Sheikh Mkuu DSM: Diamond acha utani na Mungu, utapotea

Sheikh Mkuu DSM: Diamond acha utani na Mungu, utapotea

watu bhana!!! Kwa hiyo kusalia video zake ndo kumdhihaki Mungu!!!! Mnafikiri mambo ya kidunia ndo hayahitaji Mungu!!!!!!!! Kila kitu ni imani, Mungu ni mwenye huruma, Watu wote wanamwitaji Mungu haijalishi ni wadhambi. Mungu hayupo kwa watakatifu, yupo kwa ajili ya wadhambi.

umenena vyema mkuu....wengi wetu tunaamka asubihi kukabidhi shughuli zetu kwa Mungu lakini tunayoyafanya kutwa nzima hadi shetani anashangaa
 
Kwani hata mchawi akitaka kumroga na kumuua mtu c anamuomba mungu?

Mungu yupi anaemuomba mchawi ili kuua mtu ndiyo jibu la Diamond kumuomba mungu.
Labda wachawi wa Nigeria
 
N
Kwa mtu wa kaliba ya nasibu abduli na kwa maisha aliyoyachagua kuishi,sidhani kama anapata hata muda wa kusali rakaa moja sembuse mbili!! Ila mungu wake anajua zaidi,tusiusemee moyo
Ninyi ndio mnaojidai kuhukumu bunadamu wenzenu duniani! Ni Mungu tu Narudia tena ni Mungu tu ndiye anayeruhusiwa kuhukumu Binadamu!
 
watu bhana!!! Kwa hiyo kusalia video zake ndo kumdhihaki Mungu!!!! Mnafikiri mambo ya kidunia ndo hayahitaji Mungu!!!!!!!! Kila kitu ni imani, Mungu ni mwenye huruma, Watu wote wanamwitaji Mungu haijalishi ni wadhambi. Mungu hayupo kwa watakatifu, yupo kwa ajili ya wadhambi.
Well said. Utadhani wengine hawatendi dhambi!
 
mwenyezi mungu ni mwenye huruma kwa waja wake....

tutafakari...
 
Diamond kasema huwa anamwomba Mungu. Hajasema huwa anamwomba Mungu yupi maana kuna miungu mingi hapa duniani. Kama angesema huwa anamwomba mungu wa mbinguni hapo tungesema anafanya makufuru. Labda yeye huwa anamwomba mungu wake asiyekuwa wa mbinguni.
 
Mungu ni wetu wote,Huyo shekhe asitake kujifanya yeye kujua kiarabu ndio kua karibu sana Mungu! Wezi,makahaba,wanaijitoa mhanga haya wao wanasali pia awapige marufuko na hao basis ili dunia iwe mahali salama pa kuishi
 
Hakika mungu anajua zaidi!! Anajua anaswali au haswali anajua anamuomba au hamuombi!! Na mm sishangai mungu huyo huyo unaemuomba ww akakunyima akampa diamond wengine ma roho yenu mungu anayajua anajua akikupa ndio kimefika hicho hakitoki tena lakini ona kwa diamond wangapi wananufaika kwa riziki anayo pata? Mm sijui mungu anajua zaidi!! Diamond ukisali omba umri, afya na uwezo wa kumkumbuka pia, utakuja kutubu mungu unaemuamini anaitwa mwenye huruma kizungu anaitwa (The Most Forgiving)huyo sheikh pia anaamini hvyo ukitubu atakusamehe tu
Dah,hii comment bora kabisaaa,kuna watu watabaki kushqngaa tu siku ya mwisho,hao wanaowaona wadhambi ndo wanaingia peponi,wao kusali huku wqmekunja sura wanakuwa viranja motoni
 
Hawa mashekhe wanaowaza ubwaubwa tu ni shida sana,anajiona yeye malaika,huo mzuki ni biashara km ilivyo kuuza tenda nk aheshimu kazi za watu wengine,na ajue Mungu anaangalia matendo na sio nyimbo
 
Watanzania ni wataaalam sana wa kutoa ushuhuda kwa vitu vya kusikia na ambavyo hawajawahi kuvifanya eti hata mchawi anamuomba Mungu akiwa anaenda kuwanga kuthibitisha hili ni kwa njia moja umeshawahi kuwa mchawi na ukafanya huo mchakato au kusema jambaz anaomba Mungu nayo pia lazima uwe umepitia kama unashudiabkwa story za kusikia nakushauri badilika acha story za kukariri na kama mnayosema ni kweli basi jamii forum kuna wachawi na majambaz wengi sana na hapa ndio wanatoa ushuhuda.!
 
Sheikh ametumia hekma na busara kumtaka kuachana utani na Mungu! Na Kukumbushwa ni jambo la kheri, hata mimi nina haki ya kukumbushwa pale napomkosea muumba..huyu sheikh yupo sahihi bwana, na anamtakia mazuri kijana Abdul..
 
Kwa mara ya kwanza nimefurahishwa na Sheikh wa Mkoa wa Dar kwa kusimama na miguu yake mwenyewe...
 
Shehe Mkuu Dar: Diamond Acha Utani na Mungu http://www.muungwana.co.tz/2017/01/shehe-mkuu-dar-diamond-acha-utani-na.html
DAR ES SALAAM: Kufuatia kauli ya msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwamba kabla ya kuachia video zake huwa anasali rakaa mbili ndiyo maana huwa zinakubalika kwa watazamaji wake, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum amemjia juu na kumtaka kuacha utani na Mungu.

Kwa kauli yake, wakati akihojiwa na kituo kimoja cha runinga, Diamond alisema huwa anafanya maombi maalum usiku kwa kuswali rakaa mbili kabla ya kuachia video yoyote, jambo alilosema kwamba ndiyo siri ya mafanikio yake.

“Unajua mimi huwa nafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye video zangu kwa sababu huwa nasali rakaa mbili usiku na kumuomba Mungu ili nifanikiwe kwa video nzuri, nashukuru Mungu anasikia maombi yangu,” alisema Diamond.

Amani lilipomtafuta Shehe Alhadi na kumuuliza kama alichokisema Diamond kina mashiko yoyote kidini, alisema katika dini ya Uislam, muziki wa kidunia ni dhambi na haukubaliki ndiyo maana wasanii kama Mzee Yusuf, wameamua kujiweka nao mbali kwa sababu ni kumkosea Mwenyezi Mungu.

Akaongeza kuwa, alichokisema Diamond ni kama kumfanyia Mungu utani kwa sababu huwezi kuswali, ukamuomba baraka zake ili uende kufanya jambo ambalo ni chukizo mbele zake. Akasema dua za namna hiyo huwa hazipokelewi na Mungu na yeyote anayefanya hivyo, huzidi kumkosea Mungu.

Shehe mwingine aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutochorwa jina gazetini, alisema anachokifanya Diamond ni sawa na mtu ambaye anamuomba Mungu kabla ya kwenda kuiba, jambo ambalo ni tofauti kabisa na misingi ya dini.

View attachment 459113


SOURCE; MUUNGWANA BLOG
Tatizo mashehe ni wachawi sana tena wanamiliki majini;ndiomaana Mimi huwa najiepusha na mashehe
 
Back
Top Bottom