Shauri la jinai namba 8606/2025 Jamhuri vs Tundu Lissu, kesi ya uchochezi na kuchapisha taarifa za uongo imehairishwa hadi Julai 01, 2025

Shauri la jinai namba 8606/2025 Jamhuri vs Tundu Lissu, kesi ya uchochezi na kuchapisha taarifa za uongo imehairishwa hadi Julai 01, 2025

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779

View: https://youtu.be/ZbNLPqfSiQ8

Wakuu

Kesi ya uchochezi na kuchapisha taarifa za uongo inayomkabili Mwenyekiti wa chadema Tundu Lissu inaendelea muda huu.

Awali Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu aliiomba mahakama kumpa nafasi ya nusu saa kuweza kujadiliana na mawakili wake juu ya namna ya kuliendea shauri la uchocheza na kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa YouTube.

Hakimu alimruhusu Lissu na kutoa dakika 45 hivyo shauri hilo kuhairishwa kuanzia saa 11:35 AM mpaka saa 12:20 PM. Ambapo mahakama imetoa dakika 45 kwa ajili ya kuteta na pia kupata mapumziko madogo kwa mawakili.

Shahidi namba moja (PF. 22863 Inspector John) katika kesi ya uchochezi na kuchapisha taarifa za uongo akitoa ushahidi wake.

Awali wakili wa Serikali Mwandamizi Nassoro Katuga aliieleza mahakama hiyo kuwa tarehe 9 Juni 2025 mahakama hiyo iliamua juu ya maombi madogo Na. 13298 /2025 ya kuficha mashahidi ambao ni raia ambao sio askari na kwamba iwe sehemu ya mwenendo huo.
1750072835685.png

Shauri Na. 8606/2025 la uchochezi na kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa YouTube linalomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antiphas Lissu limeahirishwa mpaka Julai 1, 2025 baada ya upande wa jamhuri kuomba ahirisho hilo.

Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga aliieleza mahakama kuwa shahidi Na.01 (aliyejitambulisha kama Inspekta John) aahirishe kutoa ushahidi mpaka pale Mtaalam Mchunguzi kutoka kitengo cha uchunguzi wa vifaa vya elektroniki atakapotoa ushahidi wake.

Awali shahidi huyo alipokuwa akitoa ushahidi aliieleza mahakama kuwa kupitia video iliyochapishwa na chombo cha habari cha Jambo TV ilichapisha maudhui kwa mfumo wa live (mbashara) ambayo ndani yake yalikuwa na maneno yenye kuonesha kuzua taharuki.

Shahidi huyo ameieleza mahakama kuwa baada ya kusikia maneno hayo alitoa taarifa kwa kiongozi wake na ambapo aliamriwa kwenda kwa Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum aitwaye SACP George na kumuelezea na kisha baadaye kupakua picha mjongeo(video) hiyo na kuikabidhi kanda maalum.

Shahidi huyo ameieleza mahakama kuwa baadhi ya taarifa zenye viashiria vya uchochezi na kuzua taharuki ambazo zilizungumzwa na Lissu siku hiyo zilichapishwa katika kurasa za mitandao ya kijamii na vyombo vingine ikiwemo Clouds TV, Arusha One TV na The Chanzo.

Akiendelea kutoa ushahidi huku akiongozwa na Wakili Katuga, upande wa Jamhuri uliiomba Mahakama kusitisha utoaji wa ushahidi kwa shahidi wa kwanza mpaka pale shahidi wa pili, mtaalam mchunguzi kutoka kitengo cha uchunguzi wa vifaa vya elektroniki atakapokuja na kutoa ushahidi kupitia kielelezo ambacho kina picha zikimuonesha Lissu akitenda makosa aliyoshtakiwa nayo.

Pamoja na upande wa utetezi kupinga hoja hiyo wakiongozwa na Wakili Kibatala ukidai kuwa ni janjajanja za shahidi kupoteza muda. Akihojiwa nje ya mahakama hiyo Kibatala amesema wanamsubiri kwa hamu shahidi huyo na mashahidi wengine katika kesi.
 
View: https://youtu.be/ZbNLPqfSiQ8

Wakuu

Kesi ya uchochezi na kuchapisha taarifa za uongo inayomkabili Mwenyekiti wa chadema Tundu Lissu inaendelea muda huu.

Awali Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu aliiomba mahakama kumpa nafasi ya nusu saa kuweza kujadiliana na mawakili wake juu ya namna ya kuliendea shauri la uchocheza na kuchapisha taarifa za uongo kupitia mtandao wa YouTube.

Hakimu alimruhusu Lissu na kutoa dakika 45 hivyo shauri hilo kuhairishwa kuanzia saa 11:35 AM mpaka saa 12:20 PM. Ambapo mahakama imetoa dakika 45 kwa ajili ya kuteta na pia kupata mapumziko madogo kwa mawakili.

Shahidi namba moja (PF. 22863 Inspector John) katika kesi ya uchochezi na kuchapisha taarifa za uongo akitoa ushahidi wake.
View attachment 3371449

Huyu shahidi ajiandae vema na kama hajala akashiba akafanye hivyo chap
 
Back
Top Bottom