benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,503
- 2,980
Leo hii Jumatatu April 17 2023 Serikali imesaini mikataba na kampuni tatu za madini za Australi zinazohusisha uendeshaji wa uchimbaji wa Madini ya Kinywe (GRAPHITE) na madini adimu (RARE EARTH ELEMENTS) katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma na kushuhudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Moja kati ya mengi niliyoyanasa ni hili alilolisema Prof Palamagamna Aidan Mwaluko Kabudi, Mwenyekiti Timu Maalum ya Serikali ya Majadiliano ya Mradi.
Prof Kabudi ameeleza kuwa Katika kampuni zote mbili Serikali ya Tanzania ina hisa ya asilimia 16 ya hisa katika kampuni hizo isiyofifishwa, yaani (Non-Dilutable Free Carried Interest)
Prof Kabudi amesisitiza Tanzania ndio nchi nchi pekee ya Kiafrika kuingiza katika mikataba yake aina hii ya hisa na nchi nyingine zimekuwa zikijaribu kuweka kipengele hicho bila mafanikio
Kiufupi ni kwamba Kazi inaendelea na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia inaendelea kuweka historia.