Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Sheikh Khalifa Khamis amzushia UDINI Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.
Lakini kama watu wanateuliwa kwa vigezo vya elimu sion swala la kuanza kupotosha umma kwamba udini
Takwimu za elimu zinahitajika na idadi yao kwa ujumla unaweza ukakuta idadi ya wanaopaswa kupewa vyeo hvyo kwa waislamu ni wachache mno kutokana na sifa

Utashangaa mohamed said anafanya research kuhusu ajira baina ya waislamu na wakristu anasahau kuwa elimu na ajira are directly related,jinsi udhahili unavyoongezeka ktk jamii ya itikadi zote lidini output yake ndo ina determine teuzi,kama vyuo wamesajili wakristu 40,000 wakristu na 5,000 waislamu unategemea waajiriwe waislamu 20000 na wakristu 10000.shekhe mohamed,faizafox nendeni vyuoni mtafiti hilo
 
Mimi toka siku ile nilipoona serikali ya Magufuli imeamua kujitoa Muhanga kuwajengea misikiti Waislamu miwili(Ule wa Makonda na Ule wa Mfalme wa Morocco), hapo hapo ndipo nilipoamini kwa 100% Mtoto huwa anapewaga Pipi tu ili asilie lie, huku mtu mzima akipewa Ugali Mzito ale ashibe.

Wenye Hekima wameshanielewa.
 
Kwa hiyo mfalme ndo alimuomba na makonda je?kwanza sjasema serikali ina dini ila viongozi wa serikali waliomba kujengwa nyumba za ibada na ofisi
Rais hakuomba Mkuu, Bakwata na Wizara ya mambo ya dini ya Morocco walikubaliana tangu mwaka jana na hiyo ofisi waliotoa fedha ni GSM, Makonda sijui alijiingiza vipi kwa hiyo tusiingize Serikali kuwa waliomba kujengewa
 
Hata mimi nilishangaa serikali isiyo na dini izungumze habari za kujenga msikiti, Serikali ya kisecular na misikiti wapi na wapi?

Nilihisi hii inalenga kufunika jambo kwa sababu ya guilty consciousness

Enough is enough, Watu wote wapewe fursa sawa!
 
Umenena vyema ila haya maneno ''KIPENZI CHA WATANZANIA WENGI'' umeyapata wapi? yameharibu uzi mzima maana sikuweza kuendelea tena kusoma uzi wako!
 
mkwere alipoteua waislam wachache watu walitokwa na mapovu kwamba JK ni mdini, mpaka ikafikia yule mzee gavana wa zamani akasema JK amejaza waislam. baada ya kufaya uchambuzi waislam wakabainika ni wachache. nongwa ilikuja baada ya dg wa TISS na IGP kuteuliwa waislam. cha ajabu leo hii mtukufu uchwara anatuhumiwa kwa udini wazee wa povu wanakuja kumtetea bila kufanya analysis. hizi tabia za kukurupuka kurupuka kama popcorn kwenye kikaango mbaya sana. JK alipoteua waislam watoa povu hawakuona weledi ila mtukufu uchwara akifanya teuzi ni weledi umezingatiwa hata wakati jamaa aliowateua wana CV nyepesi kama unyoya halafu wanaongoza wizara nyeti kwa mustakabali wa uchumi na maisha yetu. imani zetu tuweke pembeni maana mwisho wake sio mzuri, pia kama kiongozi aghalabu haidhuru kuwa na busara ya kuangalia/kuguswa na hisia za watu. lisemalwo lipo na kama halipo laja
 
Umenena vyema ila haya maneno ''KIPENZI CHA WATANZANIA WENGI'' umeyapata wapi? yameharibu uzi mzima maana sikuweza kuendelea tena kusoma uzi wako!
wengi ndio walimchagua , wengi ndio waliompa ushindi
 
Dau alisakamwa sana wakati ratio ya staff nssf ilikuwa 55 wakristo 45 waislmu, kikwte kumteua CAG muislamu ilikuwa shida watu walisema kikwete amejaza waislamu kwny serikali wakati wao ndio wengi zaidi, yaani wakiristo usawa kwao ni kuwa na waislmu asilimia 5 na wakirsto 95
Leo wanatetea bila haya ama kweli quran ni kitabu cha ukweli kabisa
 
