Maonesho ya CIIE ya China yatoa jukwaa la mtandaoni kwa Afrika kutangaza bidhaa zake na kujikuza kibiashara

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
NA PILI MWINYI

VCG111258136755.jpg


Maonesho ya Nne ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China CIIE, yanayofanyika mjini Shanghai yamepata mafanikio makubwa na kutoa jukwaa muhimu sio tu kwa China kuendelea kufungua milango yake na kukuza ushirikiano wake wa kimataifa na biashara huria, bali pia kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi hasa wa Afrika kuonesha bidhaa zao, kubadilishana uzoefu wa kufanya biashara, kutafuta soko la kimataifa pamoja na kutoa fursa za uwekezaji.

Mwaka huu karibu makampuni 3,000 kutoka nchi na sehemu 127 yamejitokeza kushiriki. Wakati janga la virusi vya Corona likiendelea kuitafuna dunia na kuleta uharibifu mkubwa, maonesho mengi makubwa ya kimataifa yamesitishwa, lakini maonesho ya Uagizaji Bidhaa ya China CIIE ya Shanghai yanaendelea kama yalivyopangwa, huku umaarufu wake ukiongezeka kila mwaka. Swali la kujiuliza ni je, nini hasa siri ya China kuweza kujiamini na kunuia kushinda taabu na changamoto hadi kuweza kufanya maonesho haya kwa mafanikio makubwa bila ya kuahirisha au kuyafuta?

Siri ya mafanikio haya naweza kuielezea kwa maneno ya rais Xi: "CIIE imewezesha bidhaa zinazooneshwa kuweza kuuzika na waoneshaji kuona fursa zaidi za uwekezaji."

Kwa mujibu wa bodi ya CIIE mwaka huu, nchi 58 na mashirika matatu ya kimataifa yamejiunga kwenye maonesho haya kwa njia ya mtandaoni, miongoni mwao nchi 15 zitakuwa ndio mara yao ya kwanza kushiriki. Wakati huohuo, makampuni 90 kutoka nchi 33 zinazoendelea pia yatashiriki kwenye maonesho haya.

Afrika, ambayo nchi zake nyingi zinafanya biashara na China, hii imekuwa ni fursa ya pekee kuonesha bidhaa zao kwa wenzao wa China. Miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zimekuwa na ushiriki mkubwa ni Rwanda. Nchi hii imeleta bidhaa zake bora kabisa zikiwemo kahawa, chai, pilipili na mafuta ya zeituni. Safari hii Rwanda itakuwa inashiriki kwa mara ya nne mfululizo kwenye maonesho haya, ikimaanisha kuwa imeanza kushiriki tangu maonesho ya kwanza kabisa kuzinduliwa mwaka 2018.

Mbali na Rwanda, Ethiopia nayo pia imeamua kutumia fursa hii adhimu kujitangaza na kujikuza kibiashara, ambapo mamlaka ya Kahawa na Chai ya nchi hiyo (ECTA) inaona maonesho haya yatarahisisha maingiliano kati ya wafanyabiashara wa Ethiopia na wanunuzi wa kahawa ya nchi hiyo wa China, pamoja na kupiga jeki usafirishaji wa kahawa nchini China.

Shafi Oumer, naibu mkurugenzi mkuu wa ECTA, anasema awali makampuni ya China yalijadiliana na wasafirishaji wa kahawa wa Ethiopia, ambapo upande wa China umetekeleza kwa vitendo na kuleta matokeo mazuri juu ya mambo yaliyojadiliwa, na sasa wamechangia usafirishaji wa kahawa ya Ethiopia nchini China katika miaka mitatu iliyopita. Ethiopia ni maarufu kwa kahawa yake isiyowekwa kemikali na ni kitovu cha kahawa yake ya Arabika.

Wakati huohuo Tanzania ikiwa mshiriki wa maonesho mengi yanayofanyika China, nayo pia imeshiriki kwenye maonesho ya safari hii ambayo yamekuwa jukwaa kubwa la manunuzi na mabadilishano ya utamaduni duniani katika miaka mitatu iliyopita. Makampuni ya Tanzania yanashiriki maonesho haya kwa njia ya mtandao, ili kutambulisha na kutangaza bidhaa mbalimbali zenye ubora wa hali ya juu nchini China, zikiwemo kahawa, korosho, mvinyo, pamoja na madini ya vito kama vile Tanzanite.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na forodha ya China, Afrika inazidi kuimarisha ushirikiano wake wa kibiashara na China, ambapo mwaka huu biashara ya pande mbili imekuwa kwa asilimia 40 kuliko mwaka jana na kufikia thamani ya $162.7 bilioni katika miezi minane ya mwaka huu. Hata hivyo bara la Afrika bado lina urari mbaya wa biashara na China, ndio maana China inajitahidi kutafuta ufumbuzi kwa kuanzisha majukwaa kama haya ya biashara na kuyapatia fursa makampuni ili kuinua usafirishaji wake wa bidhaa.

Makampuni makubwa ya China pia yanatoa usaidizi wake kwa Afrika. Kampuni inayofanya biashara zake mtandaoni ya Alibaba imesaini makubaliano na Angola, Afrika Kusini na hivi karibuni, Misri, ili kuongeza usafirishaji bidhaa wa mazao ya kilimo hasa chakula nchini China.
 
Hao washenzi watacopy kila kitu kesho mtakuta bidhaa zote mlizowapa sample wanauza k;koo.
 
Back
Top Bottom