Shaka: Wakurugenzi acheni kuchukua 10% mnakwamisha miradi ya maendeleo, TAKUKURU fanyeni kazi yenu haraka

Mwananchi Huru

JF-Expert Member
Nov 20, 2021
1,448
1,003





==
SHAKA HAMDU SHAKA AWATAKA WATUMISHI KOTE NCHINI KUFIKA KWA WANANCHI KUSIKILIZA KERO NA CHANGAMOTO MBALIMBALI.

Na Mwandishi Wetu, Sikonge

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka amewataka watumishi wa umma waliopewa dhamana ya kuwatumikia wananchi kwenda kutatua changamoto walizonazo.

Shaka ametoa kauli hiyo leo Agosti 18,2022 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Sikonge alipokwenda kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo ambapo ametumia nafasi hiyo kuwahimiza watumishi kufika kwa wananchi.

“Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge ina kilometa za mraba 27,873 , ni Wilaya kubwa, hakikisheni mnasimamia maendeleo lakini muwe mnafuatilia huduma za kijamii mpaka huko vijijini, vitongojini.

“Baadhi ya maeneeo hamfiki , Mbunge amesema ujenzi wa mabarabara ambayo Rais Samia Suluhu Hassan amerahisisha usafiri na usafirishaji , niwaulize mnakwama wapi?

“Ukitoka hapa kwenda Kipili ni kilometa 400 lakini wananchi wanalalamika huduma za kijamii zimekuwa ni dhaifu ,wanapohitaji kutatuliwa matatizo yao mambo hayaendi vizuri, shida nini? Changamoto iko wapi?Alihoji Shaka.

Amewaomba watumishi na watendaji waliopewa mamlaka kwenye halmashauri kumsaidia Rais Samia kwa kuwafikia wananchi na kutatua kero zao na changamoto zao.

“Ndio jukumu tulopewa , tusipofanya hivyo itakuwa ni sehemu ya kwamishana na mambo hayataenda vizuri. Sisi kazi yetu ni kuongeza kasi na spidi ili wenzetu waliopewa dhamana serikalini wafanye vizuri zaidi,”amesema Shaka.

Aidha Shaka amezungumzia barabara inayounganisha Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora na Chunya mkoani Mbeya ambapo taarifa alizonazo tayari maandiko ya kuomba fedha yameandikwa, hivyo watakwenda kusukuma andiko hilo ili barabara ijengwe kwa kiwango cha lami.

Amesema barabara hiyo ni muhimu katika kukuza uchumi wa pande zote mbili kwani hata kiwanda cha nguo Mbeya kinategemea barabara hiyo na sasa kimefungwa.

“Moja ya kazi kubwa inayofanywa na wana Sikonge ni uzalishaji wa pamba kwa sasa hivi usafirisaji na hapa mlikuwa mnasafirisha kwa karibu zaidi ni kwenda Mbeya , taarifa nilizonazo kiwanda cha kuzalisha nguo cha mbeya kimegungwa.

“Sababu iliyosababisha kufungwa kiwanda kile ni kukosekana kwa barabara na taarifa nilizonazo andiko limeandikwa kutafuta fedha sehemu yoyote ili kuifungua barabara hi kusudi kuimarisha uchumi wa wana Sikonge lakini kuimarisha uchumi wa wana Tabora .Barabara hii inaunganisha mkoa wa Tabora na Mbeya Shinyanga itakuwa inasafirishwa kupitia barabara hii ya Ipole –Rungwa,”amesema Shaka.

Katika hatua nyingine amesema katika Kata ya Tumbi kumepita mradi wa reli ya mwendo kasi lakini changamoto kubwa iliyoko ni kutokamilika kwa tathimini ya ule mradi ili wananchi walipwe fidia .

“Kuna siku itabidi tuende huko TANESCO wanakwamisha ili fidia ya wananchi isiweze kukamilika.Niwaombe sana watu wa TANESCO hebu waharakishe ili jambo limalizike ili kusudi kasi ya mradi huu kama alivyodhamira Rais imalizike kwa wakati, “amesema Shaka.

Aidha,Shaka amewaonya wale wote wanaopokea 10% toka kwa wakandarasi jambo linalopelekea miradi mingi kukwama,huku akiwataka TAKUKURU wafanye kazi yao kote nchini,
 
Naomba kufahamishwa inakuaje katibu wa CCM anaenda kukagua hospitali? Na pia kuagiza hiki na kile kwa watumishi wa umma na wakioteuliwa

Je hata katibu wa vyama vingine wana hio mandate?
 
Hamna halmashauri ya hovyo Tanzania hii kama sikonge this council is so rubbish
 
Kumbe hao wakurugenzi wanajua michezo wanayoifanya nyuma ya pazia, ndio maana wanatafuta chawa waanze kuwapamba kwenye mitandao ya jamii ili kuficha wizi wao, siku hizi tunaletewa sifa za ajabu ajabu tu mkurugenzi anachapa kazi kisa amevalisha n'gombe hereni...
 
Aje Machinjio ya kibaha aone 10% zinavyopigwa
Watu waliamua kusitisha mani yasifike machinjio ili waidanganye serikali kuwa maji hayafiki hivyo wamtafute mzabuni atakayekuwa anapeleka maji kila siku .... mchongo wa wakubwa huo..
 
Wacha waseme Chama Cha Mapinduzi kina wenyewe
...........Tumeipenda wenyewe........wacha waisome namba eeeh, wasome nambaa...CCM mbele kwa mbele.....
"Msoga Jazz Band-walamba asali leo tupo Ukumbi wa asilimia kumi, karibu sana muburudike"
 
Sasa anamlaumu nani kwa kuchelewesha maji na miradi wakati ni hao hao ccm wako zaidi ya miaka 40 kwenye uongozi.

Hao hao wanaokula 10% ni shukrani maana wanatumika kuwaibia kura. Wana kadi nyota 5 za ccm
 
Back
Top Bottom