Shekh sharif vs pastor wa loliondo......

Bila ya lengo la kuingilia wal kuathiri imani za watu, wote wana malengo yao, umaarufu na maslahi ($$$).
Yesu alipokuwa anaponya wagonjwa kwa miujiza na amri ya Mungu, alikuwa hadai "kitu kidogo". Hata waganga wengi wa jadi, wale wanaoponya kwa lengo la kutenda wema, hawadai kabla ya kutibu na kuponya. Wengi walikuwa (na ikiwabado wapo) wanakuambia "Ukishakupona ndio utaleta "ulichonacho". Ijapokuwa maisha yamepanda na nyakati zimegeuka, lakini tamaa zimezidi.

Hapa simsemi huyu pastor wa Loliondo (Mungu ambariki) kwani sijui anachokitenda zaidi ya kile ninachosoma hapa, ninakusudia waganga kwa jumla kama inavyoonekana nyakati hizi.
 
Wadau mnaokumbuka yale maajabu ya shekh sharif yule mtoto miaka ya tisini mtaweza kutoa mlinganisho yakinifu na huyu pastor aliyejitokeza huko loliondo.

Isije ikawa huyu ni yule yule mtoto sasa amekua,karudi kuwa mkirsto na anaendeleza maajabu yake.

Hakuna kitu kama hicho hawalingani hata kidogo Pastor ni oldman kabisa he is 76 years old,Shekh Sharif ni Mtoto,Pastor result hazichukui muda na matokeo hatangazi yeye,sisi wagonjwa ukipona tu jirani yako unamtonya akapone.
 
kuna posts wanasema ni 45 years.
 
Sheikh sharif ni sheikh na wa loliondo ni pastor,sheikh sharif yupo nikijana wa miaka 18,na pastor wa loliondo ana miaka zaid ya 45 ni tofauti kabisaaa.

Miaka 74 flani ,ni juu sana ya hyo 45
 
loliondo ni mchungaji anayetegemea nguvu za mungu kama musa jangwani alivyoambiwa na mungu atengeneze nyoka wa shaba yeyote atakaeng'atwa na nyoka akiangalia atapona shehe yeye aliongoza kwa kunukuu quran

Kama wengine wanavyosema ........................ crap!
 
Jamani mlio karibu muombeni pastor aiponye nchi yetu dhidi ya ufisadi uangamie na mafisadi woooote waangamie kwa kishindo!
 
nilikuja duniani naked na nitarudi nilikotokea naked.....thats it
Nimeipenda.
Ukapitia njia njia zote ya kwa baba itokeayo haja ndogo. Na njia nyingine kwa mama itokeayo haja ndogo.
Bora kuwa mtiifu kwa ALLAH S.W.
 
Wadau mnaokumbuka yale maajabu ya shekh sharif yule mtoto miaka ya tisini mtaweza kutoa mlinganisho yakinifu na huyu pastor aliyejitokeza huko loliondo.

Isije ikawa huyu ni yule yule mtoto sasa amekua,karudi kuwa mkirsto na anaendeleza maajabu yake.

ni watu tofauti kabisa
 
Sijui nia yako lakini haya ni maoni au mtazamo wangu kulingana na Sheikh Sharif na Mchungaji Ambilikile Mwasapile wa Loliondo.
Sheik Sharif yeye ni sheikh na huyu ni mchungaji wa KKKT aliyeestaafu
Sheikh Sharif alitumia mihadhara kuhubiri alichohubiri na wakati mwingine aliuponda Ukristo bali Mchungaj hafanyi mikutano ili kuvutia watu katika huduma anayoifanya
Sheikh Sharif hakuwahi kufanya huduma ya Uponyaji bali Mchungaji anafanya huduma ya uponyaji kwa kutumia miti shamba.
Sheikh Sharif aliwafuata watu mikoni na popote alipoenda bali Mchungaji hajamfuta mtu,kundi kwa ajili ya kutangaza huduma anayoitoa bali ni watu wanaenda huko
Sheikh Sharif baadhi ya watu walibadili imani zao kwa sababu ya alichohubiri bali kwa Mchungaji hakuna aliyebadilishwa imani yake kwa kupitia huduma ya uponyaji anayotoa.
Sheikh Sharif sijui umri wake kwasasa ila alipoanza alikuwa mtoto ambaye angepaswa kuhudhuria shuleni pia ila Mchungaji ni mtu mzima.
Hayo ndiyo machache niyaonayo
Sheikh Sharif VS Mchungaji wa Loliondo
 
Wadau mnaokumbuka yale maajabu ya shekh sharif yule mtoto miaka ya tisini mtaweza kutoa mlinganisho yakinifu na huyu pastor aliyejitokeza huko loliondo.

Isije ikawa huyu ni yule yule mtoto sasa amekua,karudi kuwa mkirsto na anaendeleza maajabu yake.

Pole sana Mr Cholera, Sheikh Sharifu ni mtoto iweje leo awe keshafanya kazi kama mchungaji na kustaafu, yule wa loliondo ni babu wa miaka zaidi ya 70. Grow up!!!
 
wiiizi mtupu.. hii ilishatokea huko Bukoba miaka ya 2005 ambapo kulikuwa na dada mmona huko kanyigo alikuwa anasema kaoteshwa na mungu kutibu Ukimwi. Nina mifano mbalimbali.. wengi wao waliokwenda na walikuwa wanaumwa wameshakufa.. yeye mwenyewe kashakufa kwa UKIMWI.. kuna mwingine anaitwa NDUKAI.. alikuja kasi sana.. akawapa dawa mmoja wao ni mzee samuel aliyekuwa mmiliki wa Biafra secondary.. alikuwa anaumwa HIV naye kafa. ndukai mwenyewe kashakufa tena kwa UKIMWI If it is a miracle, then thanks GOD.... Ila mimi imani yangu ni 13 per cent out of 100
 
Nimeipenda.
Ukapitia njia njia zote ya kwa baba itokeayo haja ndogo. Na njia nyingine kwa mama itokeayo haja ndogo.
Bora kuwa mtiifu kwa ALLAH S.W.

Najaribu kusoma hii post lakini siielewi can someone interprate. Esp. mod
 
Back
Top Bottom