Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 02, 2026, katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Shabiby amesema taarifa hizo si za kweli, akisisitiza kuwa hakuna hata mmoja wao aliyepokea wito kutoka TAKUKURU kama inavyodaiwa.
“Hapana, mimi sijawahi kuitwa, na hata nimemuuliza mwenzangu Kangi Lugola, hakuna mtu ambaye ameitwa. Kama mzalendo na mwakilishi wa wananchi, yale ninayoyafahamu na yanayozungumzwa na wananchi niliyaeleza Bungeni ili mamlaka husika yafanyie utafiti wao kwa kina,” amesema Shabiby.
Ameongeza kuwa taarifa hizo hazikumstua kwani baada ya kuzisoma hakukuwa na sehemu iliyobainisha wazi kuwa aliitwa na TAKUKURU, bali zilieleza tu kuwa endapo kutahitajika, wahusika wanaweza kuitwa.
Soma Pia: TAKUKURU yawaita Shabiby na Kangi Lugola
Shabiby amesema mchango wake wote Bungeni ulizingatia Hotuba ya Rais, akieleza kuwa alinukuu moja kwa moja kutoka kwenye kitabu cha hotuba hiyo, ikiwemo matumizi ya neno mafisadi, jambo linaloondoa hofu yoyote juu ya kile alichokisema.
“Mimi mchango wangu ulifuata Hotuba ya Rais, nilikuwa nasoma na kunukuu kitabu. Kwa hiyo sina hofu yoyote. Hata neno mafisadi lipo kwenye hotuba yenyewe. Mwenye hofu labda awe fisadi kweli,” amesema.