Sheikh Ponda kwanini unakubali kutumiwa vibaya?

Juakalee

Member
Oct 3, 2018
57
95
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekuwa katika maanadalizi ya Uchaguzi Mkuu kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kurekebisha kanuni, uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuandaa maadiili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Katika shughuli hizo na nyinginezo Tume imewashirikisha wadau wake wote wakiwemo wadau wakuu ambao ni Vyama vya Siasa.

Sasa Sheikh anapoibuka na hoja mfu kama hii anatia aibu. Wadau walioshirikishwa ni pamoja na viongozi wa Dini wakiwemo hao wa Shura ya Maimamu.

Kwanini Sheikh anaupotosha umma?

Uchaguzi Mkuu: Waraka wa Waislam waibana serikali
 
sanshinda

Member
Sep 25, 2017
69
125
Hii Tume sasa imekuwa kama punching bag, yani kila anayeibuka huko anapiga ngumi. Wengine hata hawajui kwanini wanafanya hivyo. Yani anajikuta tu ameasharusha ngumi. Ila cha msingi hapa watu waache kulialia, Tume ni ile ile iliyowatawaza wapinzani waliokuwapo kwenye Bunge lililopita kwa wingi na madiwani pia. Kwa hiyo tuache visingizio tufanye siasa zenye staha.
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
100,327
2,000
Acha kuonyesha UJUHA wako hadharani. Sheikh Ponda ni akili KUBWA kuliko wewe.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekuwa katika maanadalizi ya Uchaguzi Mkuu kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kurekebisha kanuni, uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuandaa maadiili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Katika shughuli hizo na nyinginezo Tume imewashirikisha wadau wake wote wakiwemo wadau wakuu ambao ni Vyama vya Siasa.

Sasa Sheikh anapoibuka na hoja mfu kama hii anatia aibu. Wadau walioshirikishwa ni pamoja na viongozi wa Dini wakiwemo hao wa Shura ya Maimamu.

Kwanini Sheikh anaupotosha umma?

Uchaguzi Mkuu: Waraka wa Waislam waibana serikali
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
31,954
2,000
Hii Tume sasa imekuwa kama punching bag, yani kila anayeibuka huko anapiga ngumi. Wengine hata hawajui kwanini wanafanya hivyo. Yani anajikuta tu ameasharusha ngumi. Ila cha msingi hapa watu waache kulialia, Tume ni ile ile iliyowatawaza wapinzani waliokuwapo kwenye Bunge lililopita kwa wingi na madiwani pia. Kwa hiyo tuache visingizio tufanye siasa zenye staha.
Nitajie mpinzani aliyetangazwa toka awamu hii imeingia madarakani, na kilichokuwa kinaendelea kwenye vituo vya kura wananchi tumeona kwa macho yetu. Hivi unadhani watu hawajui wanaoongea nini, na malalamiko ni nini? Ukweli ni ukweli hata itumike nguvu kiasi gani, ukweli huo hauondolewi kwa mtutu wa bunduki.
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
1,325
2,000
Mambo HADHARANI.

Haya Sasa,sheikh Kundecha amejitenga na huo WARAKA wa KIZUSHI.....

Tunamueleza Sheikh wetu Ponda kuwa aendelee na harakati zake lakini si kujificha nyuma ya WANASIASA.......

Angalia Sasa alivyoaibika......

Tume hiihii ndiyo iliyomfanya Zitto Kabwe awe mbunge......

Tume hiihii ndiyo iliyowaingiza waliokuwa wabunge wa CUF bungeni.....

MANENO BATILI HAYAANDIKWI KWA WINO WA DHAHABU.

Think thrice
 
Chosen man

JF-Expert Member
Dec 30, 2017
208
250
Wewe mleta post ndiyo unatumika vibava,utamlinganisha Ponda na Mataga kama wewe,ponda anajitambua toka wewe ukiwa tumboni mwa mama yako,yeye hatumiki kama Bakwata koloni la CCM.
Ponda anajitambua sana ila bahati mbaya amezungukwa na waislamu wanafiki wengi. Wengi wao wameigeukia dunia na kuipa akhera kisogo.
 
mwarobaini_

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
655
1,000
Acha kuhadaa watu, tume iliyopo sio huru, hata ukimuuliza rais mstaafu mzee Mkapa atakwambia hilo. Ushahidi ni upumbavu uliofanyika kwenye chaguzi za marudio, sote tuliona. Labda ninyi wapumbavu wachache mnaofaidika na udhalimu wa tume hiyo ya CCM ndio mnaona iko huru.

Sheh Ponda anatetea haki, nothing more nothing less.
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
25,850
2,000
Mambo HADHARANI.

Haya Sasa,sheikh Kundecha amejitenga na huo WARAKA wa KIZUSHI.....

Tunamueleza Sheikh wetu Ponda kuwa aendelee na harakati zake lakini si kujificha nyuma ya WANASIASA.......

Angalia Sasa alivyoaibika......

Tume hiihii ndiyo iliyomfanya Zitto Kabwe awe mbunge......

Tume hiihii ndiyo iliyowaingiza waliokuwa wabunge wa CUF bungeni.....

MANENO BATILI HAYAANDIKWI KWA WINO WA DHAHABU.

Think thrice
Umepotea kweli wewe, hii tume chini ya Magu ni tofauti na tume hii chini ya JK so kuondoa utashi binafsi wa mtu ndo imahitajika tume iliyo huru
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
1,325
2,000
Umepotea kweli wewe, hii tume chini ya Magu ni tofauti na tume hii chini ya JK so kuondoa utashi binafsi wa mtu ndo imahitajika tume iliyo huru
Tume.....chini ya viongozi wawili

Tume......na utashi wa mtu

Plz nifafanulie vizuri
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,019
2,000
kurekebisha kanuni, uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuandaa maadiili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
This is nonsense and absurd, wanaboresha kwa kuleta kanuni kandamizi kwa upinzani while favouring CCM! Unjust rules aimed at oppressing your opponents!
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
3,909
2,000
Mimi ni Mkatoliki kindakindaki! Ila ninaikubali sana na kuiheshimu misimamo ya Sheikh Ponda, Askofu Mwamakula na Askofu Bagonza hasa linapokuja suala la kuipigania HAKI!

Nina imani Masheikh wa Bakwata, Maaskofu wa Katoliki, Lutherani, Anglican, wale wanaojiita mitume na manabii, nk. wana cha kujifunza kwa kuendekeza kwao unafiki, uoga na uccm! badala ya kusimama kwenye ukweli.
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
1,325
2,000
Yaan Uhuru wa tume inategemea na Raisi aliepo madarakani kama ni mdemokrasia au.
Well,

Tafsiri yenu ya demokrasia huwa inafikirisha....
Hapo juu umemvika mh.JK huo udemokrasia...

Ila japo wewe hujayasema haya niyasemayo hapa chini lakini nakukumbusha TU;

Waumini wenzako wa hiyo "demokrasia" wanasema pamoja na JK kuyatumia mabilioni ktka mchakato ule wa KATIBA YA WANANCHI...lakini kina Lipumba et al,walitoka bungeni na kusema wanakimbia "UINTARAHAMWE".
Katiba hiyo haikupita.....

Leo unasema JK ni TOFAUTI na JPM aaagh jombaaaaa😂
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom