Shein akataa tena ujumbe wa Cabinet | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shein akataa tena ujumbe wa Cabinet

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Taso, Jul 6, 2012.

 1. T

  Taso JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Kama ilivyo ada, Rais za Zanzibar leo tena amekataa kuhudhuria kikao cha baraza la Mawaziri kama mjumbe, kinyume na anavyotakiwa na Ibara ya 54 ya Katiba ya Tanzania.

  Tatizo, alikerwa alivyoitwa waziri. Ukiangalia kiti cha Rais wa Zanzibar kilivyopangwa (tupu) ni kama vile kiprotokali yeye yuko juu ya Waziri Mkuu manake anakalishwa karibu na Rais kuliko Waziri Mkuu. Lakini Ibara ya 54 inaanisha kwamba Rais wa Zanzibar hayumo katika mtiririko wa uongozi wa kikao cha Cabinet, Waziri Mkuu yumo, hivyo Rais wa Zanzibar anaona hapo anazugwa tu. Another "kiini macho cha Muungano," kwa kutumia maneno ya Tundu Lissu.

  Wakati umefika sasa kila upande uwe na cabinet yake wenyewe, Zanzibar na Tanganyika tukutane East African Community, ambapo kila nchi ni "dola huru yenye mamlaka yake kamili."
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  baraza lege lege
   
 3. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  wakati mwingine ni vema kuhushuhudia ukweli kwa vitendo. kudos kwa Rais wa Zanzibar Mh. Shein
   
 4. K

  Kiti JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 228
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Rais dahifu wa serikali dhaifu
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Basi kama hataki Uwaziri ngoja tumuite Mkuu wa Mkoa wa Zanzibar nafikiri hapo atafurahi hatakosa tena kikao
   
 6. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2012
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,964
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Raisi anatumia mafaili mekundu, wakuu maana yake nini?

  au maana yake ndani kuna siri nzito za serikali kuhusu madakitari?
   
 7. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,401
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Nyie mnaomtafuta Rais wa Zenji kwenye Baraza la Mawaziri naomba mfikirie hoja hizi;-
  - Rais wa Zenji aliapa kuilinda Katiba ipi kwenye kiapo chake, ya Zenji au ya JMT? Jibu: ni Katiba ya Zenji.
  - Katiba ya Zenji haitamki kuwa Rais wao ni sehemu ya Baraza hilo, analo Baraza lake huko kijijini kwao.
  - Katiba ya Zenji ilishaitangaza Zenji kuwa ni nchi kamili hadi leo.
  - Katiba ya JMT ilishavunjiliwa mbali na Katiba ya Zenji ya sasa.
  Halafu nyie bado mnakariri ibara ya 54 ya Katiba ya JMT. Namuonea huruma aliyeapa kuilinda Katiba ya JMT ambayo imevunjwa tayari.
   
 8. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,780
  Likes Received: 6,114
  Trophy Points: 280

  Good observation Mkuu. Baraza la Mawaziri ni chombo cha Kikatiba ambacho wajumbe wake wanapaswa kuilinda na kuihifadhi Katiba ya JMT waliyoapa kuilinda.

  Interestingly, Rais wa Zanzibar ndiye Mjumbe pekee wa Baraza la Mawaziri ambaye hakuapa kuilinda Katiba ya JMT lakini wakati huo huo ni Mjumbe wa chombo cha kikatiba cha Katiba hiyo hiyo ambayo hawajibiki kwayo! Very interesting indeed. Bora hata amekacha kikao ina mantiki zaidi kuliko kuhudhuria.
   
 9. a

  abousalah2 Member

  #9
  Jul 6, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera shein! kwa kufanya yale wazanzibar tunayataka! wajinga watazidi kuropokwa tu! mara zanzibar ni kijiji! mkoa! kujua kwingi mbele kiza! zanzibar hatushughulishwi na nchi yenye historia ya kubuni! mkapenda msipende zanzibar ni nchi na itaendelea kuwa nchi! sisi ndio walimu wao! na mabosi wao! zanzibar yetu kwa wazanzibar wote!
   
 10. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #10
  Jul 6, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Werema (AG) alimbeza Lissu lakini ukweli wa mambo muungano ni kiini macho
   
 11. m

  mkataba Senior Member

  #11
  Jul 6, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  anatoa maoni kwenye tume ya katiba ndo mana hakuwahi kufika.
   
 12. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #12
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Yule ni sawa na Katibu tarafa kwenye tarafa moja huko Shinyanga.........!!!
  Hawezi kuwa hata mkuu wa Mkoa!
  Labda ukichanganya na samaki.
   
 13. Mnama

  Mnama JF-Expert Member

  #13
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 1,651
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  duuu mgoma baridi.
   
 14. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #14
  Jul 6, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Maandishi yenye pink si ya kweli. Rais wa Zanzibar aliapishwa na Kikwete kuwa mjumbe wa baraza la mawaziri la JMT na aliapa kwa kutumia viapo vya mawaziri na hivyo kukubali kuilinda katiba ya JMT.
   
 15. M

  MKALIKENYA JF-Expert Member

  #15
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 133
  SHEIN anatimiza kile alichokisema LISSU jamani TANGANYIKA YETU ikirudi nitafurahije kwanza RAIS wake atakuwa RAIS wa awamu ya pili wa JAMHURI YA TANGANYIKA RAIS WA KWANZA NI NYERERE...jamani nasikiaje raha yani MWINYI,MKAPA,KIKWETE wote wanafutika kwenye historia sababu hakutajuwa TANZANIA na wo walikuwa MARAIS wa TZ............................yani natamani muungano uvunjwe ata kESHO yani hao marais wa TANZANIA na MAWAZIRI wakuu wake wala hatuwatengei yale mabilioni kwa ajiri ya WASTAAFU sisi TANGANYIKA YETU wastaafu ni NYERERE na KAWAWA na wote washafariki jamani TANGANYIKA itapendezaje.
   
 16. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #16
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Aiseee! Rais hajailinda katiba ya JMT akaacha ikavunjwa kwa kubadili ile ya Zanzibar. Sasa hili kosa si ndo la kumuondoa rais madarakani? Tufanye nini sasa? Wanasheria mtoe mwanga hapa.
  Shein yuko sawa kabisa kwa kulinda ile ya Zanzibar aliyoapa kuilinda sio ya JMT ambayo hakuapa kuilinda....nadhani Shein ni smart katika hili. JK, wake-up man..!
   
 17. kibai

  kibai JF-Expert Member

  #17
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 201
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kiukweli huu muungano kwa sasa let it go jamani, hatuhitaji uongo huu uendelee, kuna nchi kama burundi ni ndogo tu lakini nchi, we have alot to do, ngoja zanzibar nayo iende, hakuna haja, ila kweli kabisa, mi nawaonea huruma sana ndugu zangu wazanzibari huko kwenu ni padogo mno, mngefurahia kuzunguka katika li nchi kubwa kama tanganyika mkafaidika sana, bora mngesema hata mko tayari kuwa wilaya ya tanzania maana hata mkoa ni mkubwa sana, but mmeendelea kudai nchi, ili nini, mwende unoja wa mataifa kuhutubia? au hasa mtapata faida gani, kuwa n rais? its too costly kwenu, lakini nendeni na sisi kwakweli sasa tumechoka hii kitu haina maana kabisa. Watanganyika tujitokeze tudai katiba huru na hakuna haja tena ya muungano wa aina hii.
   
 18. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #18
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Wakati mwingine ni vema kufanya uchunguzi wa sababu zinazopelekea mkuu huyu kukosa vikao. Nijuavyo mimi, Rais Shein yuko ziarani nchini Uingereza
   
 19. T

  Taso JF-Expert Member

  #19
  Jul 6, 2012
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Na ndio maana ame plan safari kwa ajili ya watu kama nyinyi mseme "yuko ziarani Uingereza."

  Hii si mara ya kwanza au ya pili Shein kukwepa vikao vya Cabinet. Kutakuwa na vikao virefu vya Cabinet siku tatu mfululizo kuanzia jana, Shein alijua si rahisi kukwepa siku zote hizo, akapanga itinerary ya safari yenye mgongano na schedule ya Cabinet, yeye sio mjinga, ndio maana hata alipoondoka hawakusema Uingereza anaenda kufanya nini cha zaidi.

  Shein aliitisha press conference, very rare for Tanzanian presidents, aliitisha press conference mahsusi ku deny kwamba yeye sio waziri hata kama ni mjumbe wa Baraza, hiki kitu kinamuuma sana. Nani asiyejua Shein hafurahii huu mpango wa kiutwa Rais lakini yuko chini ya Makamu wa Rais? Yuko chini ya Waziri Mkuu? Anakwepa Cabinet makusudi.

  Dawa ni kila upande uwe na Cabinet yake, tukutane EAC, kila upande uwe dola huru yenye mamlaka yake kamili.
   
 20. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #20
  Jul 6, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Lakini katiba ya Zenj ni batili. Shukuruni tu kuwa tuna rais dhaifu anayeongoza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tungekuwa na rais makini mngekiona.
   
Loading...