Shanghai, China: Mwanamke akamatwa akiwa na mikoba iliyotengenezwa kwa Cocaine

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
6a497c170cc4c04fc6a34edae076fecf.jpg
Maafisa wa Forodha mjini Shanghai nchini China, wanasema kuwa wamemkamata mwanamke ambaye alijaribu kusafirisha mikoba miwili hadi nchini Uchina, ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa kutumia dawa ya kulevya ya cocaine.

Mwezi Februari mamlaka za viwanja vya ndege katika moja ya viwanja vya kimataifa mjini humo zilikagua kwa njia ya x-ray mkoba wa mwanamke ambaye alikuwa amesafiri kutoka nchi ambayo haikutajwa ya Amerika Kusini

Mashine ya x-ray ilionyesha kuwa mkoba wake ulikuwa mweusi kuliko kawaida na pia ukawa mzito hata ulipokuwa bila mzigo

Baada ya uchunguzi mkoba huo uligundulika kutengenezwa na karibu kilo kumi ya cocaine

Sheria za China zinasema kuwa yeyote ambaye atapatikana na hatia ya kusafirisha zaidi ya gramu 50 ya cocaine atanyongwa.

Chanzo: BBC
 
Pole yake high risk high return. I wonder why american hiphop culture glorify drug dealers.
 
Back
Top Bottom