Sheikh Ponda amua moja ueleweke!

Kipara kipya kwa mujibu wa maandiko na mafundisho ya dini ya kiislamu ambayo najua wewe sio muumini wake. Muislamu kumjulia hali mgonjwa ni sehemu ya ibada . Mungu hajasema aina, muda, saa wala itikadi za huyo mgonjwa! Wala haikatazwi aliyekwenda kumjulia mgonjwa hali kuja kuwapa habari za ugonjwa wengine.. alichokifanya ponda ni kutimiza wajibu wake kama muumini wa dini husika na ni thawabu mbele ya allah. Jk alimtembelea pengo alipokuwa matibabuni hatukuambiwa asiwe mwanasiasa awe sheikhe hamkusema!
Mwalimu nyerere alifunga Ramadan na kwenda kwa kina sheikhe ramia kufuturu haijawahi semwa mwalimu achane na siasa ati awe padre!
Mnaosema ponda amekosea na ajitoe kwenye dini ili awe mwanasiasa twambieni kakosea wapi?
Raisi MAGUFULI kila uchao anaongelea mambo ya kitaifa mazabahuni mmeshawahi kulalamika wapi? Mwinyi, kikwete na mkapa walikuwa na dini zao umeshawahi wasikia, kama ulikuwa unasikiliza wakihutubia wakiwa kwenye ibada?
SIO LAZIMA KUANDIKA HUMU ILI KUONESHA KUWA WEWE NI JUHA KIASI GANI LAKINI WAKATI MWINGINE MUWE MUNA AIBU BAS
 
Slaa hajawai kuwa askofu mkuu.tengua hiyo kauli
 
Hayo ni maoni yako tu.Anayetetewa (sheikh Ponda) si lazima afungamane na itikadi ya wakili (Prof Safari wa chadema)
Kwa hiyo si sahihi kusema Sheikh Ponda sasa ni mwanachadema!
Amekwenda nairobi amerudi na ujumbe kama ni hivyo wacha tusubiri fatuma karume nae aitishe press conference yake!
 
Dr Slaa mwaka gani alikuwa askofu? Jimbo gani hilo alikuwa askofu?
Spinning Doctors wa Lumumba hao..... Labda kuna siku watanuomba na Pengo aachane na atale aingie kwenye siasa.

Jamaa alivyo bure hajui hata kazi ya Slaa kabda ya kuingia kwenye siasa.
 
Spinning Doctors wa Lumumba hao..... Labda kuna siku watanuomba na Pengo aachane na atale aingie kwenye siasa.

Jamaa alivyo bure hajui hata kazi ya Slaa kabda ya kuingia kwenye siasa.
Kila mmoja hasemi alikua nani!
 
Tunasafari ndefu sana sisi,kwa vijana wa namna hii mh!
 
Wakili wa Shekhe Ponda ni Prof. Safari. Huenda walikutana Msikitini na sio lazima Ponda awe mwanachama wa CHADEMA ili apate services za Lawyer Prof. Safari.
 
Polycarp pengo walipambana na Gwajima....Yusuph makamba akaongelea kwenye mkutano mkuu wa ccm......Kumbe pengo ni ccm?.......Tafakari kabla ya kuandika
 
Wakili wa Shekhe Ponda ni Prof. Safari. Huenda walikutana Msikitini na sio lazima Ponda awe mwanachama wa CHADEMA ili apate services za Lawyer Prof. Safari.
ameongoza jopo la wanasheria wanne si kwa bahati mbaya nenda kaseme sisi tunakuja tunasubir kibatala!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…