Shairi: Nampenda Kuku Wangu

Shairi: Nampenda Kuku Wangu

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
Ni sehemu ya mfululizo wa mashairi ya IDD NINGA, fuatilia shairi hili na toa maoni yako.

JINA LA SHAIRI: Nampenda Kuku Wangu.
MTUNZI:Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
Simu: 0755519736


Kuku ndie jina lake, mtetea ni matani.
Kuku anamwenzi wake, waishi nae bandani.
Jogoo na ndugu zake, wanavilemba kichwani.
Nampenda kuku wangu, ndo mana yupo bandani.


Kokoriko wimbo wake, auimbao mjini.
Ni nzuri sauti yake, hata kule kijijini.
Lapendeza vazi lake, la manyoya ya shingoni.
Nampenda kuku wangu, ndo mana yupo bandani.


Ni salama lake teke, mwanae yu salimini.
Hata ampige teke, amuui asilani.
Hawezi mwacha mpweke, akachunge jalalani.
Nampenda kuku wangu, ndo mana yupo bandani.


Kuku hana baba ake, si yatima duniani.
Anampenda mamake, kamwe hawi na huzuni.
Ni laini nyama yake, ukiipika jikoni.
Nampenda kuku wangu, ndo mana yupo bandani.


Ni litamu yai lake, uliwekapo mezani.
Ni nzuri harufu yake,i kiwepo kisosini.
Ila ngumu kucha zake, akikuchoma machoni.
Nampenda kuku wangu, ndo mana yupo bandani.


 
Mmmmh shairi tam

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom