Shahidi: Lema alimkashifu Dk. Buriani jukwaani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shahidi: Lema alimkashifu Dk. Buriani jukwaani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Feb 14, 2012.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Huyu ni mwanasiasa ambaye anadhamana ya kuwawasikilisha wananchi bila kuwabagua.

  MDAI wa pili katika shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Arusha mjini, jana aliieleza mahakama kuwa alimsikia mdaiwa kwa kwanza katika kesi hiyo, Godbless Lema (Chadema), ikiwataka wapiga kura kutomchagua aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Batilda Burian kwa kuwa ameolewa Zanzibar na ana ujauzito wa mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.

  Akiongozwa na wakili wake, Alute Mughwai, mdai huyo, Agnes Mollel (44) alidai kumsikia Lema akitamka maneno hayo katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita uliofanyika eneo la Big Sister, Mtaa wa Roman Catholic, Kata ya Olorien, Manispaa ya Arusha.

  Aliieleza mahakama mbele ya Jaji Gabriel Rwakibarila kuwa mkutano huo ulifanyika eneo hilo ambako yeye ni Mwenyekiti wa mtaa Septemba Mosi, mwaka juzi.

  Agnes alikuwa akitoa ushahidi wake, akiwa shahidi wa pili baada ya mdai wa kwanza, Mussa Mkanga kumaliza ushahidi wake, ambapo alidai kumwona kwa macho yake na kumsikia kwa masikio Lema akihutubia jukwaani na kuwaeleza wananchi waliohudhuria mkutano huo kwamba Dk Batilda hastahili kuchaguliwa kwa sababu ni mwanamke.

  "Msimchague huyo mwanamke Dk Batilda kwa sababu ameolewa na Mzanzibari na hapo alipo ana mimba ya Lowassa. Hivyo mkimchagua jimbo hili mtakuwa mmeliuza kwa Lowassa na amesema akichaguliwa atakifunga kituo cha Radio cha Safina," alisema Agnes akidai kumkariri Lema.

  Shahidi huyo alidai maneno hayo yalimkera na kumfanya aondoke kwenye mkutano huo kabla Lema hajamaliza hotuba yake na siku iliyofuata alitoa taarifa kwa Dk Burian kuhusu tuhuma na kashfa zilizotolewa dhidi yake na mgombea huyo wa upinzani.

  Hata hivyo shahidi huyo alikiri kuwa madai ya Lema kutamka kuwa Dk Burian alizaa na mwanamume mwingine hayako katika hati ya madai waliyowasilisha mahakamani na wala jina la muhusika halikutajwa kwa kile alichodai inawezekana ilisababishwa na makosa ya kiuchapaji.

  Aliiomba mahakama kutengua matokeo na kumvua ubunge Lema iwapo itaridhika na ushahidi wao pamoja kuamuru wadai kulipwa gharama za shauri hilo namba 13/2010 ambayo awali ilikuwa ikisilikizwa na Jaji Aloyce Mujulizi aliyejitoa baada ya mdai wa kwanza kukosa imani naye.

  Akihojiwa na wakili wa Lema, Method Kimomogoro, shahidi huyo alikana maelezo yaliyo kwenye hati yao ya madai kuwa yeye alimsikia mbunge huyo akitoa kauli za kashfa na udhalilishaji dhidi ya Dk Burian katika mkutano wa hadhara uliofanyika Saa 10:00 jioni ya Septemba 22, 2010 eneo la Fantastic, Olmatejoo, Kata ya Elerai.

  Hata baada ya kuonyeshwa maelezo yaliyo katika hati hiyo ya madai aliyotia saini yeye pamoja na wenzake Mkanga na Happy Kivuyo, shahidi huyo alisisitiza kutotambua maelezo hayo na kudai kauli yake mbele ya mahakama ndiyo sahihi kwamba mkutano aliohudhuria ni ule uliofanyika Big Sister na siyo vinginevyo.

  "Mimi maneno niliyosikia na kumshuhudia Lema akitamka ni yale ya Big Sister, siyo Olmatejoo. Kwanza mie sipafahamu hata huku Fantastic na niliweza kuyakariri kauli hizo bila kuzinasa kwa kinasa sauti wala kuziandika sehemu yoyote," alisisitiza Agnes.

  Katika hatua nyingine, shahidi huyo alidai kutosoma wala kusomewa maelezo ya Dk Burian katika barua yake ya malalamiko kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Arusha akilalamikia kauli za Lema dhidi yake.

