My Best Friend: Vunja ukimya, kuwa muwazi kwa mtu unayempenda

Mwanibombo

Member
Mar 25, 2023
61
84
FIRST YEAR: Nikiwa nimekaa "lecture room" nikimuangalia msichana aliyekaribu yangu, niliyekuwa namuita 'Bestfriend' . Nilikuwa nikimuangalia nywele zake nzuri na sura yake ya upole huku nikitamani awe wangu. Lakini yeye halikuwa anatamani hilo, na nilikuwa nakilitambua hilo.

Baada ya lecture, alikuja kwangu na kuniomba notice za siku ya nyuma kwa sababu hakuweza kuingia darasani siku iliyopita.Baada ya kumpa akasema 'asante' na kushikana mkono na mimi. Nilitamani kumwambia. Nilitamani ajue kuwa nataka tuwe zaidi ya marafiki. Nilimpenda but I was just too shy, and I didn't know why.

SECOND YEAR: Simu yangu iliita, kupokea alikuwa ni yeye alikuwa akilia akinielezea jinsi boyfriend wake broke her heart, she asked me to come over because she didn't want to be alone. kwakuwa ni rafiki yangu kipenzi ilinibidi kwenda kumfariji.

As I sat next to her on the sofa, nilikuwa nikimuangalia machoni nikitamani awe wangu. Baada ya masaa mawili baada ya kuangalia nae movie mbili tatu na kula nae chakula pamoja akarudi kwenye hali yake ya kawaida. Hivyo akaamua kwenda kulala, before akaniangalia na kuniambia 'asante' na kunipa tabasamu tamu. Nilitamani kumwambia. Nilitamani ajue kuwa nataka tuwe zaidi ya marafiki. Nilimpenda but I was just too shy, and I didn't know why.

3RD YEAR: Siku moja kabla ya tamasha la mziki chuoni alkuja kwenye meza yangu lecture room na kuniambia "'Boyfriend wangu' amepata udhuru hivyo naomba unipe kampani leo usiku katika tamasha la mziki". Kwa kuwa tuliwekea promise kwamba ikitokea kila mmoja wetu amekosa mtu wa kudate nae basi tutaenda pamoja just as 'friends' hivyo tukaenda.

Katika tamasha baada ya kila kitu kuisha na mziki kufungwa, nilikuwa nimekaa nje ya ukumbi nikimuangalia jinsi alivyokuwa anacheka na rafiki zake, she saw me looking to her she smiled at me. I want her to be mine lakini yeye alikuwa hafikirii hilo kabsa na nilikuwa nikilitambua hilo. tjen she said to me "nimekuwa na muda mzuri na wew asante sana" and she gave me a sweet smile.

Nilitamani kumwambia. Nilitamani ajue kuwa nataka tuwe zaidi ya marafiki. Nilimpenda but i was just too shy, and I didn't know why.

GRADUATION DAY: Siku, wiki, miezi vikapita, ilikuwa ni mahafali yetu tukimaliza masomo ya chuo. Akainuka akaenda kutunukiwa shahada yake ya uchumi. Nilikuwa nikimuangalia alikuwa amependeza sana siku ile.
I wanted her to be mine, but she didn't notice me like that and i knew it. Kabla watu hawajatawanyika kwenda makwao, alikuja kwangu akiwa na vazi lake la mahafali, na kulia pale nilipo mkumbatia. Akainua kichwa chake na kuniambia"you are my bestfriend asante sana."

Nilitamani kumwambia. Nilitamani ajue kuwa nataka tuwe zaidi ya marafiki. Nilimpenda but i was just too shy, and I didn't know why.

MIAKA 3 BAADAE: Nikiwa kanisani yule msichana alikuwa anaolewa. Nilimuangalia akiwa anasema "Ndiyo nakubali" and drive off to new life. Moyo wangu ukapasuka 'paaa.. Akaolewa na mwanaume mwingine.
I wanted her to be mine, but she didn't see me like that and i knew it. Lakini kabla ya kwenda ukumbini, alikuja kwangu na kusema "asante sana, u have been my bestfriend ever". Kisha akani-kiss kwenye paji la uso akiwa na vazi lake la harusi. Nilitamani kumwambia. Nilitamani ajue kuwa nataka tuwe zaidi ya marafiki. Nilimpenda but i was just too shy, and I didn't know why.

KWENYE MAZISHI: Miaka mitano baadae, nilikuwa kwenye ibada ya mazishi ya binti niliyempenda lakini nikaogopa kumwambia. Binti aliyekuwa my best friend. I looked down katika jeneza lililokuwa na msichana ambaye alikuwa ni 'bestfriend' wangu.

Katika service ya mazishi wakasoma diary ya Bestfriend ambayo alikuwa akiiandika enzi za maisha ya chuo. Mchungaji akasoma yaliyokuwemo kwenye diary, ilikuwa ikisomeka hivi. I stare at him napenda awe wangu, but doesn't notice me like that, andIi know it.

Alisoma mchungaji kisha akaendelea. Nilitamani kumwambia. Nilitamani ajue kuwa nataka tuwe zaidi ya marafiki. Nilimpenda but i was just too shy, and I didn't know why. Niliishiwa nguvu katikati ya kundi la watu.. Nilipiga magoti nikilengwalengwa na machozi. Maneno yale yalinichoma sana hasa ukizingatia kuwa nilimpenda lakini niliogopa kumwambia. Kumbe na yeye alinipenda pia lakini aliogopa kuniambia. I wish ningemwambia ukweli ila nilishachelewa. Sipo nae tena ameshatangulia mbele za haki.

MORAL OF THE STORY: Vunja ukimya. Be free when you love someone kuwa muwazi kwake.
 
Siku hizi kuna vijana wanajiita Mabaharia' wanasema ukimwambia binti unampenda unampeperusha' Kwa hiyo weka mazingira ya kula mzigo au kuwekeza kimatendo kuliko Kauli/neno lenyewe.

Halafu ndio mengine yanafuata. Ila kama ni kweli ulikuwa too slow..anakuita room peke yake umliwaze unaishia kuangalia movie na kupiga story!

Anyway nimeshangazwa na msibani kusomwa diary! Au sijui Mimi sihudhurii sana misiba! Au ni kisa Cha kubuni!
 
Siku hizi kuna vijana wanajiita Mabaharia' wanasema ukimwambia binti unampenda unampeperusha' Kwa hiyo weka mazingira ya kula mzigo au kuwekeza kimatendo kuliko Kauli/neno lenyewe. Alafu ndio mengine yanafuata. Ila kama ni kweli ulikuwa too slow..anakuita room peke yake umliwaze unaishia kuangalia movie na kupiga story!

Anyway nimeshangazwa na msibani kusomwa diary! Au sijui Mimi sihudhurii sana misiba! Au ni kisa Cha kubuni!
kwa kumbukumbu zangu sio mara ya kwanza hii 'stori' kuja humu jamvini.
 
Inawezekana ikawa kama story ya kutunga ila hii inatokea sana siwezi kueleza zaidi ila sna inatokea.

Ego yaani unakataa ukweli haswa kwa wanawake anajaribu mtu anayempenda kumptezea ila wapi ..Ni kiburi flani je nikiwambia atanionaje better kumwambia mtu ila sio kumezea
 
Siku hizi kuna vijana wanajiita Mabaharia' wanasema ukimwambia binti unampenda unampeperusha' Kwa hiyo weka mazingira ya kula mzigo au kuwekeza kimatendo kuliko Kauli/neno lenyewe.

Halafu ndio mengine yanafuata. Ila kama ni kweli ulikuwa too slow..anakuita room peke yake umliwaze unaishia kuangalia movie na kupiga story!

Anyway nimeshangazwa na msibani kusomwa diary! Au sijui Mimi sihudhurii sana misiba! Au ni kisa Cha kubuni!
Baba kausha story ni ya kutunga. Chukua tu ujumbe ila ukaushe.
 
Chuo Kijiji kidogo ila wambea wengi.
Unamfungukia saa mbili saa tatu habari zipo chuo mkoa mwingine.
Watu wana mtandao mkubwa na taarifa zetu ndio maisha Yao.
Bora ulosungu tu.
 
Kama huna pesa unashindia miogo ya kukaanga huo ujasiri wa kumtongoza pisi kali unautoa wapi mkuu haya mambo yasikie tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom