Shaka Hamdu Shaka msumari wa moto kwa Upinzani Tanzania

Kwa maoni yangu ni kuwa CCM haiwezi kujiongeza upendo kwa wananchi hata kifanye mazuri mengi kiasi gani. Hata kilipe jobless mishahara lakini bado upendo kwao utaendelea kupungua.

Na sababu kubwa ni kwamba watu wameichoka tu, wengine hata hawana sababu za msingi zaidi ya kukichoka tu.

Njia pekee ya kurudisha upendo ni kustep down. kikae pembeni, kwani hii njia itawapunguza wengi wale wa ccm chumia tumbo, na kubakia na ccm-imani, ccm itikadi.

Chama kitakachotawala kwa umasikini wetu huu kitafanya fyongo tu, na hivyo kitalalamikiwa pia kama ccm. - Huu utakuwa wakati muafaka kwa ccm kujisafisha na kutengeneza upendo kwa wananchi. - Baada ya hapo uchaguzi utakaofuata (ulio fair) ccm inaingia madarakani bila makando yoyote.

Angalizo: jaribio hili lifanywe tu baada ya kuwa kimeweka misingi imara ya utawala bora nchini.
 
Kwa maoni yangu ni kuwa ccm haiwezi kujiongeza upendo kwa wananchi hata kifanye mazuri mengi kiasi gani. Hata kilipe jobless mishahara lakini bado upendo kwao utaendelea kupungua...
Wakina nani wamechoka?

Nilini walikufanya kuwa msemaji wao?
 
Sijawahi ona kiongozi mnyenyekevu kama Shaka, Kama mnamfahamu nitajieni
 
Msingi wake ukiwa ni aina ya Siasa anazozifanya kijana huyu Mzalendo wa kweli wa Taifa hili zimekizolea umaarufu na heshima kubwa ndani na nje ya nje Chama cha Mapinduzi kwa kipindi hiki kifupi tangu kuteuliwa kwake...
Hana lolote huyu dogo!

Anatakiwa amsaidie Mama Samia ili sera za uchumi ziwe dhahiri ndani ya chama.

Awe na lugha ya kuelezea msimamo wa chama juu ya uchumi, kitu ambacho hajakifanyia uenezi.

Siyo siri, upeo wake bado mchanga mno.
 
Ni kijana gani anaweza kujiunga na ccm kwa hiari? Vijana wamepigika mtaani hawana hamu kabisa na ccm labda kipindi Cha jk ambacho ajira zilikuwa bwerere Kila Kona. Sasa hivi mwenye masters anaendesha bodabida au Ni shoeshiner halafu aipende ccm? Kwa lipo!!
 
Tanzania inawatu wasiopenda kuwatia moyo Wale wanaofanya kazi kwa bidii,

Tanzania tunaishi kwa gubu katika kila jambo
 
MLETA MADA HUJITAMBUI, Siasa zinafanywa na CCM tu huku vyama vya upinzani hata vikifanya jogging, Polisi hawa hapa. Leo unaongea utumbo. WEKENI mizani sawa ya siasa tuone huo Msumari wa Moto inayozungumziwa.
Soma polepole kwa kuelewa mkuu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…