Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,498
Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda amesema;
"Mwezi Oktoba mwaka huu nchi yetu inatarajia kufanya uchaguzi mkuu, katika kulizungumzia jambo hilo nyeti tumeona ni vyema tukayarejea maneno muhimu tulioyatoa katika Baraza la Eid lililopita Machi 31, 2025 ya kwamba kauli ya CHADEMA ya 'No Reforms, No Election' na ile ya ACT Wazalendo ya kupinga uchaguzi wa siku mbili kule Zanzibar, zinaakisi malalamiko ya uchaguzi 'mbovu' kama ule wa serikali ya mitaa 2019, uchaguzi mkuu 2020, na uchaguzi wa serikali za mtaa 2024"
"Ukiachilia mbali vyama hivyo, viongozi mashuhuri na wengine wastafu wa serikali, wanasheria na viongozi wa dini kwa nyakati tofauti wamekiri kwamba chaguzi hizo zilikua na kasoro kubwa mno, wengi wao wanasema kasoro hizo ni kubwa kwa kiasi cha kusema hapakuwa na uchaguzi kwa kuwa mfumo uliotumika unapoka haki za wananchi za kidemokrasia, haki ya kuishi na kuhatarisha usalama wa taifa, tunatoa wito kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuitisha wadau wawakilisha wa umma kujadili utekelezwaji wa makubaliano ya msingi ya mfumo wa uendeshwaji wa uchaguzi yaliyofikiwa kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu Oktoba 2025"
"Aidha tumelipokea kwa mstuko mkubwa tamko la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuliagiza Jeshi la Ulinzi (JWTZ) lijiandae kwa uchaguzi mkuu Oktoba 2025, mshtuko wetu ni kwa kuwa suala la uchaguzi ni la kiraia na jeshi halihusiki na masuala ya kiraia, kumbukeni kumekuwa na tuhuma kuhusu Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama kudaiwa kuingilia masuala ya chaguzi zilizopita lakini pamoja na hayo kwa mujibu wa Katiba ya nchi wao ndio weyenye dhamana ya kulinda uchaguzi wa kiraia, jambo muhimu kwa Rais Samia ni kuzuwia kile wanachokiona wananchi, majeshi hayo kushiriki siasa"
"Aidha, kwa heshima kubwa tunatumia fursa hii kumuomba Rais Samia Suluhu Hassan atoe ufafanuzi wa kuwahakikishia Watanzania na Dunia kwa ujumla kwamba Jeshi la wananchi (JWTZ) litaendelea na wajibu wake wa kulinda mipaka ya nchi tu na kamwe halitaingilia uchaguzi mkuu ujao na mwingine, Watanzania wengi kupitia viongozi wa kijamii, kidini, makundi ya harakati na vyama vya siasa wamekua wakilalamikia madhila na ukandamizaji unaotokana na mfumo huo wa siasa tuliouna huko nyuma, hivyo"