Shahidi: Lema alimkashifu Dk. Buriani jukwaani

Shahidi: Lema alimkashifu Dk. Buriani jukwaani

Acha ujinga wewe! Mbona kova anatahadharisha uwepo wa al-shabaab,je we ndio al-shabaab? Au sisi wa-tz leo tumegeuka al-shabaab? Lema ametoa tahadhari tu,unakumbuka NBC ubungo yule jambazi wa kike aliyevaa vazi la kininja(silijui jina lake upendwa na wapemba na waarabu),mbona Ufaransa wamezuia uvaaji wa mavazi hayo? Ni tahadhari tu lema ametoa na si ubaguzi.
 
kama aliwaambia hivyo na kweli wakamchagua basi hapo kuna tatizo! Halafu kitu kingine mbona hiyo kauli sikuwahi kuisikia kabla!?
 
Maneno haya alitamka Mussa Ikangaa na sio Lema. Kuanza kutoa hukumu badala ya hakimu ndio matatizo ya elimu tunayopewa na ccm kudandia treni kwa mbele ama kutumia masaburi kufikiria

na huyo Musa Ikanga ni nani na ana mahusiano gani na Lema wakati wa kampeni au baada ya kampeni
 
Chadema bana .. kwa kauli za viongozi wenu kama hizi ... mkiambiwa ni chama cha kanisa ... mnasema propaganda ... inaelekea mkiingia madarakani mtatuletea mambo ya ufaransa kuwazuia dada zetu kuvaa stara..

ndio tatizo lako hilo njiwa! Inamaana ulikuwepo wakati anasema au ulimsikia!? Au wewe ndio kati ya wale watu sheikh anakuja na utafiti wake wa kisayansi kwa nini shule na wanafunzi wa kiislamu wamefeli yeye anasema tatizo ni Katibu wa baraza na mnampigia makofi!
 
JF ni mahala ambapo habaguliwi mtu

hili ni jukwaa la siasa na hayo maneno amesema mwanasiasa ambaye kapewa dhamana kubwa sana na wananchi

sasa kwa nini hamtaji yajadiliwe? kwa nini mnawapiga presha akina invisible wahamishe thread?

mnaogopa nini?
Wewe kweli ni chuki na inaonyesha una chuki sana na Lema, hapa hakuna anayemwogopa mwenzie ila sema hakuna cha maana kinachofaa kujadiliwa!
 
Huyu ni mwanasiasa ambaye anadhamana ya kuwawasikilisha wananchi bila kuwabagua.




Mmojawapo wa wabunge ambao wanamalizia mda wao na hawatakanyaga tena bungeni ni huyu ganja man; lakini usishangae huu ukiwa ni mtazamo wa chama chake
 
JF ni mahala ambapo habaguliwi mtu

hili ni jukwaa la siasa na hayo maneno amesema mwanasiasa ambaye kapewa dhamana kubwa sana na wananchi

sasa kwa nini hamtaji yajadiliwe? kwa nini mnawapiga presha akina invisible wahamishe thread?

mnaogopa nini?

Naomba kwa ridhaa yako nikuite MJINGA, na ujinga wako upo hapo kwenye bold.

Kesi inaendelea mahakamani, wewe una-quote maneno ya shahidi na kuyaleta hapa kama mada. No one is guilty until proven so. Have you proved that he said so? Kwa nini tukae kudiscuss issues ambazo I can say "hazina ushahidi"?

I repeat my plea once again, hili jukwaa la siasa linahitaji kuwa na Entry Exam, tupunguze rubbish hapa.
 
Tusubiri mahakama itoe hukumu ndio tumjadili.

You dont need a PHD to see this, let's wait then discuss.

Juzi tu hapa kulikuwa na kesi Malaysia ya mpinzani mkuu wa serikali Anwar Ibrahim. Na kesi yake ilikuwa mbaya sana (sodomy), lakini mahakama iliamua kuwa hana hatia, ingekuwa TZ si mngedai kichwa chake! kwa nini tuanze ku-judge kesi ya Lema kwa maneno ya mashahidi?
 
Na sasa Al-Qaeeda wameshaungana na Al-Shabaab na kauli mbiu yao inasema: "Ugomvi kwetu sherehe!". Sijui itakuaje kwa wale watu wenye Ugonjwa mbaya sana unaojuilikana kama; Islamaphobia! Au ndio huyu Mh. Lema anaanza kuweweseka hata mambo hayajapamba moto!!!
 
ndio ni magaidi na wamachama wa Mungiki na AL shabab...
 
