Nampenda kuku wangu

Nampenda kuku wangu

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
1.Kuku Ndie jina lake,mtetea ni matani.
Kuku anamwenzi wake,waishi nae bandani.
Jogoo na ndugu zake,wanavilemba kichwani.
Nampenda kuku wangu,ndo mana yupo bandani.

2.Kokoriko Wimbo wake,auimbao mjini.
Ni nzuri sauti yake,hata kule kijijini.
Lapendeza vazi lake,la manyoya ya shingoni.
Nampenda kuku wangu,ndo mana yupo bandani.

3.Ni Salama lake teke,mwanae yu salimini.
Hata ampige teke,amuui asilani.
Hawezi mwacha mpweke,akachunge jalalani.
Nampenda kuku wangu,ndo mana yupo bandani.

4.Kuku Hana baba ake,si yatima duniani.
Anampenda mamake,kamwe hawi na huzuni.
Ni laini nyama yake,ukiipika jikoni.
Nampenda kuku wangu,ndo mana yupo bandani.

5.Ni Litamu yai lake,uliwekapo mezani.
Ni nzuri harufu yake,ikiwepo kisosini.
Ila ngumu kucha zake,akikuchoma machoni.
Nampenda kuku wangu,ndo mana yupo bandani.

Jina la shairi= nampenda kuku wangu.
Mtunzi= idd ninga wa tengeru arusha.
Simu= 0755519736


 
YAI LASHINDA UTAMU KUKUYO HAONI NDANI:

1.Bure wamsifu kuku kwa kuila nyama yake,hebu jaribu na yai ujue utamu wake,hakika utafurahi kuionja tamu yake,yai lashinda utamu kukuyo haoni ndani.

2.Ninga kula kiini ujue utamu wa yai,kuku bure wajihini wala huyo hakufai,yai ni kitu laini mwenyewe utafurahi,yai lashinda utamu kukuyo haoni ndani.

3.Kuna viini vya njano tena vile vya asili,vyeupe vilivyonona na kujazia misuli,chemsha au kaanga uvipate kwa uzuri,yai lashinda utamu kukuyo haoni ndani,
 
KUKU HUYO KUKU GANI?

1.Unamsifia kuku huyo ndede wa manyoya, ana kipi cha ziada chambua kimoya kimoya,kuku huyo kuku Ninga alokuchanganya?

2.Kuku wamfuga leo kesho hakai bandani,wamfanya kitoweo kwisha hana thamani,wamnywa supu leo kesho waenda chooni,kuku huyo kuku gani Ninga alaokuchanganya?

3.Tena unaeza kuta kuku wako kuku boy,hawezi kufurukuta roundi moja yeye hoi,huku kule ajivuta na safari hatoboi,kuku huyo kuku gani Ninga alokuchanganya?
 
Back
Top Bottom