Shamba la ng’ombe lililoacha gumzo ziara ya Pinda Uarabuni

Shamba la ng’ombe lililoacha gumzo ziara ya Pinda Uarabuni

komeka

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2013
Posts
1,072
Reaction score
404
pinda.jpg

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa na meneja wa shamba, Ahmed Al Mansour. wakati wa msafara wa kukagua na kujifunza kuhusu mradi huo wa shamba la ng'ombe. Picha na Ibrahim Bakari

Ukiingia kwa gari, iwe kubwa au dogo, lazima litamwagiwa dawa kuua wadudu ama vimelea vya magonjwa.Baada ya ukaguzi wa gari, kinachofuata ni kufunguliwa bomba maalumu za dawa kwa ajili ya gari iwe kubwa au dogo.

Pia, kuna kijibwawa chenye maji ya dawa ili kuua bakteria wa magonjwa kwenye matairi. Kila gari lazima litumbukie kwenye ‘kibwawa' hicho wakati wa kuingia na kutoka.

Shamba hilo la ng'ombe wa maziwa la Al Rawabi, lipo eneo la jangwa. Sehemu kubwa ya Dubai iko jangwani, lakini imeendelezwa.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alikuwa na ziara ndefu kutembelea nchi za Dubai na Qatar yenye lengo la kutafuta wawekezaji, fursa za biashara pamoja na kudumisha ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hizo za Kiarabu.

Wakati wa ziara yake, Waziri Mkuu na ujumbe wake, alipata fursa ya kutembelea shamba hilo na kujionea shughuli mbalimbali kuanzia utunzaji, kulisha, kukamua, uhifadhi wa maziwa, kuzalishwa kiwandani, kufungwa hadi kumfikia mlaji.

Katika ziara hiyo aliyofuatana na mawaziri, wakuu wa mikoa na wabunge, kati ya vitu vilivyovutia zaidi ni shamba hilo la ng'ombe lililopo jangwani, lakini ngombe wake wote wana afya, wanakula vizuri na hata kutoa maziwa kwa wingi.

Kwanza; aina ya ng'ombe wanaotunzwa hapo hadi uzalishaji wa maziwa.

Meneja wa shamba hilo, Ahmed Al Mansour, anasema kuwa walianza na ng'ombe 500, lakini sasa wana ng'ombe 12,000.

"Shamba hili ni muungano wa wafugaji watano ambao walikuwa na lengo moja la kuzalisha maziwa, walipeleka mapendekezo serikalini na serikali ilikubali kusaidia kama kikundi kwa baadhi ya maeneo," alisema.

Alisema kuwa Serikali imewapa msaada wa kutosha katika kufanikisha kazi zao.

Mifugo

Eneo la mifugo limetengwa kulingana na aina ya ng'ombe. Kuna eneo maalumu kwa ng'ombe wanaozaliwa, eneo la ng'ombe wanaoendelea kukua na maeneo mengine ni kwa ng'ombe waliokamilika.

Ng'ombe mmoja aliyekamilika, hutoa lita 64 za maziwa. Ng'ombe wa kawaida wa Tanzania hutoa wastani wa lita 15 hadi 20 kwa siku ikiwa ni mara tatu ya ng'ombe hao.

Ng'ombe hao huangaliwa saa 24 na madaktari wa mifugo wapatao 300 ambao hupokezana kwa zamu.

Katika eneo la kukamulia, ni mashine tu ndizo zinazofanya kazi na mashine za kukamua zimeunganishwa na mipira maalum ambayo huyapeleka maziwa moja kwa moja kiwandani. Eneo la shamba kuna kiwanda cha kusindika maziwa katika ujazo mbalimbali na kupelekwa katika masoko ya ndani na nje ya Dubai.

Kiwanda cha Al-Rawabi kilichoanzishwa miaka 25 iliyopita, ndicho kinachotoa huduma ya maziwa Dubai nzima.

Al Mansour anasema ng'ombe pamoja na shamba kuwa na ng'ombe wengi, lakini wote huogeshwa na wanapolala hujisikia raha.

Anasema kuwa kama shamba, walitengeneza mabomba ya majosho ya kutosha kwa ajili ya kuwaogeshea.

Al Mansour anasema pia kuwa kati ya ng'ombe 12,000 zaidi ya ng'ombe 3,000 huwa na mimba na hutoa maziwa mengi na hupatiwa huduma maalumu na hawa huogeshwa mara tatu kwa siku na hata kabla ya kukamuliwa.

Ng'ombe wengine huogeshwa mara moja kwa siku na pia hulishwa zaidi chakula, mashudu, mahindi na majani vijavyotengenezwa na kiwanda kilichopo eneo hilo.

Chakula kinachotengenezwa kina mchanganyiko wa vitamini kinachosaidia wazalishe maziwa zaidi.

Anasema huagiza majani kutoka Afrika Kusini, Marekani na nchi nyingine za Ulaya tani kwa tani na huwa na akiba ya muda mrefu.

Katika shamba hilo, kuna kitengo cha kuhifadhia chakula hicho na mashine za kuchanganya majani hayo makavu na vitamini.

Hamad anasema kuwa mara nyingi wakati wa joto, uzalishaji maziwa hupungua kwa asilimia 40, lakini kinachofanyika ni kuhakikisha ng'ombe wanaishi katika mazingira mazuri kwa kujenga maeneo yanayotengeneza ubaridi.

Mabanda mengi yamefungwa feni kubwa pamoja na mabanda yenye kutengeneza ubaridi kwa ajili ya kipindi cha joto na mpango umesaidia kupunguza kiasi cha joto kutoka nyuzijoto 50 hadi 30.

Meneja wa Kitengo cha Uzalishaji, Nasser Hassan anasema kuwa miezi ya Juni, Julai na Agosti huwa ya joto kali na kupunguza uzalishaji wa maziwa.

Hata hivyo, anasema kuwa pamoja na changamoto hizo, mpango uliopo ni kuongeza uzalishaji hadi kufikia lita 170,000 na zaidi ni lita kufikia 200,000 kwa siku.

Kwa sasa, katika saa 21 kila siku, ng'ombe 210 wanakamuliwa ndani ya dakika saba.

Aina ya ng'ombe wanaofugwa hapo ni maalumu kwa kutoa maziwa mengi na hupatikana zaidi Uholanzi na Ujerumani.

Mpango mwingine endelevu uliopo ni kufungua shamba kama hilo, eneo la Liwa, Abu Dhabi umbali wa kilomita 120 likianza na ng'ombe 6,000.

Mashamba hayo yanalengwa katika masoko yote ya Falme za Kiarabu, Qatar na Oman ndani miaka mitano ijayo.

Waziri wa Mifugo

Akizungumzia hali hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani anasema kuwa atapeleka wataalamu wake wa mifugo kuona jinsi gani ya kuanzisha mashamba hayo Tanzania.

Akizungumza baada ya kutembelea shamba hilo, Dk Kamani anasema kuwa Tanzania ina maeneo ya kutosha kwa ufugaji, majani na maji ikilinganisha na Dubai ambao sehemu kubwa ni jangwa.

"Tutakwenda kuangalia muundo wa Ranchi ya Ruvu na Kongwa kuona jinsi ya kuziendeleza kwa kufuga ng'ombe wa kisasa wa maziwa kama ilivyo kwa Al Rawabi," alisema.

Dk Kamani alisema pia kuwa wanataka kuunganisha wafugaji kuona jinsi gani wanaweza kufikia lengo kama ilivyo kwa shamba la Al Rawabi.

Chanzo
:Mwananchi
 
Hawa viongozi, badala ya kwenda nje kushangaa ufugaji, waende Kitulo na hata Uyole kujionea mafanikio lakini pia changamoto zitokanazo na ukosefu wa pesa ambazo zinawafanya washindwe kuzalisha ng'ombe wa kutosha kukidhi soko.

Tanzania kama nchi inayokabiliwa na uhaba w ajira. Hatuhitaji mashamb makubwa makubwa ya ufugaji, tunahitaji kuwawezesha vijana wengi ili wafuge ng'ombe wanaofaa wa maziwa na hivyo kutengeneza ajira nyingi kwa vijana.
 
Hawa viongozi, badala ya kwenda nje kushangaa ufugaji, waende Kitulo na hata Uyole kujionea mafanikio lakini pia changamoto zitokanazo na ukosefu wa pesa ambazo zinawafanya washindwe kuzalisha ng'ombe wa kutosha kukidhi soko.

Tanzania kama nchi inayokabiliwa na uhaba w ajira. Hatuhitaji mashamb makubwa makubwa ya ufugaji, tunahitaji kuwawezesha vijana wengi ili wafuge ng'ombe wanaofaa wa maziwa na hivyo kutengeneza ajira nyingi kwa vijana.

wenzako wako picnic
 
Huyo waziri wa mifugo ni mat&@#!ko, inamaana bila hiyo ziara wizara yake haina mpango wowote na hizo ranch za ruvu na kongwa.
 
Hata chuo cha Mpwapwa kinahizo huduma kasoto hela za kukimanyain.
 
Hahahahahaaaaa na yeye angewafundisha ufugaji wa Nyuki..... Kwani hakwenda nao wa sample? Kwa hapa Tanzania Ukija na idea ya namna hio lazima siasa ziingizwe. Trust me
 
hao warabu mazingira yao ni magum sana kwa ufugaji ila wameweza zaidi yetu! tumewapa wanyama pori bure tutegemeye ifikapo 2025 kwenda kushangaa wanyama pori kama waziri mkuu alivyokwenda kushangaa ngombe !!
 
Kama ziara za kujifunza mbona viongozi wetu wamebobea; hakuna hakuna hata siku 1 walipoweza kufanya yale waliojifunza toka hizo nchi nyingine; wakisikia mtu mweusi Mtanzania kafanya robo ya hilo tu utasikia vita atakayopigwa na hawa waungwana.
Ni nchi hizi hizi za Kiarabu ambazo wameweka sera nzuri ya uwekezaji kwamba mgeni yoyote atakae kwenda kwao hata na mtaji wa kuinunua dunia yote lazima atafute mbia/share holder mzawa, hapa kwetu tunajua kinacho wapata wawekezaji wazawa (mfano Mengi). Jambo hili hawa akina Pinda wanalifahamu vizuri sana, hi ziara nayo itakua kama tour kama zingine tu, nikiliona badiriko lolote kwa hawa watu basi nitajua nipo ndotoni lakini sio hawa akina pinda.
 
Mdau anaejua kiarabu awatahadharishe hawa mabwana na ugeni kutokea huku, mifugo yao inaweza kuambukizwa maradhi wapate hasara kubwa. Huku kwetu tangu miaka ya uhuru mpaka sasa maradhi ni adui wa maendeleo bado tunaendelea kutafuta ufumbuzi wake. Hukawii kusikia wameambukizwa mafua ya nguruwe.

Ukitumia akili kidogo utaona ziara hii inatokana na kuiga/ kujibu ile ya mkuu ya vietenam.
 
Hawa viongozi, badala ya kwenda nje kushangaa ufugaji, waende Kitulo na hata Uyole kujionea mafanikio lakini pia changamoto zitokanazo na ukosefu wa pesa ambazo zinawafanya washindwe kuzalisha ng'ombe wa kutosha kukidhi soko.

Tanzania kama nchi inayokabiliwa na uhaba w ajira. Hatuhitaji mashamb makubwa makubwa ya ufugaji, tunahitaji kuwawezesha vijana wengi ili wafuge ng'ombe wanaofaa wa maziwa na hivyo kutengeneza ajira nyingi kwa vijana.

Haya ndo wanapaswa kuyafanya lakini hawa watawala wetu kawaida yao na furaha yao kuona mtanzania anaendelea kuwa manamba ila sio kumsaidia kutoka chini kwenda juu nadhani mnayaona na kusikia yanayowapata wakulima wa miwa,mchele,mahindi hata wachimbaji wadogo,kwa mujibu wa taarifa hiyo hao jamaa waliiomba serikali yao ikawasaidia na ndo maana wako hapo ila serikali hii ya ccm inajua kuwaangamiza wakulima wake wali wanao lima miwa waliokuwa na mikopo ndo wamefilisika tayari miwa haiuziki tena maana sukari ya nje imejaa tele ya ndani haiuziki
 
Akizungumzia hali hiyo, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani anasema kuwa atapeleka wataalamu wake wa mifugo kuona jinsi gani ya kuanzisha mashamba hayo Tanzania. Akizungumza baada ya kutembelea shamba hilo, Dk Kamani anasema kuwa Tanzania ina maeneo ya kutosha kwa ufugaji, majani na maji ikilinganisha na Dubai ambao sehemu kubwa ni jangwa. “Tutakwenda kuangalia muundo wa Ranchi ya Ruvu na Kongwa kuona jinsi ya kuziendeleza kwa kufuga ng’ombe wa kisasa wa maziwa kama ilivyo kwa Al Rawabi,” alisema. Dk Kamani alisema pia kuwa wanataka kuunganisha wafugaji kuona jinsi gani wanaweza kufikia lengo kama ilivyo kwa shamba la Al Rawabi. Chanzo:Mwananchi

Yaani ina maana semina elekezi, mipango mkakati ya wizara, na ziara za kujifunza pale waziri alipopata kuandamana na Mhe Rais walikuwa hawajapata kujipanga vizuri hadi wanataka kulazimisha kupeleka wataalamu wetu wakajifunze namna ya kufuga ngombe ambao licha ya mangione wanaishi mabanda airconditioned na wanakula nyasi imported!!! Hii ni biashara kichaaaaaaa, Waziri atafute eneo jingine la kupigia paranja!!

View attachment development_strategy-_Livestock_sw.pdf
View attachment Livestock_Programe_sw.pdf
View attachment Hotuba-ya-Bajeti-tarehe-12-Mei-2014-draft.doc
 
Kuna mkulu fulani alienda Zimbabwe na kuwashangaa ng'ombe walio na uzito mkubwa. Alitaka na maofisa wetu wa mifugo waende huko wakajifunze. Waswahili wakamwambia kuwa Kitulo kuna ng'ombe wakubwa zaidi yao!
 
kwan hela wanazopiga na kutumia ktk ziara si ndo hizo wenzao wanazielekeza kwenye miradi....watashangaa sana.....
 
Ngamia si wanastawi sana huko jangwani? Tena nasikia maziwa yake mazuri sana hata Mtume aliyatumia kama dawa na nyama yake ni aghali na inaheshimika sana; kama ndivyo ya nini kuhangaika na mang'ombe ya kijerumani na kidachi yaliyozoea baridi kali? Ya nini kuingia gharama kubwa kuyatengenezea AC na dawa lukuki? Eti madaktari 300 wa ng'ombe; duh!
 
Subiri baada ya muda utasikia mabilioni ya tena ya manunuzi ya viyoyozi vya kufunga kwenye mabanda ya ng'ombe mtabaki midomo wazi!!!!
 
Hapo mawazo hayapo kwenye ziara kabisa, wanawaza watapata wapi zingine za kupiga za escrow.
 
Back
Top Bottom