SHAKA: Igunga ni shamba darasa kwa miradi ya maendeleo

Mpekuzi Tanzania

JF-Expert Member
Mar 11, 2018
585
906
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka H. Shaka (MNEC) ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwa usimamizi mzuri wa Fedha za Miradi ya Maendeleo na kuiita ni "Shamba Darasa la Miradi ya Maendeleo".

Ndg. Shaka (MNEC) ameyasema hayo akiwa kwenye Kituo cha Afya cha Nanga kilichopo Jimbo la Igunga kwenye ziara ya kikazi aliyoifanya Wilaya ya Igunga kwa ajili ya kufuatilia utekekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM);

"... Mhe. Mkuu wa Mkoa nimeona miradi inayofanyika kwenye majimbo yote mawili ya Wilaya ya Igunga (Jimbo la Igunga na Jimbo la Manonga), kiukweli Halmashauri ya Igunga imenikosha na wameweza kusimamia vizuri Fedha za Miradi zilizotolewa na Mhe.

Samia Suluhu Hassan, Nakuomba ukawafikishie salam Halmashauri zingine za Mkoa wa Tabora wafike Igunga kujifunza kwenye swala la thamani ya Fedha kwenye miradi (value for money).

Wabunge wa Majimbo ya Igunga (Mhe. Ngassa na Mhe. Gulamali) niwahaidi nitarudi tufanye Ziara Kata kwa Kata maana nimeona kazi zenu ni nzuri na kama Chama lazima tuwaunge mkono katika kutatua kero za Wananchi kama ambavyo Rais wetu anataka. Ndio maana analeta Fedha nyingi huku chini zinufaishe Wananchi wote..."

Aidha Ndg. Shaka (MNEC) ametembelea mnada wa mifugo wa Igunga na kupokea kero ya uchakavu wa jengo la biashara iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe.

Nicholaus George Ngassa na kuahidi kulifikisha kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya utatuzi.
 

Attachments

  • IMG-20220821-WA0265.jpg
    IMG-20220821-WA0265.jpg
    49.4 KB · Views: 7
  • IMG-20220821-WA0258.jpg
    IMG-20220821-WA0258.jpg
    48.7 KB · Views: 7
  • IMG-20220821-WA0252.jpg
    IMG-20220821-WA0252.jpg
    50.6 KB · Views: 6
  • IMG-20220820-WA0738.jpg
    IMG-20220820-WA0738.jpg
    81.8 KB · Views: 7
  • IMG-20220820-WA0760.jpg
    IMG-20220820-WA0760.jpg
    97.7 KB · Views: 8

Similar Discussions

Back
Top Bottom