Sheikh Yahya ashitakiwa Mahakama Kuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh Yahya ashitakiwa Mahakama Kuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Sep 29, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Wana-JF:
  Hii ni sehemu ya mwisho ya stori ya ‘Dr Slaa atabiriwa kifo’ katika Tanzania daima ya leo.

  ….Wakati huo huo Makama Kuu jijini Dar es Salaam imeombwa kumkamata na kumshitaki mnajimu Sheikh Yahya Hussein kwa kutoa kauli ya kitisho kwamba yeyote ambaye angeshindana na Rais Kikwete katika kinyang’anyiro cha kura ya maoni ya urais ndani ya CCM angefariki dunia ghafla.

  Taarifa za kuaminika zilizolifikia gazeti hili jana zilisema Paul Mhozya, ambaye ni mwalimu mstaafu wa taasisi ya elimu nchini, ndiye aliyewasilisha ombi hilo Mahaka Kuu akitaka Sheikh Yahya ahukumiwe kwa kukiuka sheria ya makosa ya ushirikina na uchawi ‘Witchcraft Act’ aliyodai inakataza kitendo cha mtu kutumia uwezo wake katika mambo ya kishirikina kutisha wengine.

  Ibara ya tatu ya sheria hiyo inasema: “Mtu yeyote ambaye, kwa kauli au kwa matendo anajipambanua kuwa na nguvu ya uchawi au kutishia kuitumia au kuegemea katika matumizi ya kichawi juu ya kitu chchote cha kichawiu au dhidi ya mtu yeyote, amefanya kosa.”

  Kesi hii inayogusa suala lililogubikwa na utata mkubwa ni ya pili kufunguliwa na Mhozya, baada ya kufungua kesi nyingine mwezi Julai mwaka huu akitaka jina la Rais Jakaya Kikwete liondolewe katika orodha ya wagombea urais kwa madai ya kukiuka matumizi mabaya ya madaraka na Katiba ya nchi.

  Kwa ombi hilo Sheikh Yahya ikiwa anaweza kupatikana na hatia anaweza kufungwa miaka saba jela au kulipa faini isiyopungua sh elfu moja.

   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Nadhani it's high time mtu huyu akapandishwa kizimbani kwa 'uchochezi'.
   
 3. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Mlinzi wa Rais apandishwe kizimbani ovyo ovyo, This is TZ my friend!!!
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,552
  Trophy Points: 280
  Thank you.
  Sheikh amekuwa akighilibu watu wengi sasa yamemfikaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu si ndo katuma majini kumlinda JK..
   
 6. M

  Msharika JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huyu atapandishwa mahakamani endapo jk atashindwa kura na kuzimika tena tu.
   
 7. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapandishiwi mtu mahakamani, kwa kosa gani? Yaani kutabiri kifo cha mpinzani wa mteja wake?
   
 8. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Pongezi kumfikisha mbele ya sheria fisadi wa amani, hakai kutishia uchawi waTZ mwanzo wanaThithiemu wakaogopa kuingia kwenye mchakato wa kinyang'anyiro cha U Prezida, leo tena kaja na kimbwaga kingine
  WaTZ tunaomba amani yeye kakalia uchawi uchwala
  MWAKA HUU HATUDANGANYIKI NG'OOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
   
 9. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Well ni vizuri tukiendelea kufuatilia thread hii tuone kama kweli atakamatwa. Kisheria maneno yake yanamfanya aweze kushitakiwa lakini kwa Tanzania hii sidhani.
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Hakuna Jaji/Hakimu wa kusikiliza shauri la mlinzi mkuu wa Rais ahaa ahaa ahaa.
   
 11. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,315
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Mpandisheni mahakamani kama hamkuliona jini disguising as yahaya hussein likileta kasheshe
   
 12. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mnataka kututoa katia mada ya uchaguzi,tumewashtukia hamna jipya!
   
 13. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,423
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Sipendi kweli kusikia jina la hili ****, sheikh yahaya.....so stupid and devilisH!
   
 14. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mlinzi wa rais!!!
  CCM bana, yaani secret service (ya TZ) hawatoshi tena?
   
 15. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,315
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Secret service ni visible lazima pia iwepo invisible service , na ndio hii ya majini ya shehe yahaya na huyu yupo tokea enzi za yule aitwaye Baba wa Taifa , NYERERE
   
 16. E

  Edo JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Hiyo faini ya elfu moja????
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  MTAAMBIWA LETENI USHAHIDI substancial!...sijui itakuwaje, wakati uchawi hauna ushahidi wa kuonekana na macho!Halafu anaweza akampiga juju hakimu atakayesogeza pua mahakamani kushughulikia kesi hiyo!
   
 18. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  hii ndo tz bana!
  mwivi wa kuku miaka mia,mwivi wa mabilioni na matumizi mabaya ya madaraka,kesi ndogo tu itaisha...ccm oyeeeeeee!!
   
 19. K

  Kishazi JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Mwaka huu watanzania wameamua kumuomba Mungu kisawasawa. Hivyo, hakimu atalindwa na Mungu aliye hai, jemedari wa vita, asiyeshindwa na nguvu za giza...!!!
   
 20. M

  Msharika JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mungu si binadamu aseme uongo, lazima tumpate kiongozi asiyeishi kwa ulinzi wa majini.
  Mungu tupe hekima.
   
Loading...