  Hali hiyo ilimfanya wakili Kimomogoro kumhoji iwapo alilazimishwa kufungua shauri hilo mahakamani bila ridhaa yake ndio maana hajui undani wa viambatanisho vilivyo kwenye hati yao ya madai, lakini alipinga kwa maelezo kuwa aliungana na wenzake kufungua kesi hiyo baada ya kuchukizwa na kauli za udhalilishaji na ubaguzi kijinsia, kidini na kikabila zilizotolewa na Lema dhidi ya Dk Burian.

  Katika madai yao, walalamikaji hao wanadai kuwa katika mikutano yake kadhaa ya kampeni, Lema alisikika akiwaasa wapiga kura kutomchagua Dk Burian kwa sababu atarejea Zanzibar kwa mumewe baada ya uchaguzi na kuhoji iwapo mila na desturi za makabila ya Waarusha (Wamasai) na Wachaga mwanamke anaweza kuongoza wazee wa mila.

  Kupitia kwa wakili Mughwai anayesaidiana na Modest Akida, walalamikaji hao pia wanadai Lema aliwatahadharisha wapiga kuwa kuwa makini na wanaovaa ushungi, vitambaa na hijabu wasije kujikuta wamechagua Al-Qaida huku pia akimtuhumu Dk Burian kuwa mwanamke asiye mwaminifu aliyezaa na kupata mimba nje ya ndoa.

  Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ni mdaiwa wa pili katika shauri hilo anawakilishwa na mawakili wa Serikali, Timoth Vitalis na Juma Masanja


  Source: Mwananchi la leo
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  duh...ccm mwishowe watakuja kujichokonoa bila kujijua
   
 3. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ukisikia siasa uchwara ndo hizi sasa zilizomkimbiza rostam ccm
   
 4. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  CCM na mchezo wenu huu wa kupandikiza mbegu za chuki za kidini, siku kikiwaka tutagawana macho na roho zenu.

  Ninyi endeleeni kucheza mchezo mkifikiri tunafurahia.
   
 5. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ni kweli anapigania haki lakini kwa hili aliteleza
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wewe ni kipofu
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  sasa mnakataa nini?
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni kauli ya LEMA wa CHADEMA.... CCM hapa inauhusiano gani?
   
 9. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Msilete chuki,kama mnamtaka lema si mumfuate? Mnamlisha maneno ili iweje.aliesema ivo ni musa mkanga
   
 10. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Sijui kama yuko sawa.... alishawahi kukesha akifanya ibada ya ufufuo kwa marehemu mke wa Mwenyekiti wa CCM Arusha akaishia patupu... hawa ndiyo CHADEMA wanaotaka kuongoza nchi na sera za ubaguzi wa kidini...
   
 11. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #11
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0

  Mods please hebu ondoa hii kitu, kwa nini mnawaacha watu kama hawa wanaotukana humu? Piga burn huyu tafadhali
   
 12. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Maneno haya alitamka Mussa Ikangaa na sio Lema. Kuanza kutoa hukumu badala ya hakimu ndio matatizo ya elimu tunayopewa na ccm kudandia treni kwa mbele ama kutumia masaburi kufikiria
   
 13. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #13
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Amesema wawe makini.
  Amesema 'wanaweza kujikuta', hakuna mahali amesema 'NI ALKAEDA'..


  Afu amesema kweli au ndio siasa za maji machafu???
   
 14. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Chadema bana .. kwa kauli za viongozi wenu kama hizi ... mkiambiwa ni chama cha kanisa ... mnasema propaganda ... inaelekea mkiingia madarakani mtatuletea mambo ya ufaransa kuwazuia dada zetu kuvaa stara..
   
 15. lidoda

  lidoda JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2012
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 632
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 80
  CCM CCM CCM CCM CCM CCM CCM CCM CCM kuna in hapooo
   
 16. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sante mkuu!
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Feb 14, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kama aliteleza basi mkono wa sheria utakuwa juu yake! ni maneno ya kupandikiza chuki za udini haya... sheria ichukue mkondo wake bana.
   
 18. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #18
  Feb 14, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ni kweli Lema amesema?
   
 19. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #19
  Feb 14, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  JF ni mahala ambapo habaguliwi mtu

  hili ni jukwaa la siasa na hayo maneno amesema mwanasiasa ambaye kapewa dhamana kubwa sana na wananchi

  sasa kwa nini hamtaji yajadiliwe? kwa nini mnawapiga presha akina invisible wahamishe thread?

  mnaogopa nini?
   
 20. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #20
  Feb 14, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  ushahidi kuwa alisema?
   
Loading...