Gamba la Nyoka
JF-Expert Member
- May 1, 2007
- 7,038
- 9,353
Nainua macho yangu
Nalilia hatma yangu
Tunu ya uhuru wangu
Twaenda dira gani?
Ubaguzi si mwema
Na si sifa ya uungwana
Hazikwepeki lawama
Hali kuisemea!
Je ni vipi vigezo
Tupewe maelezo
Hatutaki vya dezo
Haki twaulizia!
Kwenye kumi wanipa moja
Halafu wadai tuko pamoja
Ungali wajenga hoja
ufanyayo kutetea?
Tunataka haki sawa
Tunataka usawa
Hatutaki baguliwa
tujenge nchi pia!
Kama mwasema sisi duni
Tueleze mmefanya nini
Na twambieni kwa nini
Mambo haya kutokea?
Nalilia hatma yangu
Tunu ya uhuru wangu
Twaenda dira gani?
Ubaguzi si mwema
Na si sifa ya uungwana
Hazikwepeki lawama
Hali kuisemea!
Je ni vipi vigezo
Tupewe maelezo
Hatutaki vya dezo
Haki twaulizia!
Kwenye kumi wanipa moja
Halafu wadai tuko pamoja
Ungali wajenga hoja
ufanyayo kutetea?
Tunataka haki sawa
Tunataka usawa
Hatutaki baguliwa
tujenge nchi pia!
Kama mwasema sisi duni
Tueleze mmefanya nini
Na twambieni kwa nini
Mambo haya kutokea?