GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,542
- 108,877
Napenda sana Kazi yako, bidii yako na Ubunifu wako ambao hauna mfano ila Kiingereza chako kinakuharibia na sijui ni kwanini hutaki Kukiboresha wakati Uwezo huo unao na ikijulikana kwamba sasa upo vizuri Kimaisha na Pesa Kwako siyo tatizo tena.
Kwa mara ya Tatu mfululizo nimekuwa nikikusikia hasa ukiwa hewani Clouds fm ukiwa unapata ' taabu ' sana Kuzungumza Lugha ya Kiingereza hasa pale unapokuwa unamfanyia Usaili Mgeni ambaye hazungumzi Kiswahili na mara zote Shukuru Mungu kikiwa Kinakushinda kwa haraka sana huwa ' Unaokolewa ' na Watangazaji wenzako akina Jeff Lea na Nicatius Kotinyo ambao hiyo Lugha ya Kiingereza ni kama vile wamezaliwa nayo kwani wanaizungumza Kiufasaha kabisa.
Na Kinachonishangaza zaidi Kwako Big Boss Shaffih Dauda ni kwamba kila Siku unaonekana Ukichanja tu Mbuga Kutembelea nchi Kubwa mbalimbali duniani lakini nasikitika bado Kiingereza chako ni hiki hiki cha ' Kubabia babia ' kama alichonacho An Eagle ( Mimi ) wakati nilitegemea au nilijua ya kwamba kadri unavyosafiri sana Ng'ambo / Ulaya basi hadi hivi sasa ungekuwa unakizungumza vizuri kabisa.
Hebu nakuomba jitahidi uwe unatenga muda kidogo utafute Chuo Kizuri ili ukajifunze vyema kabisa Kuzungumza na pengine hata Kuandika Kiingereza ili basi usiwe ' unajichoresha ' pale ukiwa unakizungumza ' Mubashara ' katika Kituo chako cha Clouds fm. Kwa Big Boss kama Wewe Kuongeza Kiingereza ' Kibovu ' na cha Kukitafuta kama An Eagle Mimi kunakuharibia CV yako na hata kuwapa Watu wengine Mashaka na Uwezo wako.
Halafu si lazima pia kama unajua kabisa kuwa Kiingereza Kwako ni tatizo kama kilivyo Kwangu Mimi An Eagle basi uwe unang'ang'ania tu Kukizungumza Redioni bali unaweza tu ukawa unawaachia wale wanaokijua vyema kama akina Lea na Kutinyo wazungumze na Wewe Bosi Wao ukawa tu unawasilisha Maswali yako ya Kiswahili Kwao na Wao wanayawasilisha kwa Lugha hiyo ya Kiingereza ambayo wanaijua kweli kweli.
Usikasirike na wala usinikasirikie bali yapokee haya niliyokuambia hapa na yafanyie Kazi upesi. Nakukubali Kinoma ' Baharia ' wangu.