Share nasi: Ulijisikiaje siku mpenzi wako unayempenda aliposema mimi na wewe basi?

Sijawahi kuachwa kwakweli kwasababu naogopa sana maumivu ya kuachwa.
Nikianza kuona hakueleweki naanza kujitoa mdogo mdogo halafu nakupa tu taarifa kwamba mimi na wewe basi na ukitaka sababu nakupa.
Sisubiri kuachwa kwakweli na hata ikitokea nakupenda sana ukitaka kuniacha nitakubembeleza mpaka utanionea huruma na uhusiano utarudi ila huko mbele ntakayekuacha ni mimi mana hapo sitakuwa na maumivu tena.
Mmh tabia mbaya hiyo hadi uamue ww jamani!
 
Mimi nililazimika kuacha kutokana na kosa alilofanya mwenzangu lakini ..... Nimejuta hata huko kuzaliwa mbona!
 
Tulikosana kidogo then nikampigia cm ili tuyamalize,loh!!Alinijibu hataki tena kuwa nami,aisseee nikamuuliza umepata mwengine akajibu yes!!

Nilihisi ulimwengu wote umeniangukia.Kuanzia hapo kinachofuata huwa nikimuona haeleweki naanza kumwacha mimi japo huwa naumia mnoooo.
 
Mkuu sijui ulijuaje kama ndio napitia hii situation....unampenda mtu kwa moyo mmoja....lakini mwisho wa siku unaambulia maumivu.

Ila maisha lazima yaendeleee..ila kama una roho ndogo unaweza kujiuaa...ila ni mapito tu nayo yatapitaa
Aisee pole sana.Bila Kuona soni.Alianzaje kukwambia au kulikuwa Na sababu zozote??au ulimuudhi kitu?
 
Kwa wale ambao tumebahatika kuona uchi wa mwanamke zaidi ya mmoja, tunao uzoefu wa kumwaga na kumwagwa. Ukimwagwa unapata maumivu makali sana na kama kichwa chako hakina shock absorber na hauna mpango B utateseka sana. Hali kadhalika ukimwaga mtu, unaweza ukapata furaha mwanzo lakini kama huyo uliyemwaga alikua ni for real, maumivu makali utayapata baadae, tena pale unapojaribu kumrudia ikashindikana. Nasaha yangu ni kwamba usivunje mahusiano, acha muda uyauvunje, kuna wakati unaotokea mnaachana na mtu bila ata ya kusema neno lolote na kila mtu anafurahia.
Ila Mkuu lugha uliyoanza nayo kidogo.....
But ujumbe uliomalizia nao ni mzuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom