenda kwenye maneno yaliyoandikwa.
Ile doti ya dhambarau iliandikwa "Kidomodomo chako ndio kimekuponza" wakati ile ya njano iliandikwa "Na bado"
Yani sina haja ya kuwaelezea reaction yake wakuu. Kifupi tumejaribu kuzima moto kwa petrol.
Kumbe uchaguzi wao hubase kwenye maneno na sio rangi.
MSISEME HAMKUAMBIWA.
Analyse
Sent using Jamii Forums mobile app