Sheha wa Tomondo - Zanzibar amwagiwa tindikali!

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Posts
14,193
Reaction score
2,815
Matukio ya wananchi na viongozi mbalimbali kumwagiwa tindikali bado yanaitikisa nchi na habari zilizorushwa asubuhi hii kutoka Zanzibar ni kwamba sheha wa Tomondo amemwagiwa tindikali na amepata majeraha makali sana ktk sehemu mbalimbali za mwili wake.

Amelazwa hospitali na amechukuliwa DNA ili zipimwe kumtambua aliyemmwagia.

Tukio hilo limetafsiriwa kuwa ni la kisiasa.

kutoka itv/radio one

HABARI KUTOKA ZANZIBAR ZINASEMA;Sheha wa Tumondo Mohamed Omary Said,amemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana na hivyo kupata maumivu makali sehemu yake ya kifua na jicho kuumia pia.

Sheha huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Mnazi mmoja mjini Unguja ambapo alipatiwa matibabu ya dharura.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.

Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.
IMG_2380.JPG
 
Matukio ya wananchi na viongozi mbalimbali kumwagiwa tindikali bado yanaitikisa nchi na habari zilizorushwa mda huu kutoka zanzibar ni kwamba sheha wa tomondo amemwagiwa tindikali na amepata majeraha makali sana ktk sehemu mbalimbali za mwili wake.

Amelazwa hospitali na amechukuliwa DNA ili zipimwe kumtambua aliyemmwagia.

tukio hilo limetafsiriwa kuwa ni la kisiasa

Moto mwingine!
 
Siku hizi naona kuna watu wanaona kama uhalifu ni sifa. Kuna mwanasaikolojia nilimsikia siku moja anasema "Kuna mtu hawezi kulala akapata usingizi kabla ya kufanya uhalifu.Uhalifu unakuwa uko ndani yake".Sasa haya matukio ya namna hii kwakweli yanatia shaka.Kinachonisikitisha ni kwamba yule jamaa alieshitakiwa kwa tuhuma za kumpiga risasi Padre Mushi; wakati wote anapofikishwa mahakamani huwa anakuwa anacheka sana! sasa najiuliza kinachokuwa kinamchekesha hasa ni nini na kuna haja gani ya kucheka mahakamani huku akikabiliwa na kesi ya mauaji! je; anajivunia alichokifanya!
 
Siyo ugaidi tena.
 
Pole sana kwake. Hivi nani ametafsiri kuwa tukio hilo ni la Kisiasa?
 
Siku hizi naona kuna watu wanaona kama uhalifu ni sifa. Kuna mwanasaikolojia nilimsikia siku moja anasema "Kuna mtu hawezi kulala akapata usingizi kabla ya kufanya uhalifu.Uhalifu unakuwa uko ndani yake".Sasa haya matukio ya namna hii kwakweli yanatia shaka.Kinachonisikitisha ni kwamba yule jamaa alieshitakiwa kwa tuhuma za kumpiga risasi Padre Mushi; wakati wote anapofikishwa mahakamani huwa anakuwa anacheka sana! sasa najiuliza kinachokuwa kinamchekesha hasa ni nini na kuna haja gani ya kucheka mahakamani huku akikabiliwa na kesi ya mauaji! je; anajivunia alichokifanya!

Kicheka na kununa ni haki ya msingi ya binadamu, kama vile kuzomewa na kushangiliwa. Madamu hajatiwa hatiani sioni kosa lake.
 
ni katika tu kubalance story kwamba wanaoshambuliwa ni wakristo peke yao
 
Back
Top Bottom