Shambulio la Lissu kupigwa risasi: Polepole aibua mapya

Shambulio la Lissu kupigwa risasi: Polepole aibua mapya

Dereva wa lisu ,wafungua mageti , cctv wote ni shahidi muhimu lazima wahojiwe
Wameshahojiwa au kuna utaratibu wa ni lazima aanze dereva? Huenda nikawa sahihi kwasababu hakuna aliyehojiwa hadi sasa!
 
polepole.jpg

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenenzi, Humphrey Polepole amefunguka na kuhoji kuhusu kitendo cha CHADEMA kumficha dereva aliyeshuhudia tukio zima la shambulio la risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na amewataka wananchi wa jimbo la Siha kumhoji Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aeleze sababu za kufanya hivyo.

Ametaka kuhoji siri iliyopo inayowafanya CHADEMA wamfiche dereva huyo wakati anahitajika kuisaidia Serikali kufumbua ukweli na kumjua aliyehusika katika shambulio hilo.

Hivi huyu polepole yupo timamu kweli? Akipatikana dereva wa lissu hao watu wasiojulikana watapatikana baada ya kuhojiwa? Vipi dereva wa Lissu angekufa katika shambulio lile ina maana intelijensia ya jeshi la polisi ingekuwa nayo imekwisha?

Siasa za CCM kupitia huyu jamaa ni mufilisi kabisa.
Maskini Pole pole umefufua maiti!! Kha!! utajuta kwenye hizi kampeni sasa utakuwa muafaka kuchambua uhusika wa serikali kwenye hili shambulio!! Kwishney umejimaliza!! Wenzako walinyamaza wakingojea atakayemtaja muuaji mkuu wamshitaki sasa wewe umechokoza nyuki!!!!
 
Kuna siri kubwa sana .... sasa hawa machadema wanamficha nn dereva???
Yaani huelewi hata ukubwa na upana wa vyombo vyenu vya dola kuwa hakuna sehemu wanazokosa kuzifikia kwani wana mikono na macho marefu! Yaani ujifiche wapi wasikupate? Ukisema wanabuy time ili wasiumbuke kwa kile atakachosema utaeleweka vema zaidi!
 
Yaani wewe na hao ccm wenzako mmebeba mapapai yaliooza badala ya vichwa! Yaani huelewi hata ukubwa na upana wa vyombo vyenu vya dola kuwa hakuna sehemu wanazokosa kuzifikia kwani wana mikono na macho marefu! Yaani ujifiche wapi wasikupate? Ukisema wanabuy time ili wasiumbuke kwa kile atakachosema utaeleweka vema zaidi!
Wacha ulongoulongo wako..... chadema mnakijua mlichomfanyia Tundu
 
Utafit unaonyesha jeshi letu linaongoza kwa IQ ndogo barani Africa
Sijui ni ueledi gani walionao aisee hawa polisi wetu.
Leo hatujui nn kuhusu wale watoto 1,300 wa kibiti. Hatujui hatma ya wanaookotwa baharini. Hatuna majibu ya Ben sanane. Hatujui alipo mwandishi Azatory..

Lakini bado jeshi la polisi wanasema wapo kazini. Kazi gani ..
 
Wacha ulongoulongo wako..... chagadema mnakijua mlichomfanyia tundu
Kwa mtazamo wako upo sahihi but kuwa mzalendo basi ukamsaidie kamanda wa dodoma anayeshughulikia kadhia hii ushahidi ulio nao juu ya uhusika wa cdm? Vinginevyo wewe sio mzalendo bali mzandiki!
 
Huyu ni Mr slow slow anaijua siasa ya aliniacha mno nani hamjui wakati wa mapendekezo ya katiba mpya? Hebu muulizeni Leo anasemaje.atakujibu bado hajaenda jandoni.
 
polepole.jpg

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenenzi, Humphrey Polepole amefunguka na kuhoji kuhusu kitendo cha CHADEMA kumficha dereva aliyeshuhudia tukio zima la shambulio la risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na amewataka wananchi wa jimbo la Siha kumhoji Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe aeleze sababu za kufanya hivyo.

Ametaka kuhoji siri iliyopo inayowafanya CHADEMA wamfiche dereva huyo wakati anahitajika kuisaidia Serikali kufumbua ukweli na kumjua aliyehusika katika shambulio hilo.

Hivi huyu polepole yupo timamu kweli? Akipatikana dereva wa lissu hao watu wasiojulikana watapatikana baada ya kuhojiwa? Vipi dereva wa Lissu angekufa katika shambulio lile ina maana intelijensia ya jeshi la polisi ingekuwa nayo imekwisha?

Siasa za CCM kupitia huyu jamaa ni mufilisi kabisa.
Mbowe ana akili nyingi kumzidi huyo kijana mara mia.
 
Huyu buana mudogo sijui alisomea wapi propaganda! Kufikiri polepole kuna madhara yake.Yaani hii nayo inakuwa ajenda kwenye kampeni?
 
I can bet my last coin, in a few years to come this country will have a truth and reconciliation commission na kuna watu hawatamani kuwa hai.
 
Wewe ndo una argue poorly. Sifikiri hata kama umesoma critical thinking. Uwezo wako ni mdogo sana.Shuhuda namba moja ni dereva sio camera wala walinzi.Hata kama hao watahojiwa vipi lkn bado polisi haiwezi hitimisha uchunguzi bila shahidi namba moja kuhojiwa.Hao wengine ni aids za uchunguzi tu na hutumika ku reinforce ushahidi wa shahidi namba moja.huko ufipa aliyewaroga cjui nani kiasi kuwa vipofu msione umuhim wa shahidi namba moja kuhojiwa.Camera na vitu vingine vinaweza forged tu,lkn kama dereva atatoa yake mwenyewe ni rahisi sana.

Acha upumbavu,unajua maana ya critical thinking au unaropoka?Mtu wa kwanza kuitwa polisi ni Mlinzi na siyo DEREVA ,dereva ni muhanga na shahidi.

Hiyo ELIMU ya Lumumba peleka huko huko Lumumba.Hakuna kitu cha ati Camera inakuwa forged sawa,kawadanganye hao wapuuzi wenzako huko waelewa tunalijua na huyo mburura Polepole analijua.

Kwa Polisi makini Polepole alitakiwa kuitwa ili atoe ushahidi waanacho kijua,lakini hawa Policcm wanafikiria kiCCM tu.

Rafiki Muda ni dawa ya kila ugonjwa mtakuja umbuka kama ya Imran Kombe au Dr. Ulimboka,inshort acheni kuua WATANZANIA wasio na hatia
 
Si atokee mafichoni kuua mzizi wa fitina? Anajificha mpaka lini, unajua ushabiki ni ugonjwa mbaya sana! Ivi dereva huyo angekuwa ni mtu ambaye hakuwa anamwendesha Lisu angefichwa kweli?

Mbona dereva wa Marehemu cha cha wangwe alishikiliwa hakukimbizwa na mbowe? Jamani dereva rudi upambane na mkono wa Sheria wewe ni mtu muhimu kuhojiwa ni kawaida sana usihofu

Kwa kesi yoyote mtuhumiwa wa KWANZA ni mlinzi,mpaka leo wameitwa walinzi wa jengo husika?Hivi Polepole anavyoropoka kwa Polisi inayojiamini na kusimamia sheria na taratibu za kipolisi angekuwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kutoa ushahidi wa anachokijua,ukiona kimya ujue ni upumbavu tu unaosemwa lakini hata yeye moyoni mwake anajua anachokiongea hakipo.

Cha msingi acheni kuua raia wasio na hatia
 
Hivi mtu akijiunga ccm huwa akili na ufahamu unapotea au? Ni aibu kwelikweli na sitaki kuamini ujinga kama huu kusemwa na mtu niliyekuwa namheshimu na kumwona ana akili zake!
 
Back
Top Bottom