Rais Samia na siasa safi

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
Macho yangu yalipata muda mdogo wa kutazama sehemu ndogo ya mahojiano ya kipindi cha Dakika 45 kinachoruka kupitia kituo cha habari cha ITV ambapo mgeni wa siku hiyo alikuwa Mhe. Tundu Antiphas Lissu.

Nilimsikia Lissu akikiri juu ya mwenendo wa siasa na hali ya usalama hapa nchini kuwa ni shwari lakini pia alieleza namna ambavyo rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan alivyopokea malalamiko yake kuhusu madai ya stahiki zake wakati akiwa mbuge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Kwa haraka ukiona sura ya mwanasiasa wa upinzani maswali yatajijenga akilini kwamba kitu anachokizungumza kitakuwa ni cha kukinzana na serikali lakini sasa nilimuona Lissu akiongea kwa ahueni kusifu namna Rais Samia Suluhu Hassan alivyo yapokea malalamiko yake na kuanza kuyashughulikia.

Makala hii nimeamua kuiita RAIS SAMIA NA SIASA SAFI kwa sababu kuu ya msingi moja ambayo ni mwenendo wa hali ya kisiasa nchini.

Kwenye suala la uponyaji wa taifa lolote lile katika nyanja mbalimbali lazima kuwe na kipengele cha maridhiano.Hii ni hatua ambayo imebeba ubinadamu ndani yake,taifa lolote kukiwa na uhasama au tofauti za kiitikadi na hakuna maridhiano basi wanaoumia ni wananchi.

Katika hali ya kuonyesha siasa safi serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan imekubali kukaa meza moja na upande wa upinzani na kuona sasa ni wakati wa kufanya siasa za majukwaani na vyama vya siasa vifanye hivyo pasipo kuvunja sheria nyingine za nchi.

Suala hili linaweza kuonekana dogo lakini ndani yake limebeba uthubutu mkubwa kwani mikutano ya hadhara ni moja ya sehemu ambayo viongozi wa kisiasa hupeana changamoto nyingi.

Pasipo vurugu,pasipo makelele tumeiona nchi sasa ikifanya mikutano ya hadhara,hili ni suala la kuipongeza serikali pia na vyombo vyote vya ulinzi nchini.

Sasa hakuna kiongozi anayelalamika kwamba ananyimwa uhuru,kila chama kina haki ya kufanya mkutano wa hadhara.

Mama Samia Suluhu Hassan toka aingie madarakani kama rais tumemuona akitembelea nchi mbalimbali ambapo ni moja ya sehemu ya kujifunza zaidi na kukuza upeo katika uendeshaji wa nchi kwa kuiga mfano wa mataifa yaliyoendelea.

Rais Samia amekutana na viongozi wa kitafaita wa nchi mbalimbali za Afrika na ulimwengu kwa ujumla ndani ya muda mfupi aliokaa madarakani,si hayo tu pia tumeona mataifa mbalimbali ulimwenguni yanaunga mkono jitihada za maendeleo kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwaajili ya miradi ya maendeleo.

Natamani kuendelea kuzungumzia mengi yaliyofanywa na rais lakini kalamu yangu inaniambia niwe na kikomo ili niweze kusema wakati mwingine.


Nitakoses nisipo malizia hili, Rais Samia katika kipindi kifupi ameshirikiana na kukaa na viongozi wa vyama vya upinzani katika kushirikishana mambo mbalimbali yanayohusu umoja na maendeleo ya taifa.

HAKIKA KWA HAYO TUTAIONA SIASA SAFI CHINI YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN NA HII NDIYO NJIA SAHIHI YA MAENDELEO YA TAIFA.

Naiweka Kalamu Chini Mpaka Wakati Mwingine.
 
Haya kumuamini mwanasiasa wa kiafrika, ni sawa na kujifanya eti umemng'oa meno.Black mamba
 
Back
Top Bottom