sheikh yahaya hussein arejea...

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,845
Mnajimu na mtabiri maarufu Sheikh Yahya Hussein akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jana mara baada ya kuwasili akitokea India alikoenda kwa matibabu. Ameamua kujitokeza baada ya uvumi kuenea kila mahali kwamba ameshafariki.

Katika mkutano huo Sheukh Yahaya amewashukuru JK, Rais mtafu Benjmani Mkapa na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP kwa kumchangia pesa kwa ajili ya nauli na matibabu ambapo amesema baada ya kufanyiwa nuchunguzi amekutwa na matatizo ya miguu.

Alitabiri pia kwamba katika uchaguzi ujao JK atashinda kwa kishindo zaidi ya ilivyokuwa mwaka 2005. Kulia ni mkewe Ketty, mama Mufti Junior.

picha na Mzee wa Sumo

...kwa hisani ya Blogu ya Issa Michuzi, ...namtakia kila la kheri na maisha marefu Sheikh Yahya.

...doooh, tulishaanza mtolea rambirambi hapa wallahi...ama kuishi kwingi!!!
 
Back
Top Bottom