Wanamajlis,
Prof. Kighoma Malima
na Aboud Jumbe walionya kuhusu udini katika serikali ya Tanzania:
Hebu someni hapo chini:

Tarehe 5 Novemba, 1985 kabla hajastaafu urais, Nyerere aliwahutubia wazee wa Dar es Salaam. Hotuba hii ilijaa simanzi, Nyerere akikumbuka jinsi Waislam walivyompokea Dar es Salaam kwa mapenzi makubwa ingawa yeye alikuwa Mkristo. Wazee hawa wengi wao walikuwa wanachama wa zamani wa TANU waliomuunga mkono Nyerere wakati wa kudai uhuru. Nyerere aliusifia mchango wa Waislam katika kipindi kile kigumu cha kudai uhuru. Nyerere alisema kuwa upogo katika elimu uliorithiwa na serikali yake kutoka kwa Waingereza baina ya Waislam na Wakristo yeye ameuondosha katika kipindi cha utawala wake:


''Waislam wametupa nafasi kupitia sera yetu ya elimu, kurekebisha upogo. Sasa nipo katika hali ya kufarahisha kwa kuwa wakati mwingine sielewi kama Mbunge mpya, Waziri, au Katibu Mkuu katika wizara zetu za serikali, ni Muislam au Mkristo au hana dini labda pale jina lake la kwanza linapotoa utambulisho. Na hata hivyo hiyo siyo njia ya kuaminika kutoa utambulisho wa dini kwa kuwa tuna Wakristo wenye majina ya Kiislam, na Waislam wenye majina ya Kikristo. Kuvumiliana huku nyie ndiyo sababu; nilichofanya mimi ni kuzungumzia maadili haya kwa niaba yenu.''[79]

er3mN_wkwF353N0AAsbIXj4m6-3WKo4MbV1iG1xRpQIxIuKMEuppS-jUVWnP7xDLNtg4nqeyUpH7otXtLrqMJeXpwB_Q1E7oAJ_c1ZqEEB9VUqn4nywG5eW4VX9Sh_1A7xWZ16BPTFL9SMt6cFdcwCMeFGFp57GHq4tU3ya7BO6AB1ivRK8cAyUrnNRnwoAjnj-_zvrqiJZ4dL2kRBH3YkBhuy3hncjafCx_76pB-un2ay3l250aPbXqxYcqzwASH0oQuGOOIvvSh16RURA_-9jKnTZ3nSF42AHDb1ov12G9lpSHz1PdtNfmK-PNuP0wB1rA3o1kyDJao3g-Sk3FdsYbG3buJ-Hf_OUv8AgiItdiDUbe6p4jHvQncc0E1SpNF7699lok8BlOJxEe58zLN-t6n6jZ77YZW-bJXFNhVO2lzkTVYfa3vrqtLy6wq_j9915S1ACFb85ffMO7O-5uJ1Rsal1lCqzNqJcPPfAConUih_3aO9PX_s0gYAITJRtkXSoSZUOtR8pYU2Y2p0NPG9qvgH9iPsJ8bgp2vWPgONV25qpFdaWnEV7BxMvAYGVL0x46OBtOoLUqCMvN-YZePRdd4xTNCLU=w876-h657-no


Hotuba hii ilikuwa ya ulaghai. Ukweli ni kuwa miongo mitatu baada ya uhuru Waislam hawajanufaika chochote wako katika hali ile ile aliyowaacha wakoloni au mbaya zaidi. Sivalon amefichua kuwa Kanisa limeweza kujenga himaya yake ambayo inahodhi asilimia sabini na tano za viti katika Bunge la Tanzania. Kati ya viti hivyo asilimia sabini vipo mikononi mwa Wakatoliki na vilivyobaki vimegawika kati ya Waislam na Wakristo wa madhehebu nyingine.[80] Baada ya kupatikana uhuru, Kanisa lilipohisi wasiwasi, limeweza kwa urahisi kabisa kuwazuia na kuwadhibiti Waislam. Serikali imeweza kutumia nguvu iliyokuwanayo katika kudhibiti siasa kuzuia harakati za Waislam kudai fursa sawa na Wakristo katika kugawana madaraka katika serikali. Kanisa limehakikisha kuwa kupinduliwa kwa ukoloni si kizingiti kwa Ukristo, ingawa ingetegemewa kuwa Kanisa lingedhirika kwa kuanguka kwa ukoloni. Katika miaka yake zaidi ya mia moja, Kanisa lilikuwa limestarehe kama muokozi wa nafsi na watu wenyewe. Kanisa lilikuwa salama na halikupambana na msukosuko wowote kutoka kwa serikali kwa kuwa lilikuwa Kanisa ndilo lilishika hatamu ya serikali.

Baada ya kueleza hayo yote ni muhimu sasa kuangalia jinsi ukereketwa wa Kikristo unavyofanya kazi katika serikali na jinsi kazi hiyo inavyoathiri Uislam. Wizara ya Elimu inachukuliwa kama mfano kwa sababu ya umuhimu wake katika jamii. Katika wizara hii, inaweza kuonekana kwa uwazi kabisa jinsi Ukristo unavyofanya kazi na jinsi udini ulivyoshamiri katika kugawa nafasi muhimu kati ya Waislam na Wakristo. Ilikuwa katika wizara hii katika historia ya Tanzania ndipo kwa mara ya kwanza waziri Muislam alipochaguliwa kuongoza wizara, Kanisa likaingilia kati waziwazi kumpiga waziri vita na kuhoji nafasi nyingine za juu ambazo zilipewa Waislam. Serikali haikuweza kupingana na Kanisa na waziri huyo, marehemu Profesa Kighoma Ali Malima aliondoshwa katika wizara hiyo.

Mwaka 1987 Profesa Malima aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu akiwa Muislam wa kwanza kushika nafasi hiyo. Mawaziri wanane waliopita walikuwa Wakristo. Kulikuwa na malalamiko kutoka kwa Waislam kuwa wizara hiyo imegeuzwa jimbo la Wakristo, hasa pale padri alipoteuliwa na Julius Nyerere kuongoza wizara hiyo. Profesa Malima aliposhika wizara hiyo aliona upo umuhimu wa kufanya marekebisho kadhaa ili kurejesha imani ya Waislam katika wizara hiyo. Kulikuwa na tuhuma kuwa Wizara ya Elimu ilikuwa ikiwabagua vijana wa Kiislam kupata nafasi katika vyuo vya elimu ya juu na ilikuwa ikizuia kupanda vyeo kwa Waislam.

Profesa Malima alipoona dhulma ile iliyokuwapo katika wizara ile dhidi ya Waislam, Profesa Malima aliwateua Waislam wanne kushika nafasi katika kurugenzi mbalimbali na akaandika taarifa ya siri kwa Rais Ali Hassan Mwinyi[81]kumtaarifu udini [82] alioukuta katika wizara ile. Katika taarifa ile kwa rais,[83] Profesa Malima alieleza kuhusu kudumazwa kwa Waislam katika mgao wa elimu. Taarifa hii ilivuja kwa vyombo vya habari[84] na kwa Wakristo wengine. Katika watu walioipata taarifa hii ni Rais Mstaafu Julius Nyerere wakati ule akiwa Mwenyekiti wa chama tawala CCM.

Kuwekwa kando kwa Waislam kupo wazi kiasi ya kuwa mtafiti haihitaji hata kufanya utafiti wa kina unaopewa nguvu na takwimu. Mtafiti yeyote wa sayansi ya jamii hatoweza kushindwa kuona ukweli huu kwa macho tu. Hali hii inaonekana katika kila nyanja ya maisha. Utafiti wa kwanza katika tatizo hili la Waislam kudhulumiwa katika ugawaji wa madaraka ulifanywa na vijana wa Kiislam katika jumuiya yao iliyokuwa ikijulikana kama Warsha ya Waandishi wa Kiislam, kwa ufupi ikijulikana kama Warsha.

Kanisa kwa mara ya pili tokea mwaka 1963 ilipata wasiwasi kuhusu mabadiliko ambayo yalikuwa yanafanyika katika Wizara ya Elimu. Lakini katika miaka ya 1980, hali ya mambo yalikuwa yamebadilika sana. Waislam walikuwa wamejizatiti nje ya mfumo wa siasa kiasi ya kuwa hapakuweza kupatika kibaraka katika Waislam ambae angekuwa tayari kutumika kulihami Kanisa. Hali ya uhasama wa wazi kati ya Waislam na serikali ilikuwa imejitokeza wazi kabisa. Hata hivyo mawakala wa kanisa katika serikali walimshutumu Profesa Malima kwa kuwa Muislam mwenye ‘siasa kali’. Profesa Malima akatakiwa ahojiwe mbele ya Kamati Kuu ya CCM kwa kuingiza hisia za kidini ambazo zimesababisha uadui baina ya waumini wa dini hizi mbili. Suala hili likajadiliwa Dodoma chini ya uenyekiti wa Julius Nyerere. Lakini badala ya kujadili suala la dhulma kwa Waislam na kulitafutia ufumbuzi, yule anaedhulumiwa ndiye aliyewekwa kizimbani badala ya dhalim anaedhulumu; msukumo wa mjadala ukawa katika uteuzi wa wakurugenzi wanne Waislam aliofanya Profesa Malima katika Wizara ya Elimu. Profesa Malima alionekana amekiuka mwenendo na taratibu zulizodumu katika wizara ile kwa kipindi kirefu ya kuwa ni Wakristo pekee wenye haki ya kushika nafasi za juu katika wizara za serikali. Kwa ajili hii profesa Malima akavuliwa madaraka kama Waziri wa Elimu. Rais Mwinyi alikuwa hana uwezo wa kuhimili nguvu ya Kanisa. Nchi inayodai kuwa ni ya kisekula ilikuwa imeshindwa kwa mara nyingine kuwapa Waislam haki yao waliyohakikishiwa na katiba ya Tanzania.

Kwa nchi ambayo inajigamba kuwa inajali usawa kwa wananchi wake inashangaza kuona kuwa Waislam wanabaki nyuma na juhudi zozote ambazo Waislam watafanya ili kuondoa upogo kati yao na Wakristo na kujiletea maendeleo zinapata upinzani na uadui kutoka na mfumo ule ule unajidai kuwa unasimamisha usawa na haki. Kitu cha kusikitisha ni kuwa hakusimama hata Muislam mmoja katika wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM kumuunga mkono Profesa Malima kwa dhulma ambayo wote walikuwa wanafahamu kuwa imedumu kwa kipindi kirefu. Hata ndani ya Bunge hakuna Muislam aliyekuwa na ujasiri wa kumtetea Profesa Malima.[85] Muislam mmoja, Mwenyekiti wa Mkoa wa Pwani, Masudi Mtandika, aliungana na kambi ya Wakristo katka Kamati Kuu ya CCM kumshambulia Profesa Malima. Msimamo wa Mtandika ulikuwa sawa na ule wa Rajab Diwani na Selemani Kitundu walipomshambulia Bibi Titi Mohamed wakati Kamati Kuu ya TANU ilipokuwa ikijadili EAMWS mwaka wa 1963. Kampeni ya chuki na propaganda dhidi ya Profesa Malima ikaanzishwa na vyombo vya habari ambavyo vyote vilikuwa chini ya miliki ya Wakristo na hivyo chini ya Kanisa.

Aboud Jumbe, [86] rais wa zamani wa Zanzibar na Makamu wa Rais wa Tanzania, amefanya utafiti kuhusu nafasi ambazo wameshika Waislam katika serikali, Bunge na vyuo vya elimu ya juu. Takwimu alizoonyesha Aboud Jumbe zinatisha. Katika baadhi ya taasisi Waislam wanaonekana kwa kutokuwepo katika taasisi hizo. Utafiti wa Jumbe ulikuwa wa pili katika kueleza tatizo hili la Waislam na kuliweka wazi kwa matumaini ya kuwa labda serikali ingeweza kuhisi kuwajibika na kujaribu kusahihisha makosa hayo.

