Waraka wa Shura ya Maimamu Tanzania kuhusu kuachiwa Masheikh wa Uamsho

Sep 19, 2019
43
383
SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

*WARAKA WA KUTOLEWA UAMSHO

TAREHE 19 JUNI 2021*

UTANGULIZI:
Suala la kukamatwa Masheikh maarufu kwa jina la “Masheikh wa Uamsho” (2013), na kuachiwa kwao huru (2021), ni tukio kubwa Tanzania. Kwa sababu kadhaa zikiwemo za ubinadamu, haki na nafasi ya Masheikh katika imani na jamii, watu wa kada mbalimbali wamekuwa wakilijadili na kujihusisha na tukio hili kwa namna moja au nyingine.

Shura ya Maimamu Tanzania ikiwa ni Asasi kubwa ya kijamii iliyoshughulika na kadhia hii toka mwanzo mpaka mwisho, tumeona ni vizuri tukatoa Waraka huu kama mwongozo mdogo ili uwasaidie wale wanaotaka kushughulika na tukio hili kwa namna moja au nyingine.

MAENEO MAKUBWA:

Uongozi.
Masheikh wa Uamsho walikamatwa Unguja katika kipindi cha mchakato wa Katiba mpya ya Tanzania (Katiba ya Warioba). Katika mchakato huo viongozi hao wa jamii msimamo wao ulikuwa suala la katiba mpya liwe hatua ya pili bali hatua ya kwanza iwe ni kuitishwa kura ya maoni kuhusu Muungano uliopo kati ya Zanzibar na Tanganganyika.

Katika mikutano mikubwa ya hadhdhara waliyoifanya walikuwa wakikusanya saini za Wazanzibari za kuthibitisha hoja yao kitaifa. (Katika mikutano hiyo ya Unguja Shura ya Maimamu Tanzania iliwakilishwa na Sheikh Ponda Issa Ponda).

Katika mazingira hayo ndipo Masheikh hao walipokamatwa na vyombo vya dola wakafikishwa Mahakamani na kusomewa mashtaka ya uharibifu wa mali. Hatimaye waliletwa Tanganyika na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi.

Aidha muda mfupi baada ya kukamatwa Masheikh wa Uamsho, Serikali ilimkamata Sheikh Ponda Issa Ponda na kumfungulia Mashtaka ya uchochezi na uharibifu wa mali. Tukio hilo liliratibiwa na Serikali baada ya Sheikh Ponda kuzuwia zoezi la Bakwata la kuuza ardhi ya East African Muslim Welfare Society iliyokusudiwa kwa mradi mkubwa wa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Waislamu Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Hatimaye Masheikh wa Uamsho na Sheikh Ponda waliwekwa pamoja katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam (wakiwa na kesi tofauti).

Baada ya matukio hayo ndipo kikao cha Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania kilipo wateuwa Shura ya Maimamu Tanzania kushughulikia mashauri hayo kitaifa.

Huduma
Waliokamatwa walikuwa wanapaswa kupewa huduma muhimu kama chakula, matibabu madogo na makubwa. Vilevile kuwatembelea na kujua hali zao kila siku na kushughulika na familia zao. Katika hili Waislamu na wasio Waislamu walichangia upatikanaji wa mahitaji yao. Shura ya Maimamu kila siku ilipeleka gerezani chakula cha wastani wa chini wa Shilingi laki tatu (300,000), katika magereza ya Dar es Salaam. Walifanya hivyo toka mwaka (2013), mpaka mwaka huu (2021). Fedha hizi zilitolewa kwa moyo wa huruma na waumini katika Misikiti mbalimbali Bara na Visiwani pamoja na watu wengine walioguswa na moyo wa ubinadamu.

Sheria
Wanasheria wazalendo walijitokeza kuwatetea Sheikh Ponda Issa Ponda na Masheikh wa Uamsho. Miongoni mwa hao ni Mawakili Juma Nassoro, Abubakar Salim, Yahya Njama na Batholomeo Tarimo. Wengine ni Ignus Punge, Ubaid Hamidu, Abdulfatah Abdallah, Daimu Khalfani, Abdallah Juma, Husein Hitu na Jeremia Mtobesiya.

Mawakili hawa ambao ni wafanyabiashara katika eneo la uwakili walijitolea kutetea kesi hizi bure toka mwanzo mpaka mwisho. Waliamini pamoja na ujira watakaoupata kwa Mwenyezi Mungu lakini viongozi hao wana haki ya kuwakilishwa mahakamani ambayo ni haki ya Kikatiba.

Katika hatua hizo za kisheria Shura ya Maimamu pia imekuwa ikiwasiliana na ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali DPP mara kwa mara kujadili haki na mustakbali wa mashauri hayo.

Kuihusisha jamii
Katika kuwafanya Watanzania waone upogo katika utekelezaji wa sharia Tanzania na kulitumia tukio hili kusukuma mabadiliko ya kisheria, Shura ya Maimamu imepata kuketi na watu wa kada mbalimbali kushauriana nao. Miongoni mwa hao ni Wabunge, Wanasheria, watu wa Haki za Binadamu na vyombo vya Habari.

Mahakama
Sheikh Ponda alishinda mashauri yote pamoja na rufaa zilizokatwa dhidi yake na Serikali. Aidha kesi ya Masheikh wa Uamsho wao waliendelea kukaa gerezani Segerea na baadae kuhamishiwa Ukonga kwa zaidi ya miaka minane. Katika kipindi chote hicho Serikali imekuwa ikidai inatafuta ushahidi.

Hatimaye mwaka huu (2021), mwezi wa Mei shauri lilianza kusikilizwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam. Katika mpambano mkali uliojitokeza kati ya Mawakili kumi na moja wa serikali wakiongozwa na DPP (Biswalo Mganga wakati huo), na Mawakili tisa wa utetezi wakiongozwa na Wakili Juma Nassoro, Masheikh walishinda mashitaka kumi na nne (14) kati ya ishirini na tano (25), yaliyofunguliwa dhidi yao.

Mashitaka hayo (14), walishinda mara mbili. Kwanza walishinda Mahakama Kuu halafu walishinda tena Mahakama ya Rufaa Tanzania baada ya Serikali kukata rufaa dhidi yao huko. Baada ya matokeo hayo hatua iliyokuwa inafuatia ni upande wa Serikali kuleta mashahidi Mahakamani kwa yale Mashitaka kumi na moja (11), yaliyobaki dhidi ya Masheikh.

Katika mazingira hayo ndipo Serikali badala ya kuleta mashahidi wameamua kuiondoa kesi wakisema “Serikali imeona haina haja ya kuendelea na Shauri hili”. Shauri hili lilitegemewa kukamilika ndani ya mwezi huu wa Juni na kwa kuwa Mahakama ilikuwa inatenda haki, Masheikh na umma wa Watanzania walijawa na matumaini makubwa sana ya kuishinda Serikali katika kesi hii ya mwisho kwa Masheikh.

Endapo shauri hili lingemalizika Mahakamani Masheikh wangekuwa wamesafishwa dhidi ya tuhuma za ugaidi zilizokuwa zinaelekezwa kwao pasi na ushahidi wowote.

Kitaifa
Katika kipindi cha mashauri hayo yaliyodumu kwa zaidi ya miaka minane Shura ya Maimamu imekuwa ikiandika na kuchapisha kwa namna mbalimbali. Imekuwa ikipaza sauti kuhusu tatizo la mfumo wa sheria Tanzania. Miongoni mwa mambo yaliyolalamikiwa na Shura ni utendaji wa vyombo vya dola wa kumtuhumu mtu na kumkamta bila ya ushahidi. Lingine ni mtu kufikishwa Mahakamani bila ya ushahidi. Na mtu kuwekwa mahabusu kwa muda mrefu bila shauri lake kuzungumzwa kwa madai ya upande wa jamhuri kutafuta ushahidi.

Katika namna ya kulifanya jambo hili lipate uungwaji mkono wa kitaifa na kuleta msukumo mkubwa kwa viongozi wenye mamlaka ya kurekebisha hali hiyo, Shura ya Maimamu iliamua kulifanya moja ya ajenda kuu katika kampeni za kisiasa za uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani wa mwaka 2020.

Katika uchaguzi huo Katibu Mkuu wa Shura Sheikh Ponda Issa Ponda alitumia jukwaa la kampeni za urais kuzungumzia suala la kukamatwa na kuwekwa ndani Masheikh kwa muda mrefu kwa madai ya kutafuta ushahidi. Katika jukwaa hilo hoja yake pia ilikaririwa na mgombea urais wa Chama cha CHADEMA.

Aidha baada ya Serikali ya awamu ya sita kuingia madarakani Shura ya Maimamu (kupitia jukwaa mama la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania), ilimuandikia Mkurugenzi wa Mashtaka DPP, ikisisitiza wito wao wa marekebisho ya mfumo huo. Barua hiyo Kumbukumbu Na. JTKT-MMT/1/21, yenye maudhui mazito ilinakiliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania. Wengine waliopelekewa nakala ya barua hiyo ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Jaji Mkuu wa Tanzania, Jaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanziba na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Wengine ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri wa Katiba na Sheria Tanzania, Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali ya Zanzibar, Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania, Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa.

Katika muktadha huo hivi sasa tunashuhudia Mkurugenzi mpya wa Mashtaka DPP, akifanya zoezi kubwa la kukagua Magereza na kufuta kesi zote zisizokuwa na ushahidi. Shura inatazama zoezi hilo kama hatua muhimu kitaifa na tunaamini Shura ya Maimamu Tanzania inamchango mkubwa katika hilo.

Hitimisho
Katika suala la kuachiwa Masheikh wa Uamsho kuna watu wanaotamani kuzungumza chochote, kuandika chochote, kushukuru, kukosoa, kuomba dua, kutoa pongezi na mengine. Tunaamini kwa Waraka huu utawasaidia sana kama Mwongozo katika kufikia azma yao kwa usahihi.

Kwetu sisi Shura ya Maimamu kwanza tunawapongeza wale waliochanga vijisenti vyao kwa miaka minane wakiwahudumia Masheikh wao kwa chakula na matibabu. Pili tunawapongeza wale waliodumu wakiwaombea dua kwa dhahiri na kwa siri. Tunawapongeza wale waliokuwa wanaacha shughuli zao na kwenda mahakamani bila ya kujali adha, tafrani za mbwa na virungu vya polisi. Tunawapongeza watanzania wengi wa dini mbalimbali wakiwemo watu wa siasa waliokua wakiandika na kutoa wito wa haki kutendeka kwa viongozi hao.

Tatu tunawapongeza wanasheria Juma Nassoro, Abubakar Salim, Daimu Halfan, Ubaid Hamidu, Abdulfatah Abdallah, Abdallah Juma, Hussein Hitu na Jeremiah Mtobesya waliojitolea kwa hali na mali wakapambana kwa miaka minane na wakawapa ushindi Masheikh katika kesi nzito ya ugaidi iliyokuwa inawakabili.

Na mwisho tunawapongeza wale wote waliopaza sauti katika kipindi ambacho mtu hakuweza kufanya hivyo ila yule aliyekuwa tayari kuuza nafsi yake kwa thamani ya kusema kweli.

UMETOLEWA NA

IDARA YA HABARI
SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

0713118812
0755 933 008
 
Mbona hiyo shura ya Maimamu haijaelezea jinsi yao Masheikh walivyoasisi umwagiaji wa tindikali kwa watalii wanaoletea kipato Zanzibar?

Mbona hawajaeleza jinsi walivyommwagia Padri tindikali?

Mbona hawajeleza walivyoratibu mauaji ya watalii watatu Mombasa kwa kushirikiana na Masheikh magaidi wa Mombasa?

Mbona hawajaeleza kinagaubaga juu ya Uchochezi waliokuwa wanaleta juu ya Waislam wa BAKWATA na Wakristo?

Mkileta nye nye nye...Fimbo chaapaa!!

Mtafurahi wenyewe yaani
 
Mbona hiyo shura ya Maimamu haijaelezea jinsi yao Masheikh walivyoasisi umwagiaji wa tindikali kwa watalii wanaoletea kipato Zanzibar?

Mbona hawajaeleza jinsi walivyommwagia Padri tindikali?

Mbona hawajeleza walivyoratibu mauaji ya watalii watatu Mombasa kwa kushirikiana na Masheikh magaidi wa Mombasa?

Mbona hawajaeleza kinagaubaga juu ya Uchochezi waliokuwa wanaleta juu ya Waislam wa BAKWATA na Wakristo?

Mkileta nye nye nye...Fimbo chaapaa!!

Mtafurahi wenyewe yaani
Boss Una Uhakika na Kauli zako???
 
Mbona hiyo shura ya Maimamu haijaelezea jinsi yao Masheikh walivyoasisi umwagiaji wa tindikali kwa watalii wanaoletea kipato Zanzibar?

Mbona hawajaeleza jinsi walivyommwagia Padri tindikali?

Mbona hawajeleza walivyoratibu mauaji ya watalii watatu Mombasa kwa kushirikiana na Masheikh magaidi wa Mombasa?

Mbona hawajaeleza kinagaubaga juu ya Uchochezi waliokuwa wanaleta juu ya Waislam wa BAKWATA na Wakristo?

Mkileta nye nye nye...Fimbo chaapaa!!

Mtafurahi wenyewe yaani
Sio kwamba wewe ndiyo utafurahi!!! Kama Serikali imekosa ushahidi ulikuwa wapi kwenda kutoa ushahidi!
 
Vita ni vita mura:

"Shura ya Maimamu kila siku ilipeleka gerezani chakula cha wastani wa chini wa Shilingi laki tatu (300,000), katika magereza ya Dar es Salaam. Walifanya hivyo toka mwaka (2013), mpaka mwaka huu (2021). Fedha hizi zilitolewa kwa moyo wa huruma na waumini katika Misikiti mbalimbali Bara na Visiwani pamoja na watu wengine walioguswa na moyo wa ubinadamu."

