Shein akataa tena ujumbe wa Cabinet


Good observation Mkuu. Baraza la Mawaziri ni chombo cha Kikatiba ambacho wajumbe wake wanapaswa kuilinda na kuihifadhi Katiba ya JMT waliyoapa kuilinda.

Interestingly, Rais wa Zanzibar ndiye Mjumbe pekee wa Baraza la Mawaziri ambaye hakuapa kuilinda Katiba ya JMT lakini wakati huo huo ni Mjumbe wa chombo cha kikatiba cha Katiba hiyo hiyo ambayo hawajibiki kwayo! Very interesting indeed. Bora hata amekacha kikao ina mantiki zaidi kuliko kuhudhuria.

UNAFAHAMU VEMA KATIBA YA JMT AU UNAPOTOSHA WATU? RAIS WA ZANZIBAR HUAPA KULINDA KATIBA YA JMT REJEA IBARA IFUATAYO YA KATIBA YA JMT

103.-(1) Kutakuwa na Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar ambaye ndiye atakuwa Rais wa Zanzibar na Mkuu wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na vile vile Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi la Zanzibar.
(2) Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kabla ya
kushika madaraka yake ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa Zanizibar
kiapo cha kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano, na
kiapo kingine chochote kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar

kinachohusika na utendaji wa kazi yake, kisha atashika na
kutekeleza madaraka hayo kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii
na Katiba ya Zanzibar, 1984.
 
Back
Top Bottom