Sheikh Mkuu DSM: Diamond acha utani na Mungu, utapotea

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2016
Messages
212
Points
1,000

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2016
212 1,000
Shehe Mkuu Dar: Diamond Acha Utani na Mungu http://www.muungwana.co.tz/2017/01/shehe-mkuu-dar-diamond-acha-utani-na.html
DAR ES SALAAM: Kufuatia kauli ya msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwamba kabla ya kuachia video zake huwa anasali rakaa mbili ndiyo maana huwa zinakubalika kwa watazamaji wake, Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum amemjia juu na kumtaka kuacha utani na Mungu.

Kwa kauli yake, wakati akihojiwa na kituo kimoja cha runinga, Diamond alisema huwa anafanya maombi maalum usiku kwa kuswali rakaa mbili kabla ya kuachia video yoyote, jambo alilosema kwamba ndiyo siri ya mafanikio yake.

“Unajua mimi huwa nafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye video zangu kwa sababu huwa nasali rakaa mbili usiku na kumuomba Mungu ili nifanikiwe kwa video nzuri, nashukuru Mungu anasikia maombi yangu,” alisema Diamond.

Amani lilipomtafuta Shehe Alhadi na kumuuliza kama alichokisema Diamond kina mashiko yoyote kidini, alisema katika dini ya Uislam, muziki wa kidunia ni dhambi na haukubaliki ndiyo maana wasanii kama Mzee Yusuf, wameamua kujiweka nao mbali kwa sababu ni kumkosea Mwenyezi Mungu.

Akaongeza kuwa, alichokisema Diamond ni kama kumfanyia Mungu utani kwa sababu huwezi kuswali, ukamuomba baraka zake ili uende kufanya jambo ambalo ni chukizo mbele zake. Akasema dua za namna hiyo huwa hazipokelewi na Mungu na yeyote anayefanya hivyo, huzidi kumkosea Mungu.

Shehe mwingine aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutochorwa jina gazetini, alisema anachokifanya Diamond ni sawa na mtu ambaye anamuomba Mungu kabla ya kwenda kuiba, jambo ambalo ni tofauti kabisa na misingi ya dini.

View attachment 459113


SOURCE; MUUNGWANA BLOG
 

DUBULIHASA

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2016
Messages
1,860
Points
2,000

DUBULIHASA

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2016
1,860 2,000
Hata mimi naamini kabisa kwamba Mungu ninayemwamini(YEHOVA) hana mzaha hata kidogo kwa wamdhalilishao ijapokuwa ni mwingi wa fadhila na Huruma.Ajitahidi kuomba toba ili asamehewe.
Mkuu umetisha sana kwa kumuita mungu kwa kina lake Halisi YEHOVA
 

Nathd

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2016
Messages
290
Points
250

Nathd

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2016
290 250
watu bhana!!! Kwa hiyo kusalia video zake ndo kumdhihaki Mungu!!!! Mnafikiri mambo ya kidunia ndo hayahitaji Mungu!!!!!!!! Kila kitu ni imani, Mungu ni mwenye huruma, Watu wote wanamwitaji Mungu haijalishi ni wadhambi. Mungu hayupo kwa watakatifu, yupo kwa ajili ya wadhambi.
 

Forum statistics

Threads 1,389,663
Members 527,997
Posts 34,031,414
Top