Mtanzania akamatwa na dawa za kulevya China

Mocumentary

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
769
1,959
Raia wa Tanzania aliyefahamika kwa jina moja la Dossa amekamatwa katika Mji wa Macau, China kwa madai yakusafırisha dawa za kulevya aina ya cocaine.Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza kuwa raia huyo aliyekua akiendelea kukaa nchini humo licha ya muda wake kuisha amekamatwa akiwa na gramu 15 za cocaine, takribani gramu2.5 za dawa ambazo hazijulikani na fedha takribani TZS 9.6milioni zilikutwa kwenye makazi yake. Dawa zilizokamatwa zimeripotiwa kuwa na thamani ya TZS14.4 milioni.

Afisa wa serikali nchini humo, Lei Hon Nei amesema Dossa mwenye umri wa miaka 39 ana hati ya kusafıria ya Tanzania na alikaa nchini humo licha ya kibali chake kumalizika.Lei amesema maafisa wa forodha wa Hong Kong walitoa taarifa kuhusu kipeto chenye uzito wa 1kg kilichowasili Macau kutoka Ulaya. Kwa mujibu wa Idara hiyo, kipeto hicho kilikuwa na cocaine na Dossa ndiye mpokeaji na alieleza alipo. Mtuhumiwa huyo amesema kuwa alinunua dawa hizo kutoka mgeni mjini Macau kwa 290,000 kwa ajili ya matumizi binafsi.

Mtuhumiwa alikanusha kusafırisha dawa hizo na alipopimwa akakutwa na cocaine mwilini. Anashtakiwa kwa matumizi haramu na usafirishaji wa dawaza kulevya.

Swahili time.
 
China ni mahali hatar sana dunian hasa ukijijua ww ni mtumiaji au muuzaji wa dawa za kulevya wether cocain,heroin,meth etc
Haijalishi ww unatokea nchi gani hata iwe canada,Uk,US etc

Dawa yako ni kifo au kifungo cha maisha
 
Katika vita ambavyo Magufuli amevipigana kwa ujasiri na kuelekea kupata ushindi basi ni dhidi ya dawa za kulevya. Wabongo tukiingia baadhi ya nchi tunaangaliwa kwa tahadhari sana

Sasa hivi hata mateja mitaani wamepungua kwa kiasi kikubwa. Inavyoonekana kuna watu wakubwa tu walikua wanashiriki kwenye hii biashara inayoharibu nguvu kazi ya Taifa na sasa hivi wamedhibitiwa
 
Hawa wanayoyatafuta majanga shauri zao. Hakuna njia nyepesi kwenye mafanikio. Mpaka sasa nahangaika kutafuta muuza vibubu maana yule wa awali bado hali tete mahakamani
 
Kapicha kangependezesha sn story.... Unaweza kura ni mtoto wa kitaa kwetu kabisa
 
Back
Top Bottom