TANZIA Sharo Millionea afariki dunia

Dah nilikua namuigizia mke wangu nikiwa nipo tungi kupindukia anafurahi saaanaa
Daah sidhani kama ntamuigiza tena
(Only when we are alOne)
R.I.P shalobalo
 
Mimi kila nikienda kulala huwa ninamshukuru Mungu kwa kunilinda siku yote na kumuomba anilinde tena usiku na nikiamka ahsubuhi namshukuru kwa kunilinda usiku wote na kuomba tena anilinde siku yote...Watu wengi hatufahamu ni bahati gani tunayopata kila siku tunapoamka tukiwa hai tunapumua...na tena mambo yanapokuwa yanakwenda vizuri ndiyo tunazidi kujisau.
Kijana ndiyo alikuwa anaelekea kwenye pinnacle ya mafanikio yake lakini kama remmy ongala alivyosema "kifo hakina huruma"
RIP.
 
Tairi lilipasuka gari ikagonga mti ikang'oa mti na jamaa hakupatikana ndani ya gari walimkuta sehemu nyingine. Pia jamaa alifariki dunia akiwa nje ya gari.
Polisi walifika saa nne usiku.
Gari la marehemu lilivutwa na gari la tanesco leo asubuhi.
Gari halitamaniki.
Source millardi ayo
 
Pumzika Kwa amani Sharo

Leo nimesikiliza radio tokea asubuhi mpaka sasa hivi, channels tofauti tofauti

katika kusikiliza huko radio huku tukiomboleza kifo cha Sharo milllionea nimegundua lifuatalo,

nyimbo za maombolezo ni chache sana (ni jambo jema sababu hatuombei maafa), so kwa sababu hiyo radio katika kuonesha kuomboleza kwao zimekuwa zikicheza rekodi za mafunzo na zile chache za maombolezo zilizotungwa wakati maafa yalipotokea

Sasa nachowaza na kunifanya niandike headingi hiyo hapo juu ni hili,
Nyimbo zote za mafunzo zilizochezwa leo (au asilimia kubwa zaidi ya 90) ni za kuanzia miaka ya 2005 na kurudi nyuma, meaning ya kwamba sanaa za leo hazifundishi lolote juu ya madhara ya ukimwi, dawa za kulevya au anasa ilopitiliza, Zaidi na zaidi wao wanasemea starehe na kuzidi kusifia ngono

kwa mwendo huu nachelea kusema sanaa ya Tanzania inaelekea kuisha au kupotea kabisa, msanii kwenye radio release zako ambazo zinatangaza album sio mbaya kuweka nyimbo ya kufunza
mfano wa hizo nyimbo ni
Swahiba - Jebi , afande Sele
Alikufa kwa ngom - Mwana FA
Shida - Remmy
Faraja - Lady Jaydee etc



Rest In Peace Sharo Millionea
 
waimbaji na watunzi wetu wote wanaamini kila kitu katika mapenzi na mitungi basi...
 
Back
Top Bottom