Shairi: Arusha jiji letu

JOTO LA MOTO

JF-Expert Member
Apr 11, 2018
758
555
KUTOKA KWA:MSANII JOTO LA MOTO.

Arusha ni jiji letu,jiji lenye kusifika.
Jiji lenye wema watu,karibu uweze fika.
Hatufugi wale chatu, mbugani twakupeleka.
Arusha ni jiji letu, njoo mfurahi nasi.

Roho zetu wote safi,watu wema twapendeza.
Watu huku si walafi, cha mtu kukipoteza.
Mji wetu ni msafi,mazingira tunatunza.
Arusha ni jiji letu, njoo mfurahi nasi.

Ukifika jiji hili,mapokezi utapenda.
Kikazi na kitalii,sisi wote twawapenda.
Utakula vya asili,nyama ndizi za kuponda.
Arusha ni jiji letu, njoo mfurahi nasi.

Sifa zote zipo huku,wewe njoo utaona.
Masai ni kwao huku,na wengine wapo mbona.
Nyama ng’ombe mbuzi kuku,utakula vilonona.
Arusha ni jiji letu,njoo mfurahi nasi.

Hakuna damu kulaza,watu huku twajituma.
Muda mwiko kupoteza,tusijepata lawama.
hakuna vyuma kukaza,tunalala wima wima.
Arusha ni jiji letu, njoo mfurahi nasi.

Ajae akaribishwa,aone vitu adimu.
Ngorongoro utavushwa,Momela utie timu.
Mlima utaonyeshwa,na mengi ya ukarimu.
Arusha ni jiji letu, njoo mfurahi nasi.



 
Nasikia mmepandisha bei za hotel zote za Kaloleni hata kuzidi za mitaa kama hiyo za Nairobi na Dar es salaam
 
Tukitengwa twajipenda, pamoja twasimama.
Tabasam likitanda, tazama utasema.
Sababu tutakwenda, ni wote si kichama. Arusha jiji letu, .....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom