Shekhe Ponda aachiwa huru

Shekhe Ponda aachiwa huru

Status
Not open for further replies.
Hatimae sheikh ponda yupo huru na vitu alivokua anadai ni vya kweli bakwata mupo
.hivi bakwata a.k.a ccm branch mupo kwa maslahi ya nani kiwanja cha waislam mumewauzia matajiri sasa ponda anakushtakini nyinyi
 
Kutoka kwake na iwe chachu Zaidi ya kudai haki na usawa kwa jamii yote ya Watanzania... Wale Masheik wote waliolawitiwa wafungue kesi ya madai... CCM na BAKWATA na Sasa Wamiliki wa Mkombozi Bank Hawaaminiki tena ndani ya Jamii...
 
Huyu yeye hakuingiliwa kinyume na maumbile?
 
Hatimae sheikh ponda yupo huru na vitu alivokua anadai ni vya kweli bakwata mupo
.hivi bakwata a.k.a ccm branch mupo kwa maslahi ya nani kiwanja cha waislam mumewauzia matajiri sasa ponda anakushtakini nyinyi

Leo ndani ya mahakama ya kisutu Shekh Issa Ponda ambae alikuwa na tuhuma ya kuhusishwa na vurugu za kiwanja cha Markaz cha Chang'ombe.Leo hii amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja cha nje baada ya kukaa muda mrefu ndani ya mahabusu pasina kupewa dhamana.Hivyo hali hii ya Shekh Ponda pamoja na wenzake kutolewa imejenga faraja ndani ya nyoyo za waislam kwa kuachiwa kwa shekh kipenzi cha umma pamoja na wengine 49 ambao wao wameachiwa huru.

which is which?!!!!!!
 
Hakuna cha ajabu Ponda kuachiwa huru. Alikuwa mtuhumiwa kama wengine tu.
 
Majambazi yako bungeni bwana wacha kabisa yanapiga mabilioni kwa suti na kalamu tuu
 
Sasa itabid tuifungulie kesi ya madai serikali hii ya mafisadi.
 
Sheikh Ponda akiwa ndani ya Mahakama Kuu akisubiri hukumu.
…

Sheikh Ponda akiwa ndani ya Mahakama Kuu akisubiri hukumu.[na Sheikh Ponda.
Askari akidumisha ulinzi mahakamani hapo.
magereza.
Sheikh Ponda akiwa ndani ya gari la magereza tayari kwa kurudi rumande.

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imemuachia huru aliyekuwa Katibu wa Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda Issa Ponda baada ya kuona hana hatia dhidi ya Kesi ya madai ya Ardhi ya Agrekanza inayomilikiwa na Afidhi Self iliyokuwa inamkabili.

Akisoma Mashtaka hayo Mwanasheria wa Serikali, Tumaini Kweka mbele ya Jaji, Augustino Shangwe alisema baada ya kupitia vifungu vyote mahakama imejiridhisha na kuona Sheikh Ponda hana hatia

yoyote na kumuachia huru tangu leo lakini katika hali ya kushangaza Sheikh Ponda amerudishwa rumande akisubiri kesi nyingine ya madai ya uchochezi, Mkoani Morogoro inayomkabili.
Kujua mengi yaliyojiri mahakamani hapo tembeleawww.globatvtz.com
(PICHA/HABARI : DEOGRATIUS MONGELA/GPL)

Nchi hii masheikh huozea jela kwa kesi za kuunga unga na za kubambikwa. Mara utaambiwa magaidi baadae wachochezi na mengineyo ya ajabu ajabu. Lakini maaskofu na wachungaji wao wanazitafuna kiulaini tu kama mabilioni ya escrow na mou na nyinginezo. Haya ipo siku...time will tell
 
yah baada ya kuona kuna mapadri yamepiga dill za kutosha inabidi kufanya ivyo kupunguza kasi kidogo.
 
Nimepata taarifa sasa hivi kuwa shehe Ponda kaachwa huru na mahakama. Naomba taarifa halisi wana jf.

Mahakama kuu yamuachia huru sheikh ponda leo
1.JPG

Sheikh Ponda akiwa ndani ya Mahakama Kuu akisubiri hukumu.…
1.JPG

Sheikh Ponda akiwa ndani ya Mahakama Kuu akisubiri hukumu.[na Sheikh Ponda.
5.JPG

Askari akidumisha ulinzi mahakamani hapo.magereza.
7.JPG

Sheikh Ponda akiwa ndani ya gari la magereza tayari kwa kurudi rumande.

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imemuachia huru aliyekuwa Katibu wa Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda Issa Ponda baada ya kuona hana hatia dhidi ya Kesi ya madai ya Ardhi ya Agrekanza inayomilikiwa na Afidhi Self iliyokuwa inamkabili.

Akisoma Mashtaka hayo Mwanasheria wa Serikali, Tumaini Kweka mbele ya Jaji, Augustino Shangwe alisema baada ya kupitia vifungu vyote mahakama imejiridhisha na kuona Sheikh Ponda hana hatia

yoyote na kumuachia huru tangu leo lakini katika hali ya kushangaza Sheikh Ponda amerudishwa rumande akisubiri kesi nyingine ya madai ya uchochezi, Mkoani Morogoro inayomkabili.
Kujua mengi yaliyojiri mahakamani hapo tembelea.

(PICHA/HABARI : DEOGRATIUS MONGELA/GPL)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom