SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa itikadi na uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka akizungumza na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe walipokutana Kibondo mjini Leo tarehe 15 Mei 2021.
Shaka amesema inawezekana kufanya siasa safi bila kujenga uadui, uhasama, chuki au kubomoa misingi na tunu za Taifa letu. Amesisitiza anatamani kuona upinzani imara unaojenga umoja wa Taifa, unaohimiza amani na kuwa chachu ya mawazo mbadala yenye tija kwa nchi yetu. Ameshauri upinzani kuonesha ukomavu kwa kufanya siasa za maendeleo na kuepukana na siasa zinazojenga taharuki na kupinga kila kinachofanywa na serikali iliyopo madarakani.
Mwalimu Nyerere alituasa ili tuendelee tunahitaji SIASA SAFI.

#TaifaLetu #KaziIendelee #AminiaSamia