She was my my girl friend......

She was my my girl friend......

Salaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaam

Alikuwa mpenzi wangu enzi hizo tuko chuo
Tulipomaliza chuo akapata kazi nzuri
Baada ya miezi mitatu akanidump
Niliumia sana.

Maisha yakaendelea
Hisia zangu zote zilikuwa kwake
Niliona hakuna mwanamke kama yeye.
Nilikuwa namuota daily
nilisikia akijivinjari na wengine lkn nilikuwa sina cha kufanya

Miezi 10 ilipita nikiwa single
One day nikakutana na binti mmoja hivi
Nikamtamani from that day
Nikafanya mchakato nikafanikiwa kumpata
Baadae tukapendana na si kutamaniana tena
Nikaamua kumuoa
Tukafunga pingu za maisha.

Aliyenitosa akapata taarifa kuwa nimeoa
Sikumoja akanitumia mail
Akiniambia eti kasikia nimeoa mwanamke anae fanana nae
Mimi sikujibu mail yake

Kinachonishangaza baada ya hapo akaanza kunipigia simu
Akiniuliza mambo ya ndani kabisa ya familia yangu
Mala ooooh to what extent i do love my wife
Mala ooooh anaenjoy sex kama alivyo kuwa ana enjoy yeye
Mala ooooooooooh huwa unamtoa out na ni wapi


Juzi juzi hapa tumepata mtoto wa kwanza na mke wangu
Akanipigia simu tena akiuliza mambo ya ndani kabisa

Jamani nimfanyeje huyu binti
Na nikipi hasa kinachomsukuma kufuatilia maisha yangu

Huyo binti bado anapata tabu ya kukabiliana na ukweli kuwa alikupotezea na sasa umeoa na mbaya zaidi anasikia sana kwa watu juu yako which could be that wanaompa habari zako wanazitoa kwa exaggerated manner kitu kinachomfanya azidi kuumia kwa wivu. Anachotaka kujua ni jinsi gani huyo 'anaefanana nae' anaenjoy mapenzi yako. Sasa dawa yake mwambie unamtoa out mara 3 kwa wiki siku nyingine mpaka mara 5 na akiuliza vya ndani we mwambie mkeo anaenjoy sana mpaka unamshangaa. Kwa kifupi mwambie humfananishi na mahusiano yako yoyote uliyowahi kuwa nayo. Dadeq.
Koleza mzee. Hao ndo wasumbufu na dawa yao ni komoa.


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Anataka kuona kama umeoa tu ilimradi kwa vle ulikua unampenda yy maadam umempata mwingine umpendae usiwasiliane nae tena
 
Jaribu kufikiria mkeo anasumbuliwa na her ex...sasa kakufuata kukuomba ushauri kuwa afanye nini...
Huo ushauri utaoufikiria kichwani basi ndio nawe utumie huo huo kujinasua kutoka huo mtego...

...This is super!!!
 
badili namba ya simu , na usikae kupokea simu yake wala kujibu msg zake ...... huyo ni majanga full.
 
hajaolewa bado,akiolewa hatakuulizia wala kukufuatilia maana karata yake kwa sasa ni jokery teh teh alifikiria una sura kama ndimu hautapendwa tena.Mchane live kwamba hutaki usumbufu wake bhana mwishowe atakuuliza mnatumia style gani.........

ulijuaje! mbona kashauliza
 
hakujua thamani ya alichokuwa anakipoteza. sasa anatamani akipate ama aharibu. hebu kuwa ngangari nawe mpotezee. si alikudump - move on banaa! acha ushamba basi!
 
Back
Top Bottom