Wapigania haki hapa pana funzo zito!
 
Mbona hiyo shura ya Maimamu haijaelezea jinsi yao Masheikh walivyoasisi umwagiaji wa tindikali kwa watalii wanaoletea kipato Zanzibar?

Mbona hawajaeleza jinsi walivyommwagia Padri tindikali?

Mbona hawajeleza walivyoratibu mauaji ya watalii watatu Mombasa kwa kushirikiana na Masheikh magaidi wa Mombasa?

Mbona hawajaeleza kinagaubaga juu ya Uchochezi waliokuwa wanaleta juu ya Waislam wa BAKWATA na Wakristo?

Mkileta nye nye nye...Fimbo chaapaa!!

Mtafurahi wenyewe yaani

padri alikuwa muuza unga akawazulumu wenzao
 
Mbona hiyo shura ya Maimamu haijaelezea jinsi yao Masheikh walivyoasisi umwagiaji wa tindikali kwa watalii wanaoletea kipato Zanzibar?

Mbona hawajaeleza jinsi walivyommwagia Padri tindikali?

Mbona hawajeleza walivyoratibu mauaji ya watalii watatu Mombasa kwa kushirikiana na Masheikh magaidi wa Mombasa?

Mbona hawajaeleza kinagaubaga juu ya Uchochezi waliokuwa wanaleta juu ya Waislam wa BAKWATA na Wakristo?

Mkileta nye nye nye...Fimbo chaapaa!!

Mtafurahi wenyewe yaani
Wakati mwengine uwe unaficha ujinga wako.
 
Wakati mwingine mnapaswa muone aibu, hata mnyama kuna wakati anaweza kujizuia jambo baya kwa kuogopa macho ya watu.

Miaka 8 sasa Serikali ilikuwa inatafuta ushahidi, bado imeshindwa kithibitisha tuhuma dhidi ya Masheikh hao. Tungekuona wa maana sana kama ungepeleka ushahidi huo mapema ofisi ya DPP ili wafungwe au wanyongwe. Hapo ungekuwa umelitendea taifa jambo jema.

Watu wana pewa tuhuma za uongo, wanateswa. Bado unaona ni jambo jema... Kwa kukosa kwenu kithibitisha tuhuma zao mmebaki kila mkiamka Padri walimwagia tindikali. Ni kweli hamjui tukio la Kiongozi wa dini na kwa nini alimwagiwa tindikali? Au mnaamua kuficha huo uovu?

Mwenyezi Mungu amekuaibisheni sana katika tukio hili, ukiona mtu mzima kavuliwa nguo kisha akasimama na kuanza kukimbia jua huyo ni kichaa namba 1
Mbona hiyo shura ya Maimamu haijaelezea jinsi yao Masheikh walivyoasisi umwagiaji wa tindikali kwa watalii wanaoletea kipato Zanzibar?

Mbona hawajaeleza jinsi walivyommwagia Padri tindikali?

Mbona hawajeleza walivyoratibu mauaji ya watalii watatu Mombasa kwa kushirikiana na Masheikh magaidi wa Mombasa?

Mbona hawajaeleza kinagaubaga juu ya Uchochezi waliokuwa wanaleta juu ya Waislam wa BAKWATA na Wakristo?

Mkileta nye nye nye...Fimbo chaapaa!!

Mtafurahi wenyewe yaani
 
Sina hayo Mamlaka wala muda

Funzo walilopata linatosha
Akili zako fupi sana wewe. Sasa Kama kweli ulikuwa na uhakika Hawa masheikh wamefanya kosa Hilo wewe ulikuwa wapi wakati watu wanatafuta ushahidi? Umeshindiliwa mapropaganda na wewe ukajaa mzima mzima.
Mahakama imewaachia kwa vile hawana hatia ila wewe ndo bado hujaridhika yan au siyo. Muachage kurukia mambo msiyoyajua.
 
Serikali imeamua kuachana na hiyo kesi.............maana yake mahakamani wangepigwa mueleka mkubwa sana,sasa iangalie jinsi gani watawalipa fidia ya dhulma hii kwa muda wa miaka tisa,kuna waliopoteza mali zao na kuharibiwa kabisa mifumo ya kimaisha kiuchumi,kijamii,kisaikolojia pia....kibinadanu hawa masheikh walipwe chochote familia zao zimetaabishwa sana.
 
Naomba kujua maana ya neno SHURA au neno lenye maana sawa na SHURA au ni JUMUIYA??
 
Back
Top Bottom