Majaribio mengine yamewahi kufanyika huko nyuma na watu kama Sheikh Abubakar Mwilima, wakati huo akiwa Mwenyekiti wa JUWATA na katika Kamati Kuu ya chama tawala CCM, alijaribu kuieleza serikali tatizo hili la Waislam. Kitu kimoja mashuhuri kwa wote waliojaribu kuliweka tatizo hili mbele ya serikali wote hao walimalizwa kisiasa. Maisha yao katika siasa yalikatizwa – Chifu Abdallah Said Fundikira, Tewa Said Tewa, Bibi Titi Mohamed, Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Mussa Kwikima, Sheikh Abubakr Mwilima, Profesa Kighoma Malima na wengine wengi. Ilikuwa kuanzia hapa ndipo Waislam walianza kunong’ona kuhusu njama dhidi yao. Kuwepo kwa njama dhidi ya Waislam kulikuja kudhihirishwa pale watafiti wa Kikristo walipoanza kufanya utafiti kuhusu athari za Ukristo katika utawala wa dola; na bila kujali matokeo ya utafiti kwa hisia za Waislam wakawa wanaeleza jinsi Waislam kwa hila na msaada wa serikali walivyowekwa pembeni katika kugawana madaraka na Wakristo.

[79] Daily News, 6th November 1985.

[80] Sivalon, op.cit. uk.49.

[81] Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Jamuhuri ya Tanzania mwaka 1985-1995.

[82] Warsha ndiyo jumuiya ya kwanza katika historia ya Tanzania baada ya uhuru kuanza kuwaanda Waislam na kupambana na dhulma zilizokuwa zikifanyiwa Waislam. Kwa kipindi chote cha uhai wake serikali ilikataa kukipa usajili. Hii ilikuwa heri kwao kwa kuwa kiliendesha kampeni zake chini kwa chini, kampeni ambazo zilileta mafanikio makubwa hasa katika kuwaelimisha Waislam kuhusu mbinu za adui. Warsha iliweza kufikia hatua ikachukua uongozi wa BAKWATA. Warsha haikudumu katika uongozi kwa muda mrefu. Serikali ikimtumia Adam Nasibu kwa mara ya pili iliweza kuwapiga marufuku vijana hawa wasishugulike na uongozi wowote katika jumuiya yoyote ya Kiislam. Hata hivyo athaari za Warsha zingalipo hadi sasa. Vongozi wengi wa jumuiya za Kiislam hivi sasa wamepata uamsho na mafunzo yao ya awali ya uongozi katika Warsha. Mwaka wa 1981 Warsha walifanya utafiti ambao ulikuwa haujawahi kufanyika kabla, Warsha walifanya utafiti katika elimu ya Waislam Tanzania. Utafiti ulionyesha Waislam walikuwa wana nafasi chache katika vyuo vya elimu ya juu. Taarifa ya utafiti huu ilisambazwa kwa Waislam wote wa Tanzania.

[83] Angalia Kiongozi, Julai 15-31, 1993.

[84] Hali ya Waislam katika Tanzania ni ya kusikitisha inapokuja suala la kueneza habari au propaganda. Vyombo vyote vya habari, vya serikali na vilivyo chini ya wamiliki binafsi vyote vipo katika mikono ya Wakristo. Vyombo hivi vinatumika vyema katika kupiga vita Waislam.

[85] Nje ya vyombo hivyo vya serikali, Profesa Malima alikuwa na jeshi kubwa ka Waislam waliokuwa nyuma yake, wengi wao wakiwa vijana. Wakiwa hawana vyombo vya habari wanavyovimiliki, Waislam walichapa makaratasi na kuyatawanya nchi nzima yakimuunga mkono Profesa Malima huku yakieleza udhalimu wa serikali, mengine yamkitaja Julius Nyerere na Kanisa Katoliki kama washiriki katika kuwadhulumu Waislam. Kwa ajili hii Profesa Malima alipendeza machoni mwa Waislam. Profesa Malima akawa anaalikwa katika kila hafla muhimu ya Waislam. Katika hafla zile Profesa Malima aliwahutubia Waislam kuhusu madhila wanayoyapata.

[86] Aboud Jumbe, The Partner-Ship, Amana Publishers, Dar es Salaam, 1995, uk. 125-138.
Shukran sana sheikh Allah atakulipa ziada In sha Allah
Ukweli wanaujua isipokuwa wanadhan waislam bado ni watu wa kukandamizwa,utawasikia wakiongelea nafas za makam wa rais na wazir mkuu.tukileta orodha za watendaji balozi zote,mashirika ya umma,wakuu,shule na vyuo ni msiba
Ni wakat wa waumin kuamka na kupinga kwa hoja
Uasi siku zote huletwa na dhulma
 
Mkuu, serikali haina dini wala Mh Rais hakuomba hilo jambo. tusipotoshe ndugu kwa ajenda zetu binafsi
.
Mngony,
Waislam hawajapatapo kuwa na agenda yoyote nje ya maslahi ya nchi hii.
Hii ni toka walipopigania uhuru wa nchi hii hadi leo.

