SHARE: Je, simu yako ikiwa kwenye 'DATA ON' Inakaa na charge kwa muda gani?

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
796
3,248
Kati ya vitu vinakera Basi nikutumia simu kwa mashaka ya kukuishia charge/kuzima kabla ya muda ambao hutarajii/hukupanga kuicharge.

Raha ya smartphone yeyote ni kuitumia kwa uhuru kadiri ya mahitaji yako ya siku nzima,

Uhuru huo ni uhakika wa kuitumia simu yako siku nzima kuanzia asubuh unapotoka nyumbn mpk jioni/usiku unaporudi ikiwa imebakia na asilimia kadhaa za charge bila kulazimika...

kuzima Simu, Data, kuweka ultra power saving au kuiweka kwenye Airplane mode.

Hata km una smartphone nzuri kiasi gani, ya bei kubwa kiasi gani, lkn km inakupa pressure ya kukuishia charge kana kwamba kila ukiitumia macho yapo kwenye battery percentage , ni wazi hio simu Haikupatii kile unachostahili.

Sikuhizi imekua kawaida kuona brother men au sista duu anatembea na charge mkononi au power bank, mwingine analazimika kubeba begi ili aweke charge na extension popote atakapofikia akiona socket roho haitulii..

Simu yako inakufanya unakua mtumwa,

Juzi pale Ubungo nishakata tiket ya seat yang, kabla ya gari kuondoka nikatoka mara moja, narudi kuna mshkaji amekaa, namuuliza kaka vipi mbona umehamia kwenye nafasi yangu?
Jamaa aliniomba kana kwamba anataka kulia....

"Bro nakuomba nikae hapa, pale kwenye seat yangu usb port ya kuchajia simu imeharika" nikaona isiwe tabu nimwachie mwana, ikabd niende kukaa kwenye seat yake, baada ya dk kadhaa akaja mtoto mzuri, namshukuru kwa hilo.

Hii imekua kawaida tunashuhudia, kuna watu wengne km basi haina USB port ya kuchajia simu hapandi, na wengi wasivyojua zile zina madhara sana kwenye simu.

Tuambie,
Simu yako inaweza kukuaa na charge mda gani?
Tushauri simu gani inakaa na charge vzr pengne huu utakua msaada kwa wengi...

Mimi natumia s7 edge, hii yangu ni almost masaa 9 au chini ya hapo nikiwa naperuzi muda mwingi....
Hili silifurahii na ninataka kubadilisha, kabla ya kubadilisha ningependa kujua ni simu gani inakaa vizuri na charge? Lkn pia iwe NZURI, Hii ndio screeshot yangu

IMG-20200409-WA0001.jpg
 
s7 edge inakaa masaa yote hayo duh,ila nilikiwa na s8 plus ilikuwa inakaa masaa 14 data on.ila on screen masaa 8.

sasa hivi niliyo nayo on screen masaa 7,data on masaa 12.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi vitu vimekua kama magari,ukitaka kagari kadogo kama ka Vitz utakuta hakali mafuta lakini perfomance ndogo,ukitaka gari kubwa kama Lancruiser V8 utakuta linakula mafuta na perfomance ni excellent,cha muhimu hapo kama unataka simu kali kubali kuendelea kuishi kwa mashaka,otherwise jiunge na watumia vitochi full charge unatumia wiki...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusiandikie Mate..
Soma hio shughuli ya Hii Samsung hapo RIGHT NOW RIGHT HERE
Screenshot_20200409_120527.jpg

Nikurahisishie
8.7 + 17.2 = 25.9hrs DATA ON.

Na ikiwa full charge NORMAL USE FULL CHARGE Soma hilo gap hapa
Screenshot_20200409_120643.jpg


Hili dude hata huo usiku na charge tu ilimradi, na hua sizimi DATA mm.
 
Tusiandikie Mate..
Soma hio shughuli ya Hii Samsung hapo RIGHT NOW RIGHT HEREView attachment 1413681
Nikurahisishie
8.7 + 17.2 = 25.9hrs DATA ON.

Na ikiwa full charge NORMAL USE FULL CHARGE Soma hilo gap hapaView attachment 1413683

Hili dude hata huo usiku na charge tu ilimradi, na hua sizimi DATA mm.
Dude gani hilo? Niliwahi sikia Samsung lakini betri zake huwa zinawahi kuchoka sijui ni kweli?
 
Dude gani hilo? Niliwahi sikia Samsung lakini betri zake huwa zinawahi kuchoka sijui ni kweli?

Samsung Galaxy A9 Pro 2016..
5000mAh
FB_IMG_15813399729418543.jpg
FB_IMG_15813399817695660.jpg
FB_IMG_15813391693235621.jpg
FB_IMG_15813391425645790.jpg
FB_IMG_15846834663893439.jpg

FB_IMG_15813391607094830.jpg

Hii simu ni Next level...

Kuanzia body, sreen, battery, audio quality, speed, camera n.k n.k.. , yani hata ikiwa mkononi texture yake tuu unaifurahia, Glass ya Maana, Aluminium pembeni,
Hapa ndio samsung walizitendea haki A-series, Achana na hizi za leo full body ni plastic, Nilikua na S9 plus nikafanya exchange nikarudi kwenye hii.

Unaweza ukaitumia kama siraha pia.
 
Hujanijibu kuhusu betri
Hio ni mentality ya watu waliyoijenga hasa kwa kuzingatia simu za nyuma km s4 na note 7, na sio kwa sbb nyingne bali battey capacity zilikua ndogo, pia kumbuka battery ya simu inashuka ubora kadr inavyotumika, wengi wanaonunua samsung wakiwa wanalalamikia battery ujue huyo kanunua Ikiwa refurb au mtumba kwaio hata battery health inakua ipo chini sanaa.

Na kwa sasa samsung ndio anaongoza kwa battery imara per usage, battery zao zinashuka kwa 2.5% kwa mwaka while kampuni nyingne nyingi ni 5%.

Ili uinjoy simu yako Chukua simu yenye battery angalau 3500mah IKIWA MPYA.

Lkn km hio simu ni flagshipe/high end kwa battery hio tarajia disappointment.
Sbb flagship nyingi zinakua na processor yenye uwezo mkubwa(hapa nazungumzia speed), refresh rate kubwa vitu ambavyo vina drain battery sanaa..
Ndio maana S20 ultra leo ana 5000mAh lkn ukaaji wake wa charge hauendani na battery kubwa kiasi hicho.

Wanaolia samsung hazikai na charge, wengi wananunua mtumba na refurb boss na mbaya zaidi hawajui,

Wao wakisikia full boxed, basi tayar wana amini kitu ni kipyaa....
 
Back
Top Bottom