Sheikh auwawa Mwanza

Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
3,115
2,475
Sheikh wa Msikiti wa Shamsiya, Haruna Mlala (39), uliopo katika mtaa wa Ibungilo Kirumba wilayani Ilemela jijini hapa, ameuawa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake na majambazi usiku wa kuamkia jana.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana saa 7:00, baada ya kundi la majambazi kuvamia nyumbani kwake na kuvunja mlango kisha wakaingia ndani na kuanza kumshambulia.

"Mara baada ya majambazi kuvunja mlango wa nyumba yake, waliingia ndani na kumkuta mtoto wake anajisomea. Walimuamuru awaonyeshe aliko baba yake na mara baada ya kuwaonyesha alikolala, majambazi wale walimuamuru Sheikh huyo kutoka chumbani na kumtaka atoe brief case (sanduku dogo) iliyokuwa na fedha," alisema Kamanda Barlow.

Hata hivyo, Sheikh huyo hakuwa na sanduku hilo linaloaminika kuwa lilikuwa fedha, hali iliyowafanya majambazi hayo kushambulia na kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake. Kamanda Barlow alisema baada ya kutenda unyama huo, majambazi hayo yalitoweka na Sheikh huyo alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa matibabu, lakini alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapo kabla ya kuanza kupatiwa matibabu.

Alisema kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Sheikh huyo alijaribu kupambana na majambazi hao, lakini walimzidi nguvu kutokana na majeraha ya kichwani na sehemu mbalimbali za mwili aliyoyapata na kupoteza damu nyingi.

Aliongeza kuwa, Polisi inamshikilia mtu mmoja kuhusiana na tukio ambaye hakumtaja jina kwa maelezo kuwa uchunguzi unaweza kuvurugika.

Majambazi hao walifanikiwa kuiba simu moja aina ya Sumsung yenye thamani ya Sh. 85,000.

CHANZO:
NIPASHE
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,770
4,188
Kwamba walitaka briefcase yenye hela?!, kwani licha ya kuwa sheikh ni biashara ipi anayofanya?!, isijeikawa na ficha ukweli- naoan kama ni maujai ya kisasi, i stand to be corrected.
 

Bornvilla

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
924
267
Innalillah wa inna ilayh rajiuun. Uchunguzi ufanyike na wauaji wakamatwe.Mungu amsamehe madhambi yake aliyofanya na amrehemu.
 

hashycool

JF-Expert Member
Oct 2, 2010
6,568
2,803
seems like they knew whats up! good deal gone bad....alitaka zote. rip shekhe!
 

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Jun 21, 2011
6,786
1,633
naomba ile dua BAKWATA wanayotarajia kuwasomea viongozi wa CHADEMA wawasomee wauwaji hawa at least MUNGU ATAWASIKILIZA NA KUJIBU. rest in peace shekhe
 

Ami

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
3,115
2,475
Kwamba walitaka briefcase yenye hela?!, kwani licha ya kuwa sheikh ni biashara ipi anayofanya?!, isijeikawa na ficha ukweli- naoan kama ni maujai ya kisasi, i stand to be corrected.
Si tunajuwa kuwa masheikh wote wana njaa.Hiyo briefcase ya pesa aliitoa wapi?.Au ilikuwa ni mbinu ya kuficha dhamira yao ya mauwaji tu.
 

Amoeba

JF-Expert Member
Aug 20, 2009
3,292
763
Nachukia sana wezi, hasa wezi wanaoibia maskini wenzao; Kama wewe ni MWANAUME, ingia benki kachukue mule ndani strong room, au zilizo kwa teller, zile ziko Insured!
 

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,957
4,620
Marehemu alijaribu kupambana na majambazi yenye silaha? Ni hatari sana its like a suicide.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom