Share nasi: Ulijisikiaje siku mpenzi wako unayempenda aliposema mimi na wewe basi?

Heloo

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
4,391
3,402
Mapenzi yana raha pia mapenzi yanatesa sana sana.

Tena unaweza umwa na dawa hakuna hasa kwa mtu uliyeplan naye vitu vingi na pengine kumtambulisha kwa jamaa na marafiki.

Yumkini sasa hivi upo na mpenzi mpya au umeoa ama kuolewa na mambo ni mazuri. But, hii haibadilishi ukweli kwamba umewahi kupatwa na mkasa tajwa hapo juu.

Je ulijisikiaje na uliponaje maumivu hayo na sasa una furaha na maisha mengine?

Tushirikishe ili aliyepo kwenye maumivu sasa aone kumbe is not a big deal anaweza kuvuka.
 
Kwa wale ambao tumebahatika kuona uchi wa mwanamke zaidi ya mmoja, tunao uzoefu wa kuacha na kuachwa. Ukiachwa unapata maumivu makali sana na kama kichwa chako hakina shock absorber na hauna mpango B utateseka sana. Hali kadhalika ukimuacha mtu, unaweza ukapata furaha mwanzoni lakini kama huyo uliyemuacha alikua ni for real, maumivu makali utayapata baadae, tena pale unapojaribu kumrudia ikashindikana. Nasaha yangu ni kwamba usivunje mahusiano, acha muda uyauvunje, kuna wakati unaotokea mnaachana na mtu bila ata ya kusema neno lolote na kila mtu anafurahia.
 
Wengine wanafikiria ndio mwisho wa maisha.... kila baada ya jambo zito au wakati mgumu unaopitia jua kuna maisha melee yake.
 
Kwa wale ambao tumebahatika kuona uchi wa mwanamke zaidi ya mmoja, tunao uzoefu wa kumwaga na kumwagwa. Ukimwagwa unapata maumivu makali sana na kama kichwa chako hakina shock absorber na hauna mpango B utateseka sana. Hali kadhalika ukimwaga mtu, unaweza ukapata furaha mwanzo lakini kama huyo uliyemwaga alikua ni for real, maumivu makali utayapata baadae, tena pale unapojaribu kumrudia ikashindikana. Nasaha yangu ni kwamba usivunje mahusiano, acha muda uyauvunje, kuna wakati unaotokea mnaachana na mtu bila ata ya kusema neno lolote na kila mtu anafurahia.
Nimekuelewaaa sanaa mkuu
 
Nilijisikia amani coz angechelewa kidogo tu mimi ndo ningemwambia basi, nilishukuru coz kila mtu aliona chemistry haiendi yani no future ahead of us, kwakuwa niliamini kila kitu hutokea kwa sababu basi hata sikuwaza sana so tuliachana kiroho safi tu bila kununiana wala ugomvi, miaka ikapita na kila mtu hivi sasa ana new partner na maisha yakaendelea.

Huwaga sipendi kujikosesha amani kwajili ya mtu tulokutana ukubwani, kama niliweza kuishi kabla sijakutana nae siwez shindwa baada ya kuachana nae, japo haiwagi rahisi kihivyo kutokana na kumzoea mtu bt with time kila kitu kina come back to normal.
 
Nilifanyiwa roho mbaya na mdada x wangu wa kwanza kumpenda, kumbe tulipangwa kama mafungu ya nyanya. Nilipogundua nilimpiga chini mimi huku naumia kama nimeachwa.
Tabia ya kutopenda na kuthamini wanawake ndipo ilipoanzia, ikawa chapa ilale nakumbuka idadi ila majina nimewasahau
 
Mkuu sijui ulijuaje kama ndio napitia hii situation....unampenda mtu kwa moyo mmoja....lakini mwisho wa siku unaambulia maumivu.

Ila maisha lazima yaendeleee..ila kama una roho ndogo unaweza kujiuaa...ila ni mapito tu nayo yatapitaa
Vlad ana roho mbaya msamehe bure tu kadada
 
ha haha hahaaa haaaaa.
aisee mm niliona kizunguzungu ghafla baada ya kupokea txt toka kwa manzi baada ya mahusiano kudumu kwa muda wa wiki mbili tu.
mbaya zaidi kilichoniuma ni kwamba yule dem yeye ndio alijitongozesha kabla ya kuwa wapenzi mm sikuw na habar nae.
ila kiukwl ni mzur sana mpaka leo hii roho bado inaniuma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom