Yaliyojiri Mahakama Kuu: Mahakama yatupilia mbali mapingamizi ya Serikali dhidi ya Lissu, Shauri la msingi kuendelea kusikilizwa...

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
877
1,000
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo inatarajia kutoa uamuzi endapo maombi yaliyowasilishwa na aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu yanasifa ya kusikilizwa na Mahakama hiyo na kama aliyefungua kwa niaba yake anayo mamlaka ya kufanya hivyo.

Uamuzi unatarajia kutolewa leo mbele ya Jaji Sirilius Matupa,baada ya kusikiliza sababu nane za kupinga maombi hayo ambayo wanadai hayajakizi vigezo vitano kati ya sita.

IMG_20190826_143445.jpg

Kujua mapingamizi yaliyoibuliwa na Serikali, soma

Kujua kesi ilipoanzia, soma


***UPDATE***
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetupilia mbali mapingamizi ya Upande wa Jamhuri

Tundu Lissu ameshinda pingamizi la Serikali dhidi ya maombi yake ya kibali cha kufungua kesi kupinga kukoma kwa ubunge wake, Mahakama Kuu imekubali kusikiliza maombi yake

****
Zaidi, soma....

Dar es Salaam. Aliyekuwa mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), nchini Tanzania, Tundu Lissu ameshinda pingamizi la awali lililowekwa na Serikali dhidi ya maombi yake ya kibali cha kufungua shauri kupinga kukoma kwa ubunge wake.

Badala yake mahakama hiyo imekubali kuendelea na usikilizwaji wa maombi ya msingi ya Lissu.

Lissu ameshinda pingamizi hilo baada ya Mahakama Kuu Tanzani kutupilia mbali hoja za pingamizi hilo la Serikali na kukubaliana na majibu ya hoja hizo yaliyotolewa na jopo la mawakili wa Lissu, linaloongozwa na wakili Peter Kibatala.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Sirillius Matupa, leo Jumatatu, Agosti 26, 2019, baada ya kupitia na kuchambua hoja za Serikali za pingamizi hilo alilolisikiliza Ijumaa iliyopita ya Agosti 23,2019 na majibu na mawakili wa Tundu Lisuu, dhidi pingamiizi hilo.

Lissu amefungua maombi Mahakama Kuu, Masjala Kuu, Dar es Salaam chini ya hati ya dharura, kupitia kwa kaka yake Alute Mughwai, ambaye amempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo, ikiwa ni hatua ya awali kabisa ya kupigania kurudishiwa ubunge wake.

Katika maombi hayo namba 18 ya mwaka 2019, dhidi ya Spika wa Bunge la Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Lissu anaomba kibali cha kufungau shauri la maombi maalum kwa lengo la kupata amri mbalimbali kuhusiana na uamuzi huo wa kuvuliwa ubunge.

Maombi hayo yalikuwa yamepangwa kusikilizwa juzi Ijumaa Agosti 23, 2019, lakini yalikwama baada ya Serikali kupitia kwa AG, ambaye ndiye mjibu maombi wa pili, kuibua pingamizi la awali akiiomba mahakama iyatupilie mbali maombi hayo bila hata kuyasikiliza.

Katika pingamizi hilo la awali, Serikali iliwasilisha jumla ya hoja nane, ikipinga kusikilizwa kwa maombi hayo kwa madai kuwa yana kasoro za kisheria. ambazo zilikuwa zimejikita katika masuala manne, manne kama yalivyobainishwa na Wakili Mkuu wa Serikali (Solicitor General –SG) Dk. Clement Mashamba

Kutokana na pingamizi hilo la awali, mahakama imelazimika kusimamishwa usikilizwaji wa maombi ya Lissu na kusikiliza kwanza, pingamizi hilo la AG, kama ulivyo utaratibu wa kawaida, ambalo lilisikilizwa mpaka saa mbili usiku.

Katika uamuzi wake le Jaji Matupa ametupilia mbali hoja za pingamizi la awali la Serikali isipokuwa hoja moja tu ya kasoro katika viapo vinavyounga mkono maombi ya Lissu.

Kutokana na kasoro hizo Jaji Matupa amesema inapotokea kuwa kuna aya zenye kasoro za kisheria namna pekee ni kuziondoa aya hizo katika kiapo hicho na kuangalia kama aya zinazobaki zinaweza kusimama na kuthibitisha maombi.

“Nikiangalia hapa aya zinazobaki hapa baada ya kuziondoa hizo zenye kasoro, ninaridhika kabisa kuwa zinaweza kuthibitisha maombi.”, amesema Jaji Matupa na kuongeza:

Hivyo hoja zote za pingamizi la Serikali zimekataliwa isipokuwa hizo zenye upungufu kwenye hati za viapo. Ukiachilia mbali kasoro hizo za viapo, mambo mengine yote yataasikilizwa wakati wa usikilizwaji wa maombi ya msingi.”

Jaji Matupa amesisitiza kuwa pingamizi haliweza kuondoa haki za msingi kuwasikiliza wadaa kama kuna hoja za msingi za kusikilizwa.

Kuhusu hoja ya kusitisha kwa muda kuapishwa kwa mbunge mteule wa Singida Mashariki, Faraji Mtaturu, Jaji Matupa amesema kuwa sasa ni mapema mno kulitolea uamuzi na kwamba atalisikiliza ombi hilo wakati wa usikilizwaji wa maombi ya msingi.

Kwa sasa mawakili wa pande zote wamekutana kujadiliana kama wanaweza kuendelea na usikilizwaji wa ombi hilo la kusitishwa uapishwaji wa Mtaturu.

Lissu yuko nchini Ubelgiji, kwa ajili ya matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu ambao hadi sasa hawajajulikana, tangu Septemba 7, 2017, aliposhambuliwa, katika makazi yake, jijini Dodoma akitokea bungeni.

Juni 28, 2019, wakati akiahirisha mkutano wa 15 wa BungeSpika Ndugai altangaza kukoma kwa ubunge wa Lissu, huku alijitetea kuwa si yeye aliyemvua ubunge bali ni matakwa ya Katiba ya Nchi.

Alitaja sababu za uamuzi huo kuwa ni kutokuhudhuria vikao vya bunge kwa muda mrefu bila kumjulisha Spika kwa maandishi mahali aliko na kutokuja taarifa za mali na madeni kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Chanzo Mwanchi.
 

minyoo

JF-Expert Member
May 25, 2013
20,919
2,000
Kama Mahakama hawatajitoa fahamu wakafanya kazi pasipo kutumia Sheria za zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM nina hakika kesi itaendelea, lakini mahakamaccm ikitumia Sheria binafsi za CCM kesi itaishia hapo hapo, cha msingi ni kumuomba Mungu hiyo mahakama itumie Sheria za Nchi zile Sheria tenda haki wasitumie Sheria binafsi za Ndugai na watu wake.
 
Jan 3, 2015
19
75
Mungu ni mwema. Hakj itashinda
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo inatarajia kutoa uamuzi endapo maombi yaliyowasilishwa na aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu yanasifa ya kusikilizwa na Mahakama hiyo na kama aliyefungua kwa niaba yake anayo mamlaka ya kufanya hivyo.

Uamuzi unatarajia kutolewa leo mbele ya Jaji Sirilius Matupa,baada ya kusikiliza sababu nane za kupinga maombi hayo ambayo wanadai hayajakizi vigezo vitano kati ya sita.
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
27,952
2,000
Nakumbuka Lisu alionya kuwa kesi hii ni sensitive hivyo watu watulie kwa vile inahitaji umakini mkubwa kisheria namna ya kuifungua. Akataja na process yote ilivyo tedious na complicated. Akaongea mambo ya power of attorney, registration ya kesi huko ??? etc etc. Nina uhakika atapita mapingamizi hayo leo. Akaonya yasije kutokea ya Nasari, akawaasa wapenda haki watulie mambo yaende kwa umakini! Erythrocyte
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom