Sheikh Katimba: Makonda achunguzwe

Sheikh Katimba: Makonda achunguzwe

- HAHAHAHAHAHAHA Katimba kutoka U deejay zamani mpaka kuwa Sheikh only in Tanzania hahahahaha, hiyo Taasisi yake ni ipi na BAKWATA ni ipi? hahahahahaha KAtimba wewe mshikaji maan wacha haya mambo utajichafua bure hayakuhusu wachana na wanasiasa watakufikisha pabaya, mambo ya siasa waachie wanasiasa huyawezi kama vipi rudia kupiga Disco kama zamani.

- Wamekubebesha zigo usilolijua hukusoma gazeti la Mtanzania kuwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Taifa inawataka Wabunge Msukuma na Selasini kupeleka ushahidi wa maneno yao juu ya mali za MAkonda mpaka leo hawajaenda, I mean kwa nini Viongozi wa Dini mnjiingiza kwenye mkenge hivi?

le Mutuz

Unazeeka vibaya wewe mzee
 
HII NDO ILE JUMUIA YA SH.PONDA HATUWASHANGAI KUPINGA VITA DHIDI YA UNGA. WAO KAMA CDM VILE KILA JAMBO LA SERIKALI NI BAYA .
Unakichwa kigumu kama govi lako,hujaelewa kitu,pole sana kilaza mkuuuuuuuuu
 
Mali zake wameambiwa waliotuhumu bungeni wapeleke ushahidi tume ya maadili wafuatilie wamekataa kupeleka.Wewe utasemaje zipo wakati waliotuhumu wamekataa kupeleka ushahidi kwenye vyombo husika wakati bungeni walidai ushahidi wanao.Huyu shehe uhakika kautoa wapi wakati waliotoa tuhuma hawana ushahidi wa kutoa?
 
sheikh-300x199.jpg

JUMUIYA na Taasisi za Kiislamu nchini imevitaka vyombo vya kisheria na uchunguzi kuacha kupuuza kauli zilizotolewa na wabunge zilizomtuhumu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumiliki mali zisizoendana na kipato chake halali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Msemaji wa Jumuiya hiyo Sheikh Rajabu Katimba, alisema wakati wa mkutano wa Bunge lililopita baadhi ya wabunge walimtuhumu Makonda hivyo tuhuma hizo zinapaswa kufanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria.

Alisema vyombo vyenye mamlaka ya uchunguzi vinapaswa kufanya uhakiki wa mali za Makonda ili kuondoa shaka katika umiliki wa mali aliyonayo na uhalali wa misaada ya kifedha zinazotolewa kwake na taasisi rafiki.

Sheikh Katimba alisema kifungu cha (11) cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma inamtaka kiongozi kutaja hadharani mali zake ikiwemo zawadi anazopewa.

Hivi karibuni, Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) wakati akichangia taarifa za Kamati ya Bunge na Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama alisema Makonda amenunua jengo ‘(Apartment ) lenye thamani ya shilingi mil 600 jijini Dar es Salaam.

Selesini aliliambia Bunge kuwa Makonda amempa gari mkewe aina ya Mercedez Benzi lenye thamani ya Dola 250,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh milioni 550.

Mbali na Selesini, Mbunge mwingine aliyemtuhumu Makonda kujilimbikizia mali ni Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM) ambaye naye wakati akizungumza bungeni alihoji ni wapi Makonda alipata fedha za kusafiri kwenye ndege daraja la juu kwenda Marekani.

Wakati huo huo, Sheikh Katimba alisema vita dhidi ya dawa za kulevya inaweza kwenda vibaya iwapo itasimamiwa na wanasiasa.

Alisema ili kuepuka hilo vyombo vya dola vyenye mamlaka ya kisheria vinapaswa kuifanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa.

Sheikh Katimba alisema taasisi za kiislamu zinaunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali kupambana na biashara hiyo na kusisitiza kuwa vyombo vyenye mamlaka kuisimamia kwa mujibu wa Sheria ya Kudhibiti na Kupambana Dawa za Kulevya nchini ya mwaka 2014.

‘’Hatuoni ni kwa mantiki ipi watumiaji wengine washitakiwe kwa kutumia dawa na wengine waachiwe huku zitumike na fedha za kuwatibia nje ya nchi.

‘’Wasanii kama Rehema Chalamila, maarufu kwa jina la Ray C’ msanii TID nao pia walipaswa kushitakiwa kama walivyofanywa wengine na vilevile watumiaji walioko mitaani na kwenye vituo vya daladala wote wasombwe wakapimwe na kisha washitakiwe.

“Pamoja na nia ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuongoza na kuendesha vita hiyo lakini vita isimamiwe na vyombo vyenye weledi na si wateule wa kisiasa au wanasiasa,’’ alisema.

Aidha, alizungumza kesi za ugaidi inawakabili baadhi ya viongozi wa dini kwa kueleza kuwa haitakuwa na tija wala heshima iwapo viongozi hao wataendelea kushikiliwa gerezani.

“Ni kweli serikali inatutaka tuiunge mkono kwenye vita hiyo nasi tuko tayari lakini ni vuziri jitihada hii ikawa kwa watu wote, tunaiona serikali inashindwa kutenda haki kwa viongozi wa dini yetu na ni kesi gani isiyokwisha? inatia aibu masheikh kufungwa bila hatia miaka mitatu ni sawa na kufungwa bila hatia,’’ alisema Sheikh Katimba.

Source: Mtanzania
Shehe RAJAB Katimba...Aise umeongea points tupu...ila sidhani kama watamchunguza sababu WOTE ni wale wale....wakati vijana wanavamiwa MAJUMBANI na police wetu....na kuulizwa NYUMBA hii umeijengaje?...kama huna maelezo mazuri unaambiwa MUUZA UNGA...wanakuchukuwa...hata kama hawajakuta kitu...sasa iweje MTU ana maghorofa na Mali kibao kipindi cha miaka 2 tu ya UONGOZI.. na MAMLAKA HUSIKA wapo kimya...kana kwamba hakuna kinacho tuhumiwa dhidi Yake...huyo bwana DAUDI ahojiwe...hakuna ASIYEPENDA KUHONGA MAGARI na nyumba....ila tunafata maadili ya utumishi wa umma na ..nasema kwa sauti kubwa achunguzwe...DAUDI BASHITE...
 
Hivi wale mashehe Wa Zanzibar bado wako magerezani,
 
- HAHAHAHAHAHAHA Katimba kutoka U deejay zamani mpaka kuwa Sheikh only in Tanzania hahahahaha, hiyo Taasisi yake ni ipi na BAKWATA ni ipi? hahahahahaha KAtimba wewe mshikaji maan wacha haya mambo utajichafua bure hayakuhusu wachana na wanasiasa watakufikisha pabaya, mambo ya siasa waachie wanasiasa huyawezi kama vipi rudia kupiga Disco kama zamani.

- Wamekubebesha zigo usilolijua hukusoma gazeti la Mtanzania kuwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Taifa inawataka Wabunge Msukuma na Selasini kupeleka ushahidi wa maneno yao juu ya mali za MAkonda mpaka leo hawajaenda, I mean kwa nini Viongozi wa Dini mnjiingiza kwenye mkenge hivi?

le Mutuz
Mzambia
 
Katimba answari wavaa suruali njiwa atasikilizwa na nani.
Huyu ni Shekhe wa Lowassa,ana kijimsikiti nyumbani kwa Lowassa,na ndie anaemfanyia Duwa Lowassa kuhusiana na yale matatizo yake.Ziara zote za Lowassa yupo pembeni eti anamkinga majini ya maadui wa Lowassa yasimkumbe
Kiufupi Katimba ana njaa kali sana kiasi walikubaliana na Lowassa akiwa Rais,yeye atakuwa shekhe mkuu baada ya kuvunjilia mbali Bakwata
Ohooooo!!!
 
Usipotoshe, wamesema wanaunga mkono wasichotaka ni vita kuongozwa na wanasiasa wasio na weledi katika mambo hayo, na serikali iache double standard ya wabwiaji unga wengine kupelekwa Rehab wengine mahakamani! Umeelewa?
Ataelewa saa ngapi wakati anatumia makalio kufikiri
 
Nawaona kamati ya aman mkoa Chini ya sheikh SALUM na yule Askofu wakitoa tamko rasmi.
 
- HAHAHAHAHAHAHA Katimba kutoka U deejay zamani mpaka kuwa Sheikh only in Tanzania hahahahaha, hiyo Taasisi yake ni ipi na BAKWATA ni ipi? hahahahahaha KAtimba wewe mshikaji maan wacha haya mambo utajichafua bure hayakuhusu wachana na wanasiasa watakufikisha pabaya, mambo ya siasa waachie wanasiasa huyawezi kama vipi rudia kupiga Disco kama zamani.

- Wamekubebesha zigo usilolijua hukusoma gazeti la Mtanzania kuwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Taifa inawataka Wabunge Msukuma na Selasini kupeleka ushahidi wa maneno yao juu ya mali za MAkonda mpaka leo hawajaenda, I mean kwa nini Viongozi wa Dini mnjiingiza kwenye mkenge hivi?

le Mutuz
Akili zako na umri wako ni vitu viwili tofauti unapenda kuongea bila kufikiria simamia kwenye hoja punguza njaa na kujipendekeza.
 
Kama selasini sio mpelelezi aliropokaje kitu ambacho hajapeleleza .Ina maana ni mumbeya anayeokota habari vijiweni na kuzirusha bungeni.Nampongeza bunge kukataa kurusha LIVE nmaana tungekuwa tunalishwa umbeya wa akina SELASINI. no research (upelelezi) no right to speak.
Kuingiza buku saba raha sana..kwan buku saba inakufanya akili itoke ihamie makalioni
 
Katimba answari wavaa suruali njiwa atasikilizwa na nani.
Huyu ni Shekhe wa Lowassa,ana kijimsikiti nyumbani kwa Lowassa,na ndie anaemfanyia Duwa Lowassa kuhusiana na yale matatizo yake.Ziara zote za Lowassa yupo pembeni eti anamkinga majini ya maadui wa Lowassa yasimkumbe
Kiufupi Katimba ana njaa kali sana kiasi walikubaliana na Lowassa akiwa Rais,yeye atakuwa shekhe mkuu baada ya kuvunjilia mbali Bakwata
Mfuasi wa bi kirembwe at work
 
Halafu hawa washkaji kuna kashfa za mabati wanapitisha kimya kimya bandarini kutoka China lakini mijitu inakaa kimya tu,simply Makonda ni mshkaji wao.
Kwa mfano.
Wanaleta makontena 14 wanalipa manne (4)
Halafu kumi.... nawanukuu...wanajilipua.STUPID.
Mkuuu mwaga mboga mkuu
 
Back
Top Bottom