Shell ilivyoimiiki Nigeria, Je si ndivyo ilivyo kwa Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shell ilivyoimiiki Nigeria, Je si ndivyo ilivyo kwa Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rugemeleza, Dec 10, 2010.

 1. R

  Rugemeleza Verified User

  #1
  Dec 10, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nadhani mnaendelea kufuatilia kwa makini jinsi gazeti la Guardian la Uingereza linavyozidi kutuhabarisha jinsi nyaraka za kibalozi za Marekani zinavyosema kuhusu nchi mbalimbali. Moja ya habari iliyonigusa ni ile inayozungumzia jinsi Kampuni ya Shell ilivyopenyeza watu wake katika kila idara na ofisi ya serikali ya Nigeria. WikiLeaks cables: Shell's grip on Nigerian state revealed | Business | The Guardian

  Hii imenifanya nami niwaze na kuwazua jinsi ambavyo kampuni za madini zilivyojipenyeza na kuweka watu wao katika idara na wizara nyeti nchini mwetu. Vilevile zina watu wenye uhusiano na viongozi na mawaziri wa serikali wanaohusika na madini na sekta nyingine muhimu. Ukisikiliza kauli za viongozi hao utaona jinsi wanavyotetea mikataba ya shanga ambayo nchi yetu imesaini. Tunatakiwa tuamke na tupinge vitendo hivyo na haki ya nchi yetu katika raslimali zake.
   
 2. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #2
  Dec 10, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Unge......chagua CHADEMA mkuu hayo yote yangewezekana ila CCM mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Dec 10, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Rugemeleza,
  Kampuni za madini, hasa Barrick, haina haja ya kupenyeza watu wake katika idara mbalimbali kwa sababu wanajua kuwa mkuu wa nchi tayari yumo mfukoni mwao. Wakati wa zoezi la majadiliano ya tume ya Bomani, Sinclair, huyu ni CEO wa Barrick, aliwaandikia wana hisa wake kuwa hakuna litakalobadilika. Alikuwa ameshapewa rasimu ya mapendekezo ya tume ya Bomani hata kabla ya wabunge wetu kuyaona. Kuna wakati nilipata habari kuwa Sinclair alipokuwa Dar-es- Salaam alifanya kikao katika Ikulu pamoja na Kikwete na Joseph Kahama. Barrick wataendelea kupeta chini ya uongozi wa Kikwete.
   
Loading...