Wenye maslahi binafsi Sivalon amewataja katika kitabu chake
Soma kile alichoandika hapo chini:

DSCN1232.JPG
 
Shukran sana sheikh Allah atakulipa ziada In sha Allah
Ukweli wanaujua isipokuwa wanadhan waislam bado ni watu wa kukandamizwa,utawasikia wakiongelea nafas za makam wa rais na wazir mkuu.tukileta orodha za watendaji balozi zote,mashirika ya umma,wakuu,shule na vyuo ni msiba
Ni wakat wa waumin kuamka na kupinga kwa hoja
Uasi siku zote huletwa na dhulma
Mwanya...
Allahuma Amin.

Usiwadaie haki watu haki zao kabla hujawaelimisha kuhusu dhulma kwani
kufanya hivyo huenda kukapelekea wao kukupiga vita wewe unaewatetea.

Kazi kubwa ilikuwa kuelimisha kuhusu dhulma na kuandika historia yetu:
Mohamed Said: TUJIKUMBUSHE: HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA 1954 - 1961 SEHEMU YA KWANZA
 
Mwanya...
Allahuma Amin.

Usiwadaie haki watu haki zao kabla hujawaelimisha kuhusu dhulma kwani
kufanya hivyo huenda kukapelekea wao kukupiga vita wewe unaewatetea.

Kazi kubwa ilikuwa kuelimisha kuhusu dhulma na kuandika historia yetu:
Mohamed Said: TUJIKUMBUSHE: HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA 1954 - 1961 SEHEMU YA KWANZA
Sheikh hizi khabar nzito
Nilipata kuzifatilia na wallah leo asbuhi nilitaza historia yote hii kabla sijaenda kazin
Siku zote haki huchelewa tu
Athar unazozicha zitazaa matunda na utakuwa mtu mwenye kukumbukwa sana
 
Sheikh hizi khabar nzito
Nilipata kuzifatilia na wallah leo asbuhi nilitaza historia yote hii kabla sijaenda kazin
Siku zote haki huchelewa tu
Athar unazozicha zitazaa matunda na utakuwa mtu mwenye kukumbukwa sana
Mwarya...
Amin kwa idhni ya Allah.
 
Religional demographic inaonesha kuwa christian to muslim ratio in Tanzania is 60% to 36% respectively
Na hiyo 4% ni wengine kina hindiism paganism na kadhalika sasa hapo sioni hoja yako ya kidini inasimama wapi?
 
Utashangaa mohamed said anafanya research kuhusu ajira baina ya waislamu na wakristu anasahau kuwa elimu na ajira are directly related,jinsi udhahili unavyoongezeka ktk jamii ya itikadi zote lidini output yake ndo ina determine teuzi,kama vyuo wamesajili wakristu 40,000 wakristu na 5,000 waislamu unategemea waajiriwe waislamu 20000 na wakristu 10000.shekhe mohamed,faizafox nendeni vyuoni mtafiti hilo
Shinyanga,
Ungesoma historia ya Tanganyika ungekuwa katika nafasi nzuri ya kuelewa wanachotahadharisha Waislamu.

Unajua kilichozungumzwa katika Muslim Congress ya 1962 na 1963?

Unajua msimamo wa Kanisa na mipango yake katika kukabiliana na Waislamu?

Ikiwa hujui nifahamishe In Sha Allah nitoe darsa.
 
Kwa masiku kadhaa Sheikh Khalifa amekuwa akisikika na kauli yake ya kumtuhumu Rais Magufuli kuwajaza Wakristo wengi kwenye nafasi zake za uteuzi.

Aidha Sheikh huyo aliongezea kwa kusema kuwa licha ya uwepo wa suala hili la udini Rais Magufuli ameweka wazi upendeleo wake wa kikanda ambapo watu wa kanda ya Ziwa wameonekana kung’ara kwa kuteuliwa katika nafasi za uongozi kwa wingi zaidi kuliko watu wa kanda yoyote hapa nchini.

Akizungumzia suala hilo na waandishi wa gazeti la Mizani la November 11, 2016 Sheikh Khalifa Khamis alieleza kuwa katika nafasi 10 walizotumbuliwa Waislam ni nafasi 1 tu ndiyo aliyopewa Muislam.

Sheikh Khalifa alizidi kufafanua kuwa Wenyeviti wa bodi mbalimbali walioteuliwa na Rais Magufuli 18 ni Wakristo na 1 tu ndiyo Muislam.

Makatibu Tawala wa Wilaya Wakristo ni 81% huku Waislam wakiambulia 19% tu. Wakuu wa wilaya Wakristo ni 71% na Waislam ni 21%.

Makatibu Tawala wa mikoa 137 ni Wakristo na 16 tu ndiyo Waislam. Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya na majiji Wakristo ni 185 na Waislam ni 36 tu.

Kitu pekee anachopaswa kutambua Sheikh Khalifa Khamis ni kwamba Rais Magufuli hateui mtu kwa kuangalia dini bali anaangalia taaluma na uwezo wa kuongoza.

Kukiwa na kitengo kinachohitaji uwakilishi wa dini hapo ndo tunapaswa kuangalia usawa wa uwakilishi wa kidini. Pia anapaswa kutambua kuwa Tanzania haina Wakristo na Waislam tu, kuna watu wa dini tofauti tofauti na wasio na dini pia, je hao amewaweka kwenye kipengele gani?

Hizi ni njama tu za kutaka kumrudisha nyuma Rais wetu kipenzi cha Watanzania wengi. Watanzania tunahitaji MAENDELEO na AMANI tu, mambo ya dini tunayaacha kwenye nyumba za ibada. Tunapofika kwenye sekta za umma hatusemi tena mambo ya dini zetu, bali kauli yetu huwa ni moja tu nayo ni HAPA KAZI TU.

Ni jambo la kusikitisha sana kuona kiongozi mkubwa wa dini akitoa tuhuma za uongo na uzushi kwa Kiongozi Mkuu wa wa nchi yetu.

Sheikh Khalifa anakiuka misingi ya imara ya taifa letu iliyowekwa na baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ya kupiga vita udini na ukabila.

Udini na ukabila ni mbegu mbaya sana ambayo siyo tu haifai kupandwa kwenye ardhi yetu bali haipaswi hata kutunzwa majumbani mwetu, isije mea hata kwa bahati mbaya.

Mataifa mengi yameshuhudia machafuko na mauaji ya kutisha kwa udini na ukabila. Hakuna hata Mtanzania mmoja anayetamani kuona mfano wa mauaji ya Kimbari ya Rwanda au vita ya Biafra Nigeria ikitokea hapa kwetu.
insecurity ni tatizo!
sheikh yuko insecure, watu wa Imani yake na kanda yake hawaoni katika uteuzi!
mletA MADA UPO INSECURE ZAIDI!
Sheikh amehoji! amemuhoji raisi wake (hata kama utaita shutuma) lakini bado msingi wake mkuu ni kuhoji juu ya teuzi za raisi! wewe umeendeleza majibu (kama wewe ndiye unayeteua), umeelezea hofu ya vita, na mambo kadhaa!
sidhani kama ulipaswa kuhangaika na majibu yote, acha kurugenzi ya mawasiliano ikulu itolee maelezo then utasema hoja zako, lkn msubiri raisi ajibu kwanza!
 
Kulalamika ni jadi yenu! hata waislamu wangekuwa 60% bado mngelalamika tu maana mnaonaga mnaonewa kila jambo. Hapo ndo utamwelewa Trump kuhusu ile sera dhidi yenu..
Wacha kutokwa na povu wew km umekula maharage yap vileee, ukwel lazma usemwe mwenye kaya n mbaguz kuliko ww ulivo mnafik na roho yako kubwa km uso wako mm n Christian lakn hil linaniuma
 
Mimi ni mpagani! Lakini kusema ukweli ningekuwa na mamlaka ningefuta usajili Wa baadhi ya dini kwasababu ni chanzo cha ughaidi; na wakati mwingine mpagani ana nafuu....kule vikindu wale watoto chanzo ni mgongo Wa dini
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom