Shahidi aingia na bastola mahakamani kesi ya bilionea Msuya, jaji alazimika kuahirisha kesi

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Bilionea.jpg

Moshi. Mahakama Kuu imesimama kwa muda kesi ya mauaji ya bilionea Erasto Msuya baada ya shahidi wa 16, PF 1878 Willium Mziu, ambaye ni mkaguzi wa polisi upelelezi makao makuu kuingia na bastola mahakamani hali ambayo ilileta hofu kwa mawakili upande wa utetezi.

Hali hiyo iliyotokea leo Alhamisi imesababisha wakili upande wa utetezi, Hudson Ndusyepo kuiambia mahakama hiyo kuwa hawawezi kuendelea kusikiliza kesi hiyo kutokana na shahidi huyo kuonekana na silaha na kumwambia Jaji Salma Maghimbi kuwa hawapo salama.

Kwa upande wake wakili upande wa mashtaka, Abdallah Chavula ameiambia mahakama hiyo kuwa shahidi huyo anaruhusiwa kuingia na silaha mahakamani kutokana na kwamba yeye ni ofisa wa polisi.

Hata hivyo, muda kidogo Jaji Salma Maghimbi aliahirisha kusikilizwa kwa kesi hiyo muda wa nusu saa moja.

Kesi hiyo ya mauaji ya kukusudia inasikilizwa na Jaji Maghimbi ikiwa na washtakiwa saba ambao ni Sharifu Mohamed, Shaibu Jumanne, Musa Mangu, Jalila Zuberi, Karimu Kihundwa, Sadik Mohamed na Ally Musa.

Chanzo: Mwananchi
 
Tangu akiwa mdogo mzungu anasoma kwa anasa. Shuleni Kuna msosi wa nguvu. Achapwi viboko. Akirudi nyumbani mambo swafi. Anachofundishwa anaelewa. Siyo ka sisi jamii ya kisizonje eti lazima usome kwa shida utembee maili kadhaa uchapwe hili ukariri upite mtihani.

Ndio Hapo Sasa Yani kitu ukikibonyeza tu vitu vyenye ncha Kali/butu vinatoka kwenye chamber nakuruka hewani kwa kasi ya ajabu pyu pyu pyu au pah pah.

Lazima wadau ndani ya mahakama waogope

Mzungu hajakariri kasoma Na kuelewa
 
Back
Top Bottom