Shamsa Ford: Punguzeni kuniomba fedha

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,365
8,097
Pesa-Fedha-780x470.webp

Mwigizaji Shamsa Ford amesema watu wamekuwa wakimpigia simu na kumtumia ujumbe kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii kumwomba fedha.

Nyota huyo alisema kuna mtu aliomba amsaidie Sh milioni 22 akamalizie nyumba yake, akisema yeye hana fedha kwani anapambana na mikopo ili maisha yake yaende.

“Hii ni mara ya sita kupigiwa simu na meseji nyingi kuniomba pesa. Huyu wa leo (jana) alisema anaomba nimsaidie Sh milioni 22 akamalizie nyumba yake, mimi mbona sina mbwembwe zozote zinazoonesha nina pesa,” alisema na kuongeza:

“Jamani kuonekana kwenye televisheni haimaanishi nina pesa nyingi. Mimi mwenyewe napambana na mikopo, michezo ya vikoba ili maisha yaende, ndugu zangu punguzeni kuniomba pesa sina kitu,” alisema hayo Dar es Salaam jana.

Shamsa amekuwa akiigiza kwenye tamthiliya mbalimbali za televisheni na pia ni mjasiriamali wa nguo. Amekuwa akifanya shughuli hizo kuendesha maisha yake kwa muda mrefu.

HABARI LEO
 
Kama kaka hakimi vile, Nae Hana kituView attachment 2591717
Nimezistudy sura zao nimebaki kufurahi!
Sura ya hakim umejaa bashasha na furaha,haina wasiwasi,ukiingalia vizuri Kabla hatujajua mipango yake tungesema Hakim kakamatika Sana na bi dada Yuko I love🤣🤣kumbe ulikuwa bashasha ya kutokuwa na wasiwasi wowote

Upande wa bidada sura yake imekaa kimkakati Sana yaani unamuona kabisaaa Kuna mipango kichwani mwake humo🤣bahati mbaya mission impossible
 
Mwanaume akikwambia, wewe ndiye kitu changu cha thamani pekee dunia...umeumia😂😂😂😂

Wapendwa, uso ws mtu huongea kila kitu kimjazacho moyo, sema watu tu wabishi sana kuukubali ukweli.
Mimi kabla sijadeti na mtu huwa nakusoma uso, haijalishi utatamka mara ngapi kuwa wanipenda....taarifa ya kupendwa au kupangiwa mipango huwa naisoma udoni mwa mtu wangu haha
Joannah
 
Mwanaume akikwambia, wewe ndiye kitu changu cha thamani pekee dunia...umeumia

Wapendwa, uso ws mtu huongea kila kitu kimjazacho moyo, sema watu tu wabishi sana kuukubali ukweli.
Mimi kabla sijadeti na mtu huwa nakusoma uso, haijalishi utatamka mara ngapi kuwa wanipenda....taarifa ya kupendwa au kupangiwa mipango huwa naisoma udoni mwa mtu wangu haha
Joannah

Na mwanamke akikuita Honey, kipenzi changu, wa ubani, wa moyoni duuu yote hiyo utume hela

Kweli kuna utapeli na sio mapenzi
Anaekupenda hana shobo zote hizo
 
Hawa viumbe baadhi yao ni majambazi kupitia neno mapenzi, ukichunguza vizuri yaani hata hupendwi wewe bali mfuko.
dronedrake amejikomboa kutoka huu utumwa.
mzabzab yeye anabadilishana nipe nikupe.
DeepPond yeye zaidi ya kodi ya meza na kulipia mahali pa kumchinjia mamajay basi mengine hataki kusikia.🤣🤣🤣
 
Mwanaume akikwambia, wewe ndiye kitu changu cha thamani pekee dunia...umeumia😂😂😂😂

Wapendwa, uso ws mtu huongea kila kitu kimjazacho moyo, sema watu tu wabishi sana kuukubali ukweli.
Mimi kabla sijadeti na mtu huwa nakusoma uso, haijalishi utatamka mara ngapi kuwa wanipenda....taarifa ya kupendwa au kupangiwa mipango huwa naisoma udoni mwa mtu wangu haha
Joannah
Sure!sura ya mtu unaongea Sanaa!tena mtu mpya ndio utajua kabisa Kama ana Nia ovu au njema angalia macho yanasema kila kitu Ni vile tu watu huwa tunapuuzia kukubali ukweli
 
Pesa-Fedha-780x470.webp

Mwigizaji Shamsa Ford amesema watu wamekuwa wakimpigia simu na kumtumia ujumbe kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii kumwomba fedha.

Nyota huyo alisema kuna mtu aliomba amsaidie Sh milioni 22 akamalizie nyumba yake, akisema yeye hana fedha kwani anapambana na mikopo ili maisha yake yaende.

“Hii ni mara ya sita kupigiwa simu na meseji nyingi kuniomba pesa. Huyu wa leo (jana) alisema anaomba nimsaidie Sh milioni 22 akamalizie nyumba yake, mimi mbona sina mbwembwe zozote zinazoonesha nina pesa,” alisema na kuongeza:

“Jamani kuonekana kwenye televisheni haimaanishi nina pesa nyingi. Mimi mwenyewe napambana na mikopo, michezo ya vikoba ili maisha yaende, ndugu zangu punguzeni kuniomba pesa sina kitu,” alisema hayo Dar es Salaam jana.

Shamsa amekuwa akiigiza kwenye tamthiliya mbalimbali za televisheni na pia ni mjasiriamali wa nguo. Amekuwa akifanya shughuli hizo kuendesha maisha yake kwa muda mrefu.

HABARI LEO
Uwenda wanamuomba game wampelekee moto ila yeye anadhani wanamuomba pesa
 
Back
Top Bottom