Na sasa Al-Qaeeda wameshaungana na Al-Shabaab na kauli mbiu yao inasema: "Ugomvi kwetu sherehe!". Sijui itakuaje kwa wale watu wenye Ugonjwa mbaya sana unaojuilikana kama; Islamaphobia! Au ndio huyu Mh. Lema anaanza kuweweseka hata mambo hayajapamba moto!!!
lini mambo yatapamba moto? naona sifa ya kujilipua imewalewesha wengi...ukweli ni kwamba hakuna mtu anayemuogopa 'nyau' yeyote.
 
Chadema bana .. kwa kauli za viongozi wenu kama hizi ... mkiambiwa ni chama cha kanisa ... mnasema propaganda ... inaelekea mkiingia madarakani mtatuletea mambo ya ufaransa kuwazuia dada zetu kuvaa stara..

Ukweli ndiyo huo lakini jamaa wakiambiwa wanakuwa wabishi. Hawajui hata kuheshimu uhuru wa mtu wa kuabudu.
 
lini mambo yatapamba moto? naona sifa ya kujilipua imewalewesha wengi...ukweli ni kwamba hakuna mtu anayemuogopa 'nyau' yeyote.

Si muda mrefu mambo yataiva na tutawataarifu rasmi hapa mjengoni, lakini kwanza tunafanya kazi ya kutambulishana! Lakini fahamu hadi Askari wa kimarekani na ambao wameshawahi kushiriki vita kule Iraq, Afaghanistan na kwengineko sasa wanasilimu na kujiunga na haya makundi; jee wewe bado kwanza!
 
Hiyo ni kauli ya LEMA wa CHADEMA.... CCM hapa inauhusiano gani?

Hiyo si kauli ya Lema wa Chadema, Labda Lema wa ccm.

Hayo ni madai ya Musa Mkangaa kada wa ccm anayetafuta kufuta madhambi yake ya ufisadi aliopata kufanya akiwa diwani. Na hapo ndipo ccm inapohusika!!
 
Chadema bana .. kwa kauli za viongozi wenu kama hizi ... mkiambiwa ni chama cha kanisa ... mnasema propaganda ... inaelekea mkiingia madarakani mtatuletea mambo ya ufaransa kuwazuia dada zetu kuvaa stara..
Endeleeni tuu lakini hatuwashangai ni Kaka yenu Jakaya Kikwete alivyoona maji ya uchaguzi yako mushingo akaanzisha vita ya udini,haya maneno aliyosema kuna watu wana uroho wa madaraka wanatumia makanisa ili yafike IKULU yemerudi kabla hajatoka madarakani,na sijui atawezaje kujisafisha udini wake amewaambukiza watu wengi
Kumbuka hakuna mtu atakuwa salama vita vya kidini vikianza tumeona kila mahala penye vita za kidini wote huwa waathirika endekezeni ujinga huo
 
Huyu ni mwanasiasa ambaye anadhamana ya kuwawasikilisha wananchi bila kuwabagua.







Source: Mwananchi la leo
Habari nzima hii hapa chini ili tuweze kuchambua vizuri pumba na mchele
Shahidi: Lema alimkashifu Dk Burian jukwaani
Tuesday, 14 February 2012 10:48
Peter Saramba, Arusha

MDAI wa pili katika shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Arusha mjini, jana aliieleza mahakama kuwa alimsikia mdaiwa kwa kwanza katika kesi hiyo, Godbless Lema (Chadema), ikiwataka wapiga kura kutomchagua aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Batilda Burian kwa kuwa ameolewa Zanzibar na ana ujauzito wa mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.
Akiongozwa na wakili wake, Alute Mughwai, mdai huyo, Agnes Mollel (44) alidai kumsikia Lema akitamka maneno hayo katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita uliofanyika eneo la Big Sister, Mtaa wa Roman Catholic, Kata ya Olorien, Manispaa ya Arusha.
Aliieleza mahakama mbele ya Jaji Gabriel Rwakibarila kuwa mkutano huo ulifanyika eneo hilo ambako yeye ni Mwenyekiti wa mtaa Septemba Mosi, mwaka juzi.
Agnes alikuwa akitoa ushahidi wake, akiwa shahidi wa pili baada ya mdai wa kwanza, Mussa Mkanga kumaliza ushahidi wake, ambapo alidai kumwona kwa macho yake na kumsikia kwa masikio Lema akihutubia jukwaani na kuwaeleza wananchi waliohudhuria mkutano huo kwamba Dk Batilda hastahili kuchaguliwa kwa sababu ni mwanamke.
“Msimchague huyo mwanamke Dk batilda kwa sababu ameolewa na Mzanzibari na hapo alipo ana mimba ya Lowassa. Hivyo mkimchagua jimbo hili mtakuwa mmeliuza kwa Lowassa na amesema akichaguliwa atakifunga kituo cha Radio cha Safina,” alisema Agnes akidai kumkariri Lema.
Shahidi huyo alidai maneno hayo yalimkera na kumfanya aondoke kwenye mkutano huo kabla Lema hajamaliza hotuba yake na siku iliyofuata alitoa taarifa kwa Dk Burian kuhusu tuhuma na kashfa zilizotolewa dhidi yake na mgombea huyo wa upinzani.
Hata hivyo shahidi huyo alikiri kuwa madai ya Lema kutamka kuwa Dk Burian alizaa na mwanamume mwingine hayako katika hati ya madai waliyowasilisha mahakamani na wala jina la muhusika halikutajwa kwa kile alichodai inawezekana ilisababishwa na makosa ya kiuchapaji.
Aliiomba mahakama kutengua matokeo na kumvua ubunge Lema iwapo itaridhika na ushahidi wao pamoja kuamuru wadai kulipwa gharama za shauri hilo namba 13/2010 ambayo awali ilikuwa ikisilikizwa na Jaji Aloyce Mujulizi aliyejitoa baada ya mdai wa kwanza kukosa imani naye.
Akihojiwa na wakili wa Lema, Method Kimomogoro, shahidi huyo alikana maelezo yaliyo kwenye hati yao ya madai kuwa yeye alimsikia mbunge huyo akitoa kauli za kashfa na udhalilishaji dhidi ya Dk Burian katika mkutano wa hadhara uliofanyika Saa 10:00 jioni ya Septemba 22, 2010 eneo la Fantastic, Olmatejoo, Kata ya Elerai.
Hata baada ya kuonyeshwa maelezo yaliyo katika hati hiyo ya madai aliyotia saini yeye pamoja na wenzake Mkanga na Happy Kivuyo, shahidi huyo alisisitiza kutotambua maelezo hayo na kudai kauli yake mbele ya mahakama ndiyo sahihi kwamba mkutano aliohudhuria ni ule uliofanyika Big Sister na siyo vinginevyo.
“Mimi maneno niliyosikia na kumshuhudia Lema akitamka ni yale ya Big Sister, siyo Olmatejoo. Kwanza mie sipafahamu hata huku Fantastic na niliweza kuyakariri kauli hizo bila kuzinasa kwa kinasa sauti wala kuziandika sehemu yoyote,” alisisitiza Agnes.
Katika hatua nyingine, shahidi huyo alidai kutosoma wala kusomewa maelezo ya Dk Burian katika barua yake ya malalamiko kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Arusha akilalamikia kauli za Lema dhidi yake.
Hali hiyo ilimfanya wakili Kimomogoro kumhoji iwapo alilazimishwa kufungua shauri hilo mahakamani bila ridhaa yake ndio maana hajui undani wa viambatanisho vilivyo kwenye hati yao ya madai, lakini alipinga kwa maelezo kuwa aliungana na wenzake kufungua kesi hiyo baada ya kuchukizwa na kauli za udhalilishaji na ubaguzi kijinsia, kidini na kikabila zilizotolewa na Lema dhidi ya Dk Burian.
Katika madai yao, walalamikaji hao wanadai kuwa katika mikutano yake kadhaa ya kampeni, Lema alisikika akiwaasa wapiga kura kutomchagua Dk Burian kwa sababu atarejea Zanzibar kwa mumewe baada ya uchaguzi na kuhoji iwapo mila na desturi za makabila ya Waarusha (Wamasai) na Wachaga mwanamke anaweza kuongoza wazee wa mila.
Kupitia kwa wakili Mughwai anayesaidiana na Modest Akida, walalamikaji hao pia wanadai Lema aliwatahadharisha wapiga kuwa kuwa makini na wanaovaa ushungi, vitambaa na hijabu wasije kujikuta wamechagua Al-Qaida huku pia akimtuhumu Dk Burian kuwa mwanamke asiye mwaminifu aliyezaa na kupata mimba nje ya ndoa.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ni mdaiwa wa pili katika shauri hilo anawakilishwa na mawakili wa Serikali, Timoth Vitalis na Juma Masanja
 
Back
Top Bottom