Sheikh Ponda, Chagua kimoja kati ya siasa na Dini

Sheikh Ponda, Chagua kimoja kati ya siasa na Dini

Mi ccm bhana! Kwa imani yetu waislamu dini na siasa ni kitu kimoja. Anaebisha aniambie je Mtume Muhammad (s.a.w.w) alukua kiongozi wa dini pekeake na je enzi za Yesu kristu yeye alikua kiongozi wa kidini pekeake?
 
Hebu ngoja nishangae wakihudhuria makongamano ya sisiemu sawa ila wakiunga ya wapinzani wanachanganya siasa na dini hebu nifafanulieni uhalisia wake kipi kilicho sahihi
 
Tunashukuru Mtimbo umetufungua akili. Kumbe Lema anakabiliwa na kosa la KISIASA! Sasa kwa nini kosa la kisiasa liende mahakamani na jaji asite kuwaambia wakayamalize kisiasa? Mimi nilifikiri Lema ana kesi ya jinai kumbe ni SIASA! Basi mahakama zetu zinatumika vibaya. Kwa kweli Mtimbo nashukuru kwa kunifumbua macho. Wengine tulimwelewa vibaya Lema bure. Kumbe alikuwa kazini! Maana yeye ni mwanasiasa na ni halali kufanya siasa kama ilivyo halali kwa mkulima kwenda kulima shambani
 
Charity begins at home!
Kati ya Lema na wale mashekh wa Zanzibar wanaoshikiliwa na mahabusu hadi leo yupi alistahili kufarijiwa kwanza!?

Kwa mfano huo tu utaona Ponda ni mwanasiasa anaetumia dini
Dini ni pamoja na ustawi wa jamii kama mfumo uliopo SI rafiki kwa wanajamii ni wajibu kuukosoa au kuuondoa kabisa
Mtume saw hakuishia kufundisha dini tuu bali aliweka mfumo mzuri wa utawala na utoaji haki
NB: waumini wa Kiislamu hutujiiti kondoo wa mtu yoyote
 
Humu watu wanasema siasa huwezi kuitenga na dini,lakini tulishuudia viongozi wa dini wakitukwana kwa kuambiwa wanaingilia siasa.
 
Mapadri wetu wanakusanya mpaka nguo zetu kuzipeleka kwa wafungwa na mahabusu sasa Sheikh kumuona Lema tu iwe nongwa?
 
Maovu ni mengi duniani siyo sababu ya watu wabaya(ambao ni wachache) bali ni kwa sababu watu wema (ambao ni wengi) walioamua kutokemea mabaya kwa visingizia kama vya mleta mada.
 
Na ndio maana nimemtaka Shekh ponda achague kitu kimoja
Kwamba kwa vile wewe hukuja kuniona nilipokuwa gerezani nami sistahili kuja kukuona!
Hujui hapo ndio kaonyesha kuwa ni kweli yeye ni kiongozi wa dini!
Mleta mada humuoni sheikh wa Bakwata wa Dar jinsi ambavyo yuko kwenye siasa 100% kwa vile siasa zake zimeegemea Ccm ila unamuona Ponda kwa vile halambi miguu ya watawala?
 
Moderators with all respect please! Hii mada inajitegemea acheni kuinganisha.

Habari wanajamvi?
Heri ya siku ya kuzaliwa kwa bwana mtume Muhammad (S.a.W) (Happy Maulidi Day)

Salam hizi zikufikie ndugu yangu katika imani ndugu Shehk Haji Issa Ponda.
Nakuomba sana kwa sasa ni vema ukajibainisha kama unachokipigania ni dini ama siasa ili usije ukayumbisha kondoo wako.

Madai yako mengi yaliokufanya kwa mda mrefu ushinde mahabusu gerezani yameanza kufanyiwa kazi.
Tayari BAKWATA imeunda tume ya kuzibainisha mali zote za waislamu ikijumuisha viwanja mbalimbali vilivyouzwa kinyemera, nilitegemea mda huu ungekuwa ukitoa ushirikiano wa kutosha kwa tume iliondwa ili madai yako yale ya mda mrefu yabainishwe na yatatuliwe.

Jana umeonekana Mahabusu ukienda kumjulia hali Mbunge wa Arusha Godbless Lema ni jambo jema na la kiungwana.
Hata hivyo wema huo ulioufanya sina hakika kama umefanya tathmini za athari zake huko mbeleni.

Naomba unikumbushe ulipopatwa na majanga yaliokufanya kukaa mahabusu kwa mda mrefu na hata pale ulipopata majeraha ya Risasi Kiongozi gani wa CHADEMA aliekuja kukujulia hali!?

Je Godbless Lema naye alikuja kukusabahi!?

Je unafikiri kwa nini walishindwa kujitokeza na kukufariji kwenye dhahama ile uliopitia?

Je walikosa nauli au walibanwa na majukumu yao ya kazi? au
Unafikiri hawakuguswa na uonevu uliokukuta?

Jibu ni kwamba walikuwa na uwezo wa kufanya lolote ili kukufariji wewe katika kipindi kile cha mpito isipokuwa hawakufanya kwa sababu ulichokuwa unakipigania kilikuwa tu kina maslashi ya dini na sio kisiasa lakini zaidi ya hapo walishafanya tathmini ya athari ya wao kama wanasiasa kujihusisha na kesi yako ambayo ilikua ya kidini zaidi kuliko kisiasa.

Je wewe umefanya tathimini ya maamuzi yako na kupima athari zake huko mbeleni?

Kama tayari umefanya tathimini na maamuzi ya kwenda kumtembelea Lema ni matokeo ya tathimini hiyo basi kuanzia leo popote ulipo tafuta kadi ya chama cha siasa ili ufanye siasa kwa uwazi zaidi na si kwa kificho kwa kutumia mgongo wa dini.

Kwani katika hali ya kawaida haiwezekani ukaguswa zaidi na Lema anaefanya tu siasa kiasi cha kufunga safari na kumtembelea mahabusu na kuacha kuwatembelea nakuwafariji
waislamu wenzako walio mahabusu wanaoteseka kama ulivyokuwa unateseka kwa kupigania maslahi ya waislamu.

Ni dhahiri kwa ulichokifanya kinakufanya kuwa mwanasiasa zaidi,na kwenye harakati za dini huwa unazitumia tu ili kutimiza harakati zako za kisiasa.

AAWW
Picha tafadhali juu ya kwenda kumuona lema.halafu nakushauri rudi chuo ukasome FIQH ukiielewa utajua what ponda do
 
Kwenda kumuona mtu gerezan sio lazima iwe na uhusiano na kesi yake. (Kumfariji).

Inaweza ikawa mambo mengine muhim kwenye dini, jamii n.k.
Kwahiyo usikalili mambo.
 
Kuna sheria gani hapa nchini inakataza mtu kujiunga na masuala ya siasa ile hali anatumika katika dini?

Kama haipo acha kuingilia uhuru wa mtu,kama hajavunja sheria sio kosa ila kama unahisi dini na siasa ni haramu basi leo hii vyote visingekuwepo
 
Kati ya siku ulizopost ulizopost pumba ni pamoja na leo kwani sheikh haruhisiwi kusocialize na politician
 
Sioni sababu ya kumlamu Shekhe Ponda. Katimiza wajibu wake kijamii.
Labda kwa kuwa ameenda kwa mtu ChaDeMa ndio iwe tatizo.
Inawezekana anatembelea wengi zaidi. Inawezekana unaowasema nao walimtembelea bila kuwapo kwa matangazo.
Naamini dini yake inahubiri upendo na amani. Ameonyesha hivyo.
Anaamini alionewa, na nadhani anaamini Lema pia anaonewa.
 
Politics and religious are there to accomplish life facts
 
When you talk about lifes aspect you directly mean *political, social,.........."
 
Charity begins at home!
Kati ya Lema na wale mashekh wa Zanzibar wanaoshikiliwa na mahabusu hadi leo yupi alistahili kufarijiwa kwanza!?

Kwa mfano huo tu utaona Ponda ni mwanasiasa anaetumia dini

SIJAKUELEWA KABISA, LABDA KUKUSAIDIA TU NAONA WEWE NDIO UMEINGILIA UHURU WA SHEIKH PONDA, WEWE UNAJUA PONDA NA LEMA WAMEONGEA NINI? WEWE UNAJUA MASHEIKH WA ZANZIBAR WAPO GEREZA GANI? NA NANI ANARUHUSIWA KUWAONA? WEWE UNAJUA MASHEIKH WA ZANZIBAR WANAKESI GANI? KITU PEKEKEE NINACHOWEZA KUKUPONGEZA HATIKA POST YAKO HII NI UHURU WAKO WA MAWAZO JAPO UMEROPOKA TU.
 
Mbona ata rais huwatembelea VIONGOZI wa dini wa kiumwa,huu ni Utu Na usipende kuingiza siasa kila mahali
 
Back
